Compreensão
A verdadeira compreensão vem de Deus. Os caminhos do Senhor são mais altos que os nossos. Mas Ele nos convida a buscar entendimento — e promete iluminar quem o busca de coração.
A sabedoria de Deus
Os meus pensamentos não são os vossos pensamentos. A incompreensibilidade de Deus nos leva à humildade e adoração.
"Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia,
ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu
na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
"Ole wake yeye ashindanaye na Muumba wake,
yeye ambaye ni kigae tu kati ya vigae juu ya ardhi.
Je, udongo wa kufinyangia humwambia mfinyanzi,
‘Unatengeneza nini wewe?’
Je, kazi yako husema,
‘Hana mikono’?
Je wewe, hufahamu?
Je wewe, hujasikia?
Mwenyezi Mungu ni Mungu wa milele,
Muumba wa miisho ya dunia.
Hatachoka wala kulegea,
wala hakuna hata mmoja
awezaye kuupima ufahamu wake.
Mwenyezi Mungu ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana,
ukuu wake haupimiki.
Kabla ya kuzaliwa milima
au hujaumba dunia na ulimwengu,
wewe ni Mungu tangu milele hata milele.
Kwa maana kwako miaka elfu
ni kama siku moja iliyokwisha pita,
au kama kesha la usiku.
Tazama jinsi kilivyo kina cha utajiri
wa hekima na maarifa ya Mungu!
Tazama jinsi hukumu zake hazichunguziki,
na ambavyo njia zake hazitafutiki!
Buscar entendimento
Clama a mim e responder-te-ei. A sabedoria é a coisa principal — busque o entendimento com todo o coração.
‘Niite, nami nitakuitikia, nitakuonesha mambo makubwa, yasiyochunguzika na usiyoyajua.’
Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima.
Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu.
Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi,
bali anayekasirika haraka huonesha upumbavu.
Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu,
lakini kusudi la Mwenyezi Mungu ndilo litakalosimama.
Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake,
bali Mwenyezi Mungu huupima moyo.
Nazidi kumwomba Mungu wa Bwana wetu Isa Al-Masihi, Baba wa utukufu, awajalieni ninyi roho ya hekima na ya ufunuo, ili mpate kumjua zaidi.
Bali kueni katika neema na katika kumjua Bwana na Mwokozi wetu Isa Al-Masihi.
Utukufu una yeye sasa na milele! Amen.
Iluminação divina
A entrada da tua Palavra dá luz e entendimento. Deus revela verdades ocultas e transforma nossa visão da realidade.
Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru,
kunampa mjinga ufahamu.
Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea;
nitakushauri na kukuangalia.
Kama vile usivyofahamu njia ya upepo,
au jinsi mwili uumbwavyo
ndani ya tumbo la mama,
vivyo hivyo huwezi kufahamu kazi ya Mungu,
Muumba wa vitu vyote.
Isa akamjibu, "Amin, amin nakuambia, hakuna mtu anayeweza kuuona ufalme wa Mungu kama hajazaliwa mara ya pili."
Lakini Isa akawatazama, akawaambia, "Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini mambo yote yanawezekana kwa Mungu."
Akaketi chini, akawaita wote kumi na wawili, akawaambia: "Kama mtu yeyote akitaka kuwa wa kwanza, hana budi kuwa wa mwisho na mtumishi wa wote."
Wala hakuna tena Myahudi au Myunani, mtumwa au mtu huru, mwanaume wala mwanamke, maana nyote mmekuwa wamoja ndani ya Al-Masihi Isa. Nanyi mkiwa ni mali ya Al-Masihi, basi ninyi ni wa uzao wa Ibrahimu na warithi sawasawa na ile ahadi.
Jaribuni kila kitu. Yashikeni yaliyo mema. Jiepusheni na uovu wa kila namna.
Ingawa tunaishi duniani, hatupigani vita kama ulimwengu ufanyavyo.
Kwa hivyo hatuangalii yale yanayoonekana, bali yale yasiyoonekana. Kwa maana yale yanayoonekana ni ya kitambo tu, bali yale yasiyoonekana ni ya milele.
Mtu anapojaribiwa asiseme, "Ninajaribiwa na Mungu." Kwa maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu wala yeye hamjaribu mtu yeyote.