Pular para o conteúdo
Publicidade

Comunhão com os irmãos

Por Bíblia Online

A comunhão com os irmãos é marca da igreja verdadeira. Os cristãos primevos perseveravam na comunhão — partindo pão, orando e encorajando-se mutuamente.

Comunhão verdadeira

Perseveravam na doutrina dos apóstolos e na comunhão. A comunhão autêntica envolve amor sacrificial e acolhimento mútuo.

Wale wote waliopokea ujumbe wa Petro kwa furaha wakabatizwa, na siku ile waliongezeka watu wapatao elfu tatu.

Ushirika wa waumini

Nao wakadumu katika mafundisho ya mitume, katika ushirika, katika kumega mkate na katika kusali. Kila mtu akaingiwa na hofu ya Mungu, nayo miujiza mingi na ishara zikafanywa na mitume. Waumini wote walikuwa mahali pamoja, nao wakashirikiana katika mambo yote. Waliuza mali yao na vitu walivyokuwa navyo, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake. Siku zote kwa moyo mmoja walikutana ndani ya ukumbi wa Hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, wakila chakula chao kwa furaha na moyo mweupe, wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana akaliongeza kundi la waumini wa Isa wale waliokuwa wakiokolewa.

Tuangaliane na kuhimizana sisi kwa sisi katika upendo na katika kutenda mema. Wala tusiache kukutana pamoja, kama wengine walivyo na desturi, bali tuhimizane sisi kwa sisi kadiri tuonavyo Siku ile inakaribia.

Sifa za pendo la undugu

Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza

ndugu wanapoishi pamoja katika umoja!

Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani,

yakitiririka kwenye ndevu,

yakitiririka kwenye ndevu za Haruni,

hadi kwenye upindo wa mavazi yake.

Ni kama umande wa Hermoni

ukianguka juu ya Mlima Sayuni.

Kwa maana huko ndiko Mwenyezi Mungu alikoamuru baraka yake,

naam, uzima hata milele.

ambaye awali tulifurahia ushirika mzuri,

tulipokuwa tukienda na umati hekaluni mwa Mungu.

Wawili ni afadhali kuliko mmoja,

kwa sababu wana malipo mazuri kwa kazi yao:

Kama mmoja akianguka,

mwenzake atamwinua.

Lakini ni jambo la kuhuzunisha

kwa mtu yule aangukaye

naye hana wa kumwinua!

Pia, kama wawili wakilala pamoja

watapashana joto.

Lakini ni vipi mtu aweza

kujipasha joto mwenyewe?

Ingawa mtu mmoja aweza kushindwa,

watu wawili wanaweza

kumkabili adui na kumshinda.

Kamba ya nyuzi tatu

haikatiki kwa urahisi.

Amor fraternal

Amai-vos com amor fraternal sincero. Encorajem-se mutuamente e carreguem os fardos uns dos outros.

Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli hata mkawa na upendo wa ndugu usio na unafiki, basi pendaneni kwa dhati kutoka moyoni.

Kuweni wakarimu kila mtu na mwenzake pasipo manung’uniko.

Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa ndugu. Waheshimuni na kuwatanguliza wengine.

Kuiga unyenyekevu wa Al-Masihi

Kama kukiwa na jambo lolote la kutia moyo katika kuunganishwa na Al-Masihi, kukiwa faraja yoyote katika upendo wake, kukiwa na ushirika wowote na Roho wa Mungu, kukiwa na wema wowote na huruma, basi ikamilisheni furaha yangu kwa kuwa na nia moja, mkiwa na upendo huo moja, mkiwa wa roho na kusudi moja.

Neno la Al-Masihi na likae kwa wingi ndani yenu, mkifundishana na kuonyana katika hekima yote, mkimwimbia Mungu zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, huku mkiwa na shukrani mioyoni mwenu.

Kuweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi kwa ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Al-Masihi alivyowasamehe ninyi.

Ndugu zangu, ninyi mliitwa ili mwe huru, hivyo msitumie uhuru wenu kama fursa ya kufuata tamaa za mwili, bali tumikianeni ninyi kwa ninyi kwa upendo.

Kwa hiyo farijianeni na kujengana, kama vile mnavyofanya sasa.

Tukisema kwamba twashirikiana naye huku tukienenda gizani, twasema uongo, wala hatutendi lililo kweli. Lakini tukienenda nuruni, kama yeye alivyo nuruni, twashirikiana sisi kwa sisi na damu yake Isa, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.

Salamu za mwisho

Hatimaye, ndugu zangu, kwaherini. Kuweni wakamilifu, farijianeni, kuweni na nia moja, na mkae kwa amani. Naye Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.

"Amri mpya nawapa: Mpendane. Kama mimi nilivyowapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi mpendane.

Seja o primeiro