Compaixão
A compaixão é o coração de Deus em ação. Ele é compassivo e misericordioso, tardio em irar-se e grande em amor. Somos chamados a refletir essa compaixão no mundo.
Kama baba alivyo na huruma kwa watoto wake,
ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowahurumia wale wanaomcha;
Lakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema,
si mwepesi wa hasira,
bali ni mwingi wa upendo na uaminifu.
Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai,
midomo yangu itakuadhimisha.
Kwa sababu ya upendo mkuu wa Mwenyezi Mungu, hatuangamii,
kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.
Ni mpya kila asubuhi,
uaminifu wako ni mkuu.
"Je, mama aweza kumsahau mtoto
aliye matitini mwake akinyonya,
wala asiwe na huruma
juu ya mtoto aliyemzaa?
Ingawa anaweza kusahau,
mimi sitakusahau wewe!
Tazama, nimekuchora kama muhuri
katika vitanga vya mikono yangu,
kuta zako zi mbele yangu daima.
Hata hivyo Mwenyezi Mungu anatamani kutupatia neema,
anainuka ili kuwaonesha huruma.
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni Mungu wa haki.
Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!
Ni nani Mungu kama wewe,
ambaye anaachilia dhambi
na kusamehe makosa
ya mabaki ya urithi wake?
Wewe huwi na hasira milele,
bali unafurahia kuonesha rehema.
"Nitaiimarisha nyumba ya Yuda
na kuiokoa nyumba ya Yusufu.
Nitawarejesha kwa sababu
nina huruma juu yao.
Watakuwa kama watu ambao
sijawahi kuwakataa
kwa sababu mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wao,
nami nitawajibu.
"Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: ‘Fanyeni hukumu za haki, onesheni rehema na huruma ninyi kwa ninyi. Msimdhulumu mjane wala yatima, mgeni wala maskini. Msiwaziane mabaya mioyoni mwenu ninyi kwa ninyi.’
Basi, kwa kuwa ninyi mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wanaopendwa sana, jivikeni moyo wa huruma, utu wema, unyenyekevu, upole na uvumilivu.
Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Al-Masihi alivyowasamehe ninyi.
Kuteseka kwa kutenda mema
Hatimaye, ninyi nyote kuweni na nia moja, wenye kuhurumiana, mkipendana kama ndugu, mkijaliana, na wanyenyekevu.
Ikiwa mtu anavyo vitu vya ulimwengu huu na akamwona ndugu yake ni mhitaji lakini asimhurumie, upendo wa Mungu wakaaje ndani ya mtu huyo?
Mungu wa faraja yote
Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Isa Al-Masihi, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote. Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu.
Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuliana na sisi katika udhaifu wetu, lakini tunaye mmoja ambaye alijaribiwa kwa kila namna, kama vile sisi tujaribiwavyo: lakini yeye hakutenda dhambi.
Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wale waliao.
Salamu za mwisho
Hatimaye, ndugu zangu, kwaherini. Kuweni wakamilifu, farijianeni, kuweni na nia moja, na mkae kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
Este artigo te tocou? Faça uma oração!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.