Pular para o conteúdo
Publicidade

Consequências dos nossos atos

Por Bíblia Online

Toda ação tem consequências. A Bíblia ensina que colhemos o que semeamos — para o bem e para o mal. Deus pesará cada palavra e ato no dia do juízo.

Colher o que semear

Cada um prestará contas de si mesmo a Deus. O Senhor julgará as obras e os segredos dos homens com justiça perfeita.

Hivyo basi kila mmoja wetu atatoa habari zake mwenyewe kwa Mungu.

Kwa maana Mungu atamlipa kila mtu kulingana na matendo yake. Wale ambao kwa kuvumilia katika kutenda mema hutafuta utukufu, heshima na maisha yasiyoharibika, Mungu atawapa uzima wa milele. Lakini kwa wale wanaotafuta mambo yao wenyewe na wale wanaokataa kweli na kuzifuata njia mbaya, kutakuwa na ghadhabu na hasira ya Mungu. Kutakuwa na taabu na dhiki kwa kila mmoja atendaye maovu, Myahudi kwanza na mtu wa Mataifa pia, bali utukufu, heshima na amani kwa ajili ya kila mmoja atendaye mema, kwa Myahudi kwanza, kisha kwa mtu wa Mataifa. Kwa maana Mungu hana upendeleo.

Tena ile karama ya Mungu haiwezi kulinganishwa na matokeo ya ile dhambi ya mtu mmoja. Kwani hukumu ilikuja kupitia kwa dhambi ya mtu mmoja, ikaleta adhabu; lakini ile karama ilikuja baada ya makosa mengi, ikaleta kuhesabiwa haki. Kwa maana ikiwa kutokana na kosa la mtu mmoja, mauti ilitawala kupitia huyo mtu mmoja, zaidi sana wale wanaopokea wingi wa neema ya Mungu na karama yake ya kuhesabiwa haki, watatawala katika uzima kupitia kwa huyo mtu mmoja, yaani Isa Al-Masihi.

Kuwahukumu wengine

"Usihukumu ili usije ukahukumiwa. Kwa maana jinsi unavyowahukumu wengine, ndivyo utakavyohukumiwa, na kwa kipimo kile upimiacho, ndicho utakachopimiwa.

Lakini nawaambia, katika siku ya hukumu watu watatoa maelezo kuhusu kila neno walilonena lisilo la maana.

Kwa maana neno la Mungu li hai tena lina nguvu. Lina makali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili, hivyo linachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, viungo na mafuta yaliyo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Wala hakuna kiumbe chochote kilichofichika machoni pa Mungu. Kila kitu kimefunuliwa na kiko wazi machoni pake yeye ambaye lazima tutawajibika kwake.

Responsabilidade pessoal

Quem é sábio prevê o perigo e se esconde. A Palavra examina os pensamentos e intenções do coração.

Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha,

bali mjinga huendelea mbele, naye hupata madhara.

Kama wewe una hekima, hekima yako itakupa tuzo;

kama wewe ni mtu wa mzaha,

wewe mwenyewe ndiwe utateseka."

Ni mtego kwa mtu kuweka wakfu kitu kwa haraka

na baada ya kitambo kidogo kufikiria tena nadhiri zake.

Sadaka zingine za kuondoa dhambi

" Ikiwa mtu ametenda dhambi kwa sababu hakusema alipotakiwa kutoa ushahidi hadharani kuhusu jambo aliloona au kujua habari zake, yeye atastahili adhabu.

"Kama mtu akifanya dhambi, na kutenda yaliyokatazwa katika mojawapo ya amri za Mwenyezi Mungu, hata ikiwa hajui, yeye ana hatia na anastahili adhabu.

" Usimchukie ndugu yako moyoni mwako. Karipia jirani yako kwa uwazi ili usishiriki hatia yake.

Consequências inevitáveis

A terra deu seu fruto conforme as obras dos que nela habitam. Ninguém escapa do juízo — Deus pesa cada ação.

Dunia itakuwa ukiwa kwa sababu ya wakazi wake,

kwa sababu ya matunda ya matendo yao.

Utapata adhabu kwa ajili ya uasherati wako na kuchukua matokeo ya dhambi zako za uasherati. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana Mungu Mwenyezi."

Hakika damu ya uhai wenu nitaidai. Nitaidai kutoka kwa kila mnyama. Kutoka kwa kila mwanadamu pia nitaidai kwa ajili ya uhai wa binadamu mwenzake.

Kwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu?

Kwa nini anajiambia mwenyewe,

"Hataniita nitoe hesabu"?

Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni,

umekubali kuyapokea mkononi mwako.

Mhanga anajisalimisha kwako,

wewe ni msaada wa yatima.

Seja o primeiro