Buscar a Deus
Buscar a Deus é o chamado mais urgente da Bíblia. Buscai primeiro o Reino de Deus. Os que buscam de todo coração encontram — porque Ele se deixa encontrar pelos que o procuram.
Buscai ao Senhor
Buscai ao Senhor enquanto se pode achar. Buscai e achareis. O Senhor recompensa os que o buscam com diligência.
Mtafuteni Mwenyezi Mungu maadamu anapatikana;
mwiteni maadamu yu karibu.
Mtafuteni Mwenyezi Mungu maadamu anapatikana;
mwiteni maadamu yu karibu.
Hukumu na wokovu
"Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakuniulizia.
Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta.
Kwa taifa lile ambalo halikuliita Jina langu,
nilisema, ‘Niko hapa, niko hapa.’
Huwapa nguvu waliolegea
na huongeza nguvu za wadhaifu.
Hata vijana huchoka na kulegea,
nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka,
bali wale wamtumainio Mwenyezi Mungu
atafanya upya nguvu zao.
Watapaa juu kwa mabawa kama tai;
watapiga mbio wala hawatachoka,
watatembea kwa miguu wala hawatazimia.
Mtafuteni Mwenyezi Mungu na nguvu zake;
utafuteni uso wake siku zote.
Mtafuteni Mwenyezi Mungu na nguvu zake;
utafuteni uso wake siku zote.
"Nawe Sulemani mwanangu, mjue Mungu wa baba yako, ukamtumikie kwa kujitoa kwa moyo wote na kwa nia ya kumkubali, kwa maana Mwenyezi Mungu huuchunguza kila moyo na kujua kila kusudi la kila fikira. Ukimtafuta, ataonekana kwako; bali ukimwacha, yeye atakukataa milele.
ikiwa watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekeza na kuomba na kuutafuta uso wangu, na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao, na nitaiponya nchi yao.
Akatoka ili kumlaki Asa na kumwambia, "Nisikilizeni, Asa na Yuda wote na Benyamini. Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi mkiwa pamoja naye. Mkimtafuta, ataonekana kwenu, lakini mkimwacha, naye atawaacha.
Asa afanya matengenezo
Roho wa Mungu akamjia Azaria mwana wa Odedi. Akatoka ili kumlaki Asa na kumwambia, "Nisikilizeni, Asa na Yuda wote na Benyamini. Mwenyezi Mungu yu pamoja nanyi mkiwa pamoja naye. Mkimtafuta, ataonekana kwenu, lakini mkimwacha, naye atawaacha. Kwa muda mrefu Israeli walikuwa hawana Mungu wa kweli, walikuwa hawana kuhani wa kuwafundisha na wala hawakuwa na sheria. Lakini katika taabu yao walimrudia Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, na kumtafuta, naye akaonekana kwao. Katika siku hizo hapakuwa na amani kwa yeyote aliyesafiri, kutoka wala kuingia, kwa kuwa wakazi wote wa nchi walikuwa katika machafuko makubwa. Taifa moja lilipigana na taifa lingine na mji mmoja ukapigana na mji mwingine, kwa sababu Mungu alikuwa anawahangaisha kwa taabu za kila aina. Lakini ninyi, kuweni hodari wala msikate tamaa, kwa kuwa mtapata thawabu kwa kazi yenu."
Asa aliposikia maneno haya na unabii wa Azaria mwana wa Odedi yule nabii, akajipa moyo. Akaziondoa sanamu zote zilizokuwa machukizo katika nchi yote ya Yuda na Benyamini, na kutoka miji aliyoiteka katika nchi ya vilima ya Efraimu. Akakarabati madhabahu ya Mwenyezi Mungu iliyokuwa mbele ya ukumbi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu.
Kisha akakutanisha Yuda wote, Benyamini na watu kutoka Efraimu, watu wa Manase na Simeoni walioishi miongoni mwao, kwa maana idadi kubwa walikuwa wamemjia kutoka Israeli walipoona kwamba Mwenyezi Mungu, Mungu wake, alikuwa pamoja naye.
Basi wakakusanyika huko Yerusalemu mwezi wa tatu katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Asa. Wakati huo wakamtolea Mwenyezi Mungu dhabihu za ng’ombe mia saba, kondoo na mbuzi elfu saba kutoka nyara walizoteka. Wakafanya agano kumtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, kwa moyo wao wote na kwa roho yao yote. Wale wote ambao hawangemtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, wangelazimika kuuawa, akiwa mdogo au mkubwa, mwanaume au mwanamke. Wakamwapia Mwenyezi Mungu kwa sauti kuu, kwa kelele, na kupiga tarumbeta na mabaragumu. Yuda wote wakafurahia kile kiapo kwa sababu walikuwa wameapa kwa moyo wao wote. Wakamtafuta Mungu kwa bidii, naye akaonekana kwao. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akawapa amani pande zote.
Mfalme Asa akamwondolea Maaka, bibi yake, wadhifa wake kama mama malkia kwa sababu alikuwa ametengeneza nguzo ya Ashera ya kuchukiza. Asa akaikata hiyo nguzo, akaivunjavunja na kuiteketeza kwa moto katika Bonde la Kidroni. Ijapokuwa hakuondoa mahali pa juu pa kuabudia katika Israeli, moyo wa Asa ulikuwa umejiweka kwa Mwenyezi Mungu kikamilifu maisha yake yote. Akaleta ndani ya Hekalu la Mungu fedha na dhahabu na vile vyombo ambavyo yeye na baba yake walikuwa wameviweka wakfu.
Hapakuwa na vita tena hadi mwaka wa thelathini na tano wa utawala wake Asa.
De todo o coração
Buscar-me-eis e me achareis quando me buscardes de todo o coração. O Senhor é bom para os que o buscam.
Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wote.
Mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wote.
"Je, neno langu si kama moto," asema Mwenyezi Mungu, "na kama nyundo ivunjayo mwamba vipande vipande?
Lakini kama mtamtafuta Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, mtampata; kama mtamtafuta kwa moyo wote na kwa roho yote.
Heri wale wanaozishika shuhuda zake,
wanaomtafuta kwa moyo wao wote.
Heri wale wanaozishika shuhuda zake,
wanaomtafuta kwa moyo wao wote.
Ninakutafuta kwa moyo wangu wote,
usiniache niende mbali na amri zako.
Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni,
uniimarishe sawasawa na neno lako.
Nitatembea huru,
kwa kuwa nimejifunza mausia yako.
Mtafuteni Mwenyezi Mungu na nguvu zake,
utafuteni uso wake siku zote.
Mtafuteni Mwenyezi Mungu na nguvu zake,
utafuteni uso wake siku zote.
Moyo wangu unasema kuhusu wewe,
"Utafute uso wake!"
Uso wako, Mwenyezi Mungu "Nitautafuta."
Shauku kwa ajili ya uwepo wa Mwenyezi Mungu
Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu,
nakutafuta kwa moyo wote;
nafsi yangu inakuonea kiu,
mwili wangu unakuonea wewe shauku,
katika nchi kame na iliyochoka,
mahali pasipo maji.
Buscar e encontrar
Pedi e dar-se-vos-á. O Senhor está perto de todos os que o invocam em verdade. Quem o busca não ficará insatisfeito.
Omba, tafuta, bisha
"Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango.
Omba, tafuta, bisha
"Kwa hiyo nawaambia: Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa kuwa kila aombaye hupewa; naye kila atafutaye hupata; na kila abishaye hufunguliwa mlango.
Omba, tafuta, bisha
"Kwa hiyo nawaambia: Ombeni nanyi mtapewa; tafuteni nanyi mtapata; bisheni nanyi mtafunguliwa mlango.
Bali utafuteni ufalme wa Mungu, na haya yote atawapa pia.
Kwa maana Mwana wa Adamu amekuja kutafuta na kuokoa kile kilichopotea."
Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe,
kwa maana wewe Mwenyezi Mungu,
hujawaacha kamwe wanaokutafuta.
Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe,
kwa maana wewe Mwenyezi Mungu,
hujawaacha kamwe wanaokutafuta.
Nilimtafuta Mwenyezi Mungu naye akanijibu,
akaniokoa kwenye hofu zangu zote.
Wana simba wenye nguvu
hutindikiwa na kuona njaa,
bali wale wanaomtafuta Mwenyezi Mungu
hawatakosa kitu chochote kilicho chema.
Jifurahishe katika Mwenyezi Mungu
naye atakupa haja za moyo wako.
Mwenyezi Mungu anawachungulia wanadamu
kutoka mbinguni
aone kama kuna mwenye hekima,
yeyote anayemtafuta Mungu.
Mwenyezi Mungu asiyeweza kukwepwa
Ee Mwenyezi Mungu, umenichunguza
na kunijua.
Unajua ninapoketi na ninapoinuka;
unatambua mawazo yangu tokea mbali.
Huyo atapokea baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu,
na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake.
Hiki ndicho kizazi cha wale wanaomtafuta,
wale wanaoutafuta uso wako, Ee Mungu wa Yakobo.
Força na busca
Buscai o bem e não o mal. Sede fortalecidos no Senhor. A busca por Deus traz renovação e plenitude de vida.
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kwa nyumba ya Israeli:
"Nitafuteni mpate kuishi;
Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu kwa nyumba ya Israeli:
"Nitafuteni mpate kuishi;
Tafuteni mema, wala si mabaya,
ili mpate kuishi.
Ndipo Bwana Mwenyezi Mungu,
Mungu wa majeshi ya mbinguni
atakuwa pamoja nanyi,
kama msemavyo yupo nanyi.
Namwomba Mungu awaimarishe kwa kuwatia nguvu mioyo yenu kupitia kwa Roho wake Mtakatifu kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake,
Silaha za Mwenyezi Mungu
Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana Isa na katika uweza wa nguvu zake.
mkiwa mmetiwa nguvu kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu yake yenye utukufu, ili mpate kuwa na wingi wa saburi na uvumilivu. Nanyi kwa furaha
Maana Mungu hakutupatia roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana yeyote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wanaomtafuta kwa bidii.
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana yeyote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wanaomtafuta kwa bidii.
Lakini mtapokea nguvu, Roho wa Mungu akiwajilia juu yenu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na Yudea yote, na Samaria, na miisho ya dunia."
Mwenyezi Mungu na akulipe kwa yale uliyoyatenda. Ubarikiwe kwa wingi na Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, ambaye umekimbilia mabawani mwake."
Roho wa Mwenyezi Mungu akaja juu ya Samsoni kwa nguvu, naye akampasua yule simba kwa mikono mitupu kama ambavyo angempasua mwana-mbuzi, wala hakumwambia baba yake wala mama yake alichokifanya.
Ndipo Samsoni akamwomba Mwenyezi Mungu, akasema, "Ee Bwana Mungu Mwenyezi, unikumbuke. Ee Mungu, nakusihi ukanitie nguvu mara hii moja tu, ili kwa tendo hili nipate kulipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa sababu ya macho yangu mawili."
Ni bora kumkimbilia Mwenyezi Mungu
kuliko kumtumainia mwanadamu.
Ni bora kumkimbilia Mwenyezi Mungu
kuliko kuwatumainia wakuu.
Mtu anayepata mke anapata kitu chema,
naye anajipatia kibali kwa Mwenyezi Mungu.
Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako:
Ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo,
nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali.