Publicidade

Confiança

Por Bíblia Online

A confiança em Deus é âncora da alma em tempos de tempestade. Quem confia no Senhor não será abalado — porque o Deus fiel sustenta, protege e guia os que nele esperam.

Confiança inabalável

Tudo posso naquele que me fortalece. O meu Deus suprirá toda necessidade. Quem confia não será confundido.

Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Naye Mungu wangu atawajaza ninyi na kila mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya Al-Masihi Isa.

Nina hakika kwamba yeye aliyeianza kazi njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha hata siku ya Al-Masihi Isa.

Upendo wa Mwenyezi Mungu

Tuseme nini basi kuhusu haya? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani awezaye kuwa kinyume chetu?

wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chochote zitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Al-Masihi Isa, Bwana wetu.

Mwenyezi Mungu mlinzi wetu

Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana,

atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.

Nitasema kumhusu Mwenyezi Mungu, "Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu,

Mungu wangu, ninayemtumaini."

Wokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu,

ndiye mwamba wangu wenye nguvu

na kimbilio langu.

Wakati ninaogopa,

nitakutumaini wewe.

Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu,

katika Mungu ninatumaini, sitaogopa.

Mwanadamu mwenye kufa

atanitenda nini?

Fundamento de confiança

Deus não é homem para que minta. Todas as suas promessas são firmes. Confiar em Deus é segurança absoluta.

Mungu si mtu, hata aseme uongo,

wala yeye si mwanadamu, hata ajute.

Je, anasema, kisha asitende?

Je, anaahidi, asitimize?

Yalindeni maisha yenu msiwe na tabia ya kupenda fedha, bali mridhike na vile mlivyo navyo, kwa sababu Mungu amesema,

"Kamwe sitakuacha,

wala sitakupungukia."

Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri,

"Mwenyezi Mungu ni msaada wangu; sitaogopa.

Mwanadamu anaweza kunitenda nini?"

Shika kwa uthabiti kielelezo cha mafundisho yenye uzima uliyoyasikia kwangu, pamoja na imani na upendo katika Al-Masihi Isa.

Askari mwema wa Al-Masihi Isa

Basi wewe, mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo ndani ya Al-Masihi Isa.

Mtumaini Mwenyezi Mungu kwa moyo wako wote

wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

katika njia zako zote mkiri yeye,

naye atayanyoosha mapito yako.

Mtumaini Mwenyezi Mungu kwa moyo wako wote

wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

katika njia zako zote mkiri yeye,

naye atayanyoosha mapito yako.

Mkabidhi Mwenyezi Mungu lolote ufanyalo,

nayo mipango yako itafanikiwa.

Yeyote anayekubali mafundisho hustawi,

tena amebarikiwa yeye anayemtumaini Mwenyezi Mungu.

Kuwaogopa watu huwa ni mtego,

bali yeyote amtumainiaye Mwenyezi Mungu atakuwa salama.

Confiar em todas as coisas

Não pertenço ao mundo — minha cidadania é do céu. A confiança cristã repousa na fidelidade de Deus, não nas circunstâncias.

Yafikirini mambo yaliyo juu, wala si ya duniani.

Isa akamwambia, "Ati, Kama unaweza kufanya jambo lolote? Yote yawezekana kwake yeye aaminiye."

Isa akajibu, "Yasiyowezekana kwa wanadamu yanawezekana kwa Mungu."

Waangalieni ndege wa angani; wao hawapandi wala hawavuni au kuweka ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, ninyi si wa thamani kuliko hao ndege?

"Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu."

"Lakini amebarikiwa mtu anayemtumaini Mwenyezi Mungu,

ambaye matumaini yake ni katika Mwenyezi Mungu.

Atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji

uenezao mizizi yake karibu na kijito cha maji.

Hauogopi wakati wa joto ujapo;

majani yake ni mabichi daima.

Hauna hofu katika mwaka wa ukame

na hautaacha kuzaa matunda."

Unapopita kwenye maji makuu,

nitakuwa pamoja nawe,

unapopita katika mito ya maji,

hayatakugharikisha.

Utakapopita katika moto,

hutaungua,

miali ya moto haitakuunguza.

Huu ndio ujasiri tulio nao tunapomkaribia Mungu, kwamba tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.

Huu ndio ujasiri tulio nao tunapomkaribia Mungu, kwamba tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.

Hivyo nasi twajua na kulitumainia pendo la Mungu alilo nalo kwa ajili yetu.

Mungu ni Upendo. Kila akaaye katika upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake.

Zijaribuni roho

Wapendwa, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea ulimwenguni.

Esperar com confiança

O Senhor está perto de todos os que o invocam. Na espera confiante encontramos descanso e direção divina.

Mwenyezi Mungu yu karibu na wote wamwitao,

karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.

Asubuhi uniletee neno la upendo wako usiokoma,

kwa kuwa nimeweka tumaini langu kwako.

Nioneshe njia nitakayoiendea,

kwa kuwa kwako nainua nafsi yangu.

Hatauacha mguu wako uteleze,

yeye akulindaye hatasinzia,

Mtumaini Mwenyezi Mungu na utende yaliyo mema.

Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.

Tazama jinsi wema wako ulivyo mkuu,

uliowawekea akiba wanaokucha,

unaowapa wale wanaokukimbilia

machoni pa watu wote.

Nani niliye naye mbinguni ila wewe?

Dunia haina chochote ninachokitamani ila wewe.

Acheni saburi ikamilishe kazi yake, ili mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote.

Lakini anapoomba, lazima aamini wala asiwe na shaka, kwa sababu mtu aliye na shaka ni kama wimbi la bahari, linalopeperushwa na upepo na kutupwa huku na huko.

Kwa maana twaenenda kwa imani wala si kwa kuona.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-