Publicidade

Bom ânimo

Por Bíblia Online

Tende bom ânimo! Jesus repetiu estas palavras aos seus discípulos em meio às tempestades. No mundo tereis aflições, mas Ele já venceu o mundo — e nos dá coragem para enfrentar tudo.

"Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu."

Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakuwa pamoja nawe popote utakapoenda."

Yoshua akawaambia, "Msiogope, wala msivunjike moyo. Kuweni hodari na wenye ushujaa. Hili ndilo Mwenyezi Mungu atakalowatendea adui zenu wote mnaoenda kupigana nao."

Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;

usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.

Nitakutia nguvu na kukusaidia;

nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

Maana Mungu hakutupatia roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.

Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Kuweni hodari na mjipe moyo,

ninyi nyote mnaomtumaini Mwenyezi Mungu.

Nilipoita, ulinijibu;

ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari.

Sala ya kusifu
Zaburi ya Daudi.

Mwenyezi Mungu ni nuru yangu na wokovu wangu,

nimwogope nani?

Mwenyezi Mungu ni ngome ya uzima wangu,

nimhofu nani?

Lakini mara Isa akasema nao, akawaambia, "Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope."

kwa sababu wote walipomwona waliogopa.

Mara Isa akasema nao, akawaambia, "Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!"

Basi Isa akamwambia, "Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani."

Kwa hiyo siku zote tuna ujasiri, hata ingawa tunajua kwamba tukiwa katika mwili huu, tuko mbali na Bwana Isa.

Katika siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba Sulemani akawaaga watu waende nyumbani mwao, wakishangilia na kufurahi mioyoni mwao, kwa wema mwingi Mwenyezi Mungu aliomtendea Daudi na Sulemani na kwa ajili ya watu wake Israeli.

"Kuweni hodari na wenye moyo mkuu. Msiogope, msifadhaike wala msikate tamaa kwa sababu ya mfalme wa Ashuru na hili jeshi kubwa lililo pamoja naye, kwa kuwa aliye pamoja nasi ni mkuu kuliko aliye pamoja naye.

Msemo 25

Ukikata tamaa wakati wa taabu,

jinsi gani nguvu zako ni kidogo!

Hivyo jipeni moyo, enyi watu, kwa kuwa ninamwamini Mungu kwamba yatakuwa kama vile alivyoniambia.

Nina hakika kwamba yeye aliyeianza kazi njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha hata siku ya Al-Masihi Isa.

Katika haya yote mnafurahi sana, ijapokuwa kwa muda mfupi sasa mmehuzunishwa kwa majaribu ya aina nyingi.

Wokovu wa wenye haki hutoka kwa Mwenyezi Mungu,

yeye ni ngome yao wakati wa shida.

Ninatamani sana kuwaona ili nipate kuwapa karama za rohoni ili mwe imara, au zaidi, ninyi pamoja nami tuweze kutiana moyo katika imani sisi kwa sisi.

Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa utu wetu wa nje unachakaa, utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.

Kwa hiyo farijianeni na kujengana, kama vile mnavyofanya sasa.

Kwa hiyo, ndugu zetu, katika dhiki na mateso yetu yote tumefarijika kwa sababu ya imani yenu.

Ndipo hao watu wakajibu, "Hili jambo liwe mbali nasi la kumsahau Mwenyezi Mungu na kuitumikia miungu mingine! Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, mwenyewe ndiye alitutoa sisi na baba zetu akatupandisha kutoka Misri, kutoka nchi ile ya utumwa, na kutenda zile ishara kubwa mbele ya macho yetu. Ndiye aliyetulinda katika safari yetu yote na kutokana na mataifa yote ambayo tulipita katikati yao.

Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu," asema Mwenyezi Mungu, "ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-29_22-07-56-