Publicidade

O que é bom

Por Bíblia Online

O que é bom vem de Deus. A Bíblia celebra a bondade divina e nos convida a discernir, praticar e desfrutar tudo o que é bom — porque toda boa dádiva vem do Pai das luzes.

Mungu akaona vyote alivyoumba, na tazama, vilikuwa vizuri sana. Ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ya sita.

Mwenyezi Mungu ni mwema na mwenye adili,

kwa hiyo huwafundisha wenye dhambi njia zake.

Lakini kwangu mimi,

ni vyema kuwa karibu na Mungu.

Nimemfanya Bwana Mungu Mwenyezi kimbilio langu;

nami nitayasimulia matendo yako yote.

Wimbo wa kumsifu Mwenyezi Mungu

Ni vyema kumshukuru Mwenyezi Mungu

na kuliimbia jina lako, Ee Uliye Juu Sana,

kuutangaza upendo wako asubuhi,

na uaminifu wako wakati wa usiku,

kwa zeze yenye nyuzi kumi

na kwa sauti ya kinubi.

Kwa maana Mwenyezi Mungu ni mwema

na fadhili zake zadumu milele;

uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.

Sifa za pendo la undugu

Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza

ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!

Ninawapa mafundisho ya maana,

kwa hiyo msiyaache mafundisho yangu.

Mtu hupata furaha katika kutoa jibu linalofaa:

je, ni zuri namna gani neno lililotoka kwa wakati wake!

Msemo 26

Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri;

asali kutoka sega ni tamu kwa kuonja.

Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako:

Ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo,

nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali.

Hekima, kama ulivyo urithi, ni kitu chema

na huwafaidia wale walionalo jua.

Mwenyezi Mungu ni mwema kwa wale wanaomtumaini,

na kwa yule anayemtafuta;

ni vyema kungojea kwa utulivu

kwa ajili ya wokovu wa Mwenyezi Mungu.

Amekuonesha yaliyo mema, ee mwanadamu.

Mwenyezi Mungu anataka nini kwako?

Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema,

na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.

Hivyo basi, Torati yenyewe ni takatifu, na amri ni takatifu na ya haki, tena ni njema.

Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kujaribu ili kuthibitisha mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza na kamilifu machoni pake.

Usiruhusu kile ambacho unakiona kuwa chema kisemwe kuwa ni kiovu.

Maagizo kuhusu ibada

Awali ya yote, nasihi kwamba dua, sala, maombezi na shukrani zifanyike kwa ajili ya watu wote: kwa ajili ya wafalme na wale wote walio katika mamlaka, ili tupate kuishi kwa amani na utulivu, katika uchaji wote wa Mungu na utakatifu. Jambo hili ni jema, tena linapendeza machoni pa Mungu Mwokozi wetu,

Kwa maana kila kitu alichokiumba Mungu ni chema, wala hakuna kitu chochote cha kukataliwa kama kikipokewa kwa shukrani, kwa sababu kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.

Kila kitolewacho kilicho chema na kilicho kamili hutoka juu, na hushuka kutoka kwa Baba wa mianga, ambaye kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.

"Chumvi ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake utaifanyaje ili iweze kukolea tena? Mwe na chumvi ndani yenu, mkaishi kwa amani, kila mmoja na mwenzake."

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-