Autocontrole
O autocontrole é fruto do Espírito e virtude indispensável. A graça de Deus nos ensina a renunciar à impiedade e a viver com sobriedade, domínio próprio e piedade no mundo presente.
Fruto e virtude
O domínio próprio é fruto do Espírito. Acrescentai ao conhecimento o autocontrole. A disciplina interior produz maturidade.
Lakini tunda la Roho wa Mungu ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria.
Kwa sababu hii hasa, jitahidini sana katika imani yenu kuongeza wema; na katika wema, maarifa; katika maarifa, kiasi; katika kiasi, saburi; katika saburi, utauwa; katika utauwa, upendano wa kindugu; na katika upendano wa kindugu, upendo.
Kwa maana neema ya Mungu ambayo inawaokoa wanadamu wote imefunuliwa. Nayo inatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ili tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya utaua katika ulimwengu huu wa sasa,
Maana Mungu hakutupatia roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.
La, bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha, ili nikiisha kuwahubiria wengine, nisije nikakataliwa.
Kila mmoja anayeshiriki katika mashindano hufanya mazoezi makali. Wao hufanya hivyo ili wapokee taji lisilodumu, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata taji linalodumu milele.
Hakuna jaribu lolote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Naye Mungu ni mwaminifu; hataruhusu mjaribiwe kupita mnavyoweza. Lakini mnapojaribiwa atawapa njia ya kushinda ili mweze kustahimili.
Dominar a si mesmo
Melhor é quem domina o seu espírito do que quem toma uma cidade. A cidade sem muros é quem não tem autocontrole.
Ni afadhali mtu mstahimilivu kuliko shujaa,
mtu anayeitawala hasira yake kuliko yule autekaye mji.
Kama vile mji ambao kuta zake zimebomoka
ndivyo alivyo mtu
ambaye hawezi kujitawala mwenyewe.
Mpumbavu huonesha hasira yake yote,
bali mwenye hekima hujizuia.
Usigeuke kulia wala kushoto;
epusha mguu wako na ubaya.
Mpumbavu huonesha kuudhika kwake mara moja,
bali mtu wa busara hupuuza matukano.
Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi,
nao wanaoupenda watakula matunda yake.
Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kujaribu ili kuthibitisha mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza na kamilifu machoni pake.
Kusikia na kutenda
Ndugu zangu wapendwa, fahamuni jambo hili: Kila mtu awe mwepesi wa kusikiliza, lakini asiwe mwepesi wa kusema wala wa kukasirika.
Kwa maana kushindana kwetu si dhidi ya mwili na damu, bali dhidi ya falme na mamlaka, dhidi ya wakuu wa ulimwengu huu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
Kwa hiyo basi, tusilale kama watu wengine wanavyolala, bali tukeshe na kuwa na kiasi.
Ayubu anakamilisha maneno yake
"Nimefanya agano na macho yangu
yasimtazame msichana kwa kumtamani.
Jihadharini msije mkapoteza kile mlichokitenda, bali mpate kupewa thawabu kamilifu.