Publicidade

Conversão

Por Bíblia Online

A conversão é o ato de se voltar para Deus — arrependendo-se do pecado e abraçando a graça. É o início de uma vida nova, transformada pelo amor de Cristo.

Arrependei-vos

Arrependei-vos e convertei-vos para que os vossos pecados sejam apagados. A conversão começa com a mudança de mente e coração.

Tubuni basi mkamgeukie Mungu, dhambi zenu zifutwe, ili zipate kuja nyakati za kuburudishwa kutoka kwake Mwenyezi Mungu,

Petro akawajibu, "Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Isa Al-Masihi, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho wa Mungu.

Zamani wakati wa ujinga, Mungu alijifanya kama haoni, lakini sasa anawaamuru watu wote kila mahali watubu.

Tangu wakati huo, Isa alianza kuhubiri akisema: "Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia."

Basi zaeni matunda yastahiliyo toba.

akisema, "Wakati umetimia, ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Injili."

O amor de Deus converte

Céu se alegra por um pecador que se arrepende. Deus não deseja a morte do ímpio, mas que se converta e viva.

Nawaambieni, vivyo hivyo kutakuwa na furaha zaidi mbinguni kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu.

Vivyo hivyo, nawaambia, kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu juu ya mwenye dhambi mmoja atubuye."

Sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu."

Kwa maana sifurahii kifo cha mtu yeyote, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Tubuni basi, mkaishi!

"Lakini mtu mwovu akiacha dhambi zake zote alizozitenda na kushika amri zangu zote na kufanya lililo haki na sawa, hakika ataishi, hatakufa.

Atendaye dhambi atakufa

Neno la Mwenyezi Mungu likanijia kusema: "Je, ninyi watu mna maana gani kutumia mithali hii inayohusu nchi ya Israeli:

" Baba wamekula zabibu chachu,

nayo meno ya watoto yametiwa ganzi?

"Hakika kama niishivyo, asema Bwana Mungu Mwenyezi, hamtatumia tena mithali hii katika Israeli. Kwa kuwa kila roho ni mali yangu; kama vile ilivyo roho ya baba, vivyo hivyo roho ya mtoto ni mali yangu. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa.

"Mtu aweza kuwa ni mwenye haki

atendaye yaliyo haki na sawa.

Hakula katika mahali pa ibada za sanamu

kwenye milima,

wala hakuziinulia macho sanamu

za nyumba ya Israeli.

Hakumtia unajisi mke wa jirani yake,

wala hakukutana kimwili na mwanamke

wakati wa siku zake za hedhi.

Hamdhulumu yeyote,

bali hurudisha kilichowekwa rehani kwake.

Hanyang’anyi, bali huwapa wenye njaa chakula chake

na huwapa nguo walio uchi.

Hakopeshi kwa riba

wala hajipatii faida ya ziada.

Huuzuia mkono wake usifanye mabaya,

naye huhukumu kwa haki kati ya mtu na mtu.

Huzifuata amri zangu

na kuzishika sheria zangu kwa uaminifu.

Huyo mtu ni mwenye haki;

hakika ataishi,

asema Bwana Mungu Mwenyezi.

"Aweza kuwa ana mwana jeuri, amwagaye damu au atendaye mojawapo ya mambo haya (ingawa baba yake hakufanya mojawapo ya haya):

"Hula katika mahali pa ibada za sanamu kwenye milima.

Humtia unajisi mke wa jirani yake.

Huwadhulumu maskini na wahitaji.

Hunyang’anyana.

Harudishi kile kilichowekwa rehani kwake.

Huziinulia sanamu macho.

Hufanya mambo ya machukizo.

Hukopesha kwa riba na kutafuta faida ya ziada.

Je, mtu wa namna hii ataishi? Hapana, hataishi! Kwa sababu amefanya mambo haya yote ya machukizo, hakika atauawa na damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.

"Lakini yawezekana mwana huyo ana mwana aonaye dhambi hizi zote anazofanya baba yake, naye ingawa anaziona, yeye hafanyi mabaya kama haya:

"Hakula katika mahali pa ibada za sanamu

kwenye milima,

wala hainulii macho sanamu

za nyumba ya Israeli.

Hakumtia unajisi

mke wa jirani yake.

Hamdhulumu yeyote

wala kutaka rehani kwa ajili ya mkopo.

Hanyang’anyi,

bali huwapa wenye njaa chakula chake

na huwapa nguo walio uchi.

Huuzuia mkono wake usitende dhambi,

hakopeshi kwa riba

wala hajipatii faida ya ziada.

Huzishika amri zangu

na kuzifuata sheria zangu.

Hatakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake; hakika ataishi. Lakini baba yake atakufa kwa ajili ya dhambi yake mwenyewe, kwa sababu alikuwa mnyang’anyi, akampokonya ndugu yake na kufanya yaliyo mabaya miongoni mwa watu wake.

"Lakini mnauliza, Kwa nini mwana asiadhibiwe kwa uovu wa baba yake?Kwa vile mwana ametenda yaliyo haki na sawa na amekuwa mwangalifu kuzishika amri zangu zote, hakika ataishi. Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. Mwana hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya baba yake, wala baba hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya mwanawe. Haki ya mtu mwenye haki itahesabiwa juu yake na uovu wa mtu mwovu utalipizwa juu yake.

"Lakini mtu mwovu akiacha dhambi zake zote alizozitenda na kushika amri zangu zote na kufanya lililo haki na sawa, hakika ataishi, hatakufa. Hakuna kosa lolote alilotenda litakalokumbukwa juu yake. Kwa ajili ya mambo ya haki aliyoyatenda, ataishi. Je, mimi ninafurahia kifo cha mtu mwovu? Asema Bwana Mungu Mwenyezi. Je, si mimi ninafurahi wanapogeuka kutoka njia zao mbaya na kuishi?

"Lakini kama mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda dhambi na kufanya mambo ya machukizo ambayo mtu mwovu hufanya, Je, ataishi? Hakuna hata mojawapo ya matendo ya haki aliyotenda litakalokumbukwa. Kwa sababu ya kukosa uaminifu kwake anayo hatia na kwa sababu ya dhambi alizozitenda, atakufa.

"Lakini mnasema, Njia ya Bwana si ya haki.Sikia, ee nyumba ya Israeli: Je, njia yangu siyo ya haki? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki? Kama mtu mwenye haki akiacha haki yake na kutenda dhambi, atakufa kwa ajili ya dhambi yake, kwa sababu ya dhambi alizotenda, atakufa. Lakini mtu mwovu akigeuka kutoka maovu aliyoyatenda na kufanya yaliyo haki na sawa, ataokoa maisha yake. Kwa kuwa anayafikiria na kugeuka kutoka makosa yake yote aliyoyatenda na kuyaacha, hakika ataishi, hatakufa. Lakini nyumba ya Israeli inasema, Njia za Bwana si haki.Je, njia zangu si za haki, ee nyumba ya Israeli? Je, si njia zenu ndizo ambazo si za haki?

"Kwa hiyo, ee nyumba ya Israeli, nitawahukumu, kila mmoja sawasawa na njia zake, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Tubuni! Geukeni kutoka makosa yenu yote, ndipo dhambi haitakuwa anguko lenu. Tupilieni mbali makosa yenu yote mliyoyatenda, nanyi mpate moyo mpya na roho mpya. Kwa nini mfe, ee nyumba ya Israeli? Kwa maana sifurahii kifo cha mtu yeyote, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Tubuni basi, mkaishi!

Mwenyezi Mungu hakawii kuitimiza ahadi yake, kama watu wengine wanavyokudhani kukawia. Badala yake, yeye anawavumilia ninyi, maana hataki mtu yeyote aangamie, bali kila mtu afikilie toba.

Transformação

Voltai-vos para mim e sereis salvos! Rasgai o coração e não as vestes. A verdadeira conversão transforma o interior.

Mtu mwovu na aiache njia yake,

na mtu mbaya na ayaache mawazo yake.

Yeye na amrudie Mwenyezi Mungu, naye atamrehemu,

arudi kwa Mungu wetu, kwa kuwa atamsamehe bure kabisa.

Nimeyafuta makosa yako kama wingu,

dhambi zako kama ukungu wa asubuhi.

Nirudie mimi,

kwa kuwa nimekukomboa wewe."

Rarueni mioyo yenu

"Hata sasa," asema Mwenyezi Mungu,

"nirudieni kwa mioyo yenu yote,

kwa kufunga, kwa kulia na kuomboleza."

Rarueni mioyo yenu

na siyo mavazi yenu.

Mrudieni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu,

kwa maana yeye ndiye mwenye neema

na mwingi wa huruma,

si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa upendo,

huona huruma, hujizuia kuleta maafa.

ikiwa watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekeza na kuomba na kuutafuta uso wangu, na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao, na nitaiponya nchi yao.

Hezekia aadhimisha Pasaka

Hezekia akatuma ujumbe kuwaita Israeli wote na Yuda, pia akaandika barua kwa Efraimu na Manase, kuwakaribisha ili waje hekaluni mwa Mwenyezi Mungu huko Yerusalemu kuadhimisha Pasaka kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. Mfalme na maafisa wake pamoja na kusanyiko lote katika Yerusalemu waliamua kuadhimisha Pasaka katika mwezi wa pili. Kwa sababu makuhani hawakuwa wamejitakasa ya kutosha na watu wakawa hawajakusanyika huko Yerusalemu, hawakuwa wameweza kuadhimisha Pasaka kwa wakati wake wa kawaida. Mpango huu ukaonekana wafaa kwa mfalme na kusanyiko lote. Wakaamua kupeleka tangazo Israeli kote, kuanzia Beer-Sheba hadi Dani, wakiwaita watu waje Yerusalemu kuadhimisha Pasaka ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli. Ilikuwa haijaadhimishwa na idadi kubwa ya watu kama hiyo kufuatana na yale yaliyokuwa yameandikwa.

Kwa amri ya mfalme, matarishi wakazunguka Israeli na Yuda kote wakiwa na barua kutoka kwa mfalme na kutoka kwa maafisa wake, zilizoandikwa:

"Watu wa Israeli, mrudieni Mwenyezi Mungu, Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Israeli, ili naye awarudie ninyi mliosalia, mlionusurika kutoka mikononi mwa wafalme wa Ashuru. Msiwe kama baba zenu na ndugu zenu, ambao hawakuwa waaminifu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao, hivyo akawafanya kitu cha kutisha, kama mnavyoona. Msiwe na shingo ngumu, kama baba zenu walivyokuwa, bali nyenyekeeni kwa Mwenyezi Mungu. Njooni mahali patakatifu, alipopatakasa milele. Mtumikieni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ili hasira yake kali igeuziwe mbali nanyi. Mkimrudia Mwenyezi Mungu, ndipo wale ndugu zenu waliotekwa pamoja na watoto wenu watakapoonewa huruma na wale waliowateka na kuwaachia warudi katika nchi hii, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ni mwenye neema na huruma, hatageuzia uso wake mbali nanyi kama mkimrudia yeye."

Matarishi wakaenda mji hadi mji katika Efraimu na Manase, wakafika Zabuloni, lakini watu wakawadharau na kuwadhihaki. Lakini, baadhi ya watu wa Asheri, Manase na Zabuloni, wakajinyenyekeza wakaja Yerusalemu. Pia katika Yuda mkono wa Mungu ulikuwa juu ya watu kuwapa umoja katika kutenda yale ambayo mfalme na maafisa wake waliwaamuru, kulingana na neno la Mwenyezi Mungu.

Basi umati mkubwa wa watu wakakusanyika huko Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu katika mwezi wa pili. Wakajitia kazini kuyaondoa yale madhabahu yaliyokuwa huko Yerusalemu, wakayaondoa pia yale madhabahu ya kufukizia uvumba kwa miungu na kuyatupa Bonde la Kidroni.

Kisha wakamchinja mwana-kondoo wa Pasaka katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili. Makuhani na Walawi waliona aibu, wakajitakasa na kuleta sadaka za kuteketezwa katika Hekalu la Mwenyezi Mungu. Kisha wakachukua nafasi zao za kawaida kama ilivyoelezwa katika Torati ya Musa mtu wa Mungu. Makuhani wakanyunyiza ile damu waliyokabidhiwa na Walawi. Kwa kuwa wengi waliokuwa katika lile kusanyiko walikuwa hawajajitakasa, iliwapasa Walawi wachinje wana-kondoo wengine wa Pasaka kwa ajili ya wale watu ambao hawakuwa wametakaswa, ili kuwatakasa kwa Mwenyezi Mungu. Ingawa watu wengi miongoni mwa wale waliotoka Efraimu, Manase, Isakari na Zabuloni walikuwa hawajajitakasa, hata hivyo walikula Pasaka kinyume na ilivyoandikwa. Lakini Hezekia akawaombea, akisema, "Mwenyezi Mungu, ambaye ni mwema na amsamehe kila mmoja ambaye anauelekeza moyo wake kumtafuta Mungu, Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zake, hata kama yeye si safi kulingana na sheria za mahali patakatifu." Naye Mwenyezi Mungu akamsikia Hezekia akawaponya watu.

Waisraeli waliokuwa Yerusalemu wakaadhimisha Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu kwa muda wa siku saba, nao Walawi na makuhani walikuwa wakiimba kila siku, wakiwa na ala za uimbaji za kumsifu Mwenyezi Mungu.

Hezekia akazungumza akiwatia moyo Walawi wote, ambao walionesha ustadi katika kumtumikia Mwenyezi Mungu. Hivyo watu wakala chakula cha sikukuu kwa siku saba, wakitoa sadaka za amani na kumshukuru Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba zao.

Kisha kusanyiko lote wakakubali kuendelea na sikukuu kwa siku saba zaidi; kwa hiyo, kwa siku saba nyingine wakaendelea kuiadhimisha kwa furaha. Hezekia, mfalme wa Yuda akatoa mafahali elfu moja, kondoo na mbuzi elfu saba kwa ajili ya kusanyiko, nao maafisa wakatoa mafahali elfu moja, pamoja na kondoo na mbuzi elfu kumi. Idadi kubwa ya makuhani wakajiweka wakfu. Kusanyiko la Yuda, pamoja na makuhani na Walawi, na wote waliokusanyika kutoka Israeli, pamoja na wageni waliotoka Israeli na wale walioishi Yuda, wote wakafurahi. Kulikuwa na furaha kubwa katika Yerusalemu, kwa sababu tangu siku za Mfalme Sulemani mwana wa Daudi mfalme wa Israeli halijakuwepo jambo kama hili huko Yerusalemu. Ndipo makuhani na Walawi wakasimama wakawabariki watu, naye Mungu akawasikia, kwa sababu maombi yao yalifika mbinguni, makao yake matakatifu.

Wito wa kumrudia Mwenyezi Mungu

Katika mwezi wa nane wa mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Mwenyezi Mungu lilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia, mwana wa Ido, kusema:

"Mwenyezi Mungu aliwakasirikia sana baba zako wa zamani. Kwa hiyo waambie watu: Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: Nirudieni mimi,asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, nami nitawarudia ninyi,asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. Msiwe kama baba zenu, ambao manabii waliotangulia waliwatangazia: Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: Geukeni, mziache njia zenu mbaya na matendo yenu maovu.Lakini hawakunisikiliza wala kufuata maelekezo yangu, asema Mwenyezi Mungu. Wako wapi baba zako sasa? Nao manabii, je, wanaishi milele? Je, maneno yangu na amri zangu nilizowaagiza manabii watumishi wangu, hayakuwapata baba zenu?

"Kisha walitubu na kusema, Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ametutenda sawasawa na njia zetu na matendo yetu yalivyostahili, kama alivyokusudia kufanya.’ "

Maono ya kwanza: Mtu katikati ya miti ya mihadasi

Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, yaani mwezi uitwao Shebati, katika mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Mwenyezi Mungu lilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia mwana wa Ido.

Wakati wa usiku nilipata maono, na tazama, mbele yangu palikuwa na mtu akiendesha farasi mwekundu! Alikuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi kwenye bonde. Nyuma yake walikuwepo farasi wekundu, wa kikahawia, na weupe.

Nikauliza, "Hivi ni vitu gani bwana wangu?"

Malaika aliyekuwa akizungumza na mimi akanijibu, "Nitakuonesha kuwa ni nini."

Kisha yule mtu aliyesimama katikati ya miti ya mihadasi akaeleza, "Ni wale ambao Mwenyezi Mungu amewatuma waende duniani kote."

Nao wakatoa taarifa kwa yule malaika wa Mwenyezi Mungu, aliyekuwa amesimama katikati ya miti ya mihadasi, "Tumepita duniani kote na kukuta ulimwengu wote umepumzika kwa amani."

Kisha malaika wa Mwenyezi Mungu akasema, "Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, utazuia hadi lini rehema kutoka Yerusalemu na miji ya Yuda, ambayo umeikasirikia kwa miaka hii sabini?" Kwa hiyo Mwenyezi Mungu akazungumza maneno ya upole na ya kufariji kwa malaika aliyezungumza nami.

Kisha malaika yule aliyekuwa akizungumza nami akasema, "Tangaza neno hili: Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: Nina wivu sana kwa ajili ya Yerusalemu na Sayuni, lakini nimeyakasirikia sana mataifa yanayojisikia kuwa yako salama. Nilikuwa nimewakasirikia Israeli kidogo tu, lakini mataifa hayo yaliwazidishia maafa.

"Kwa hiyo, hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu: Nitairudia Yerusalemu kwa rehema na huko nyumba yangu itajengwa tena. Nayo kamba ya kupimia itanyooshwa juu ya Yerusalemu,asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.

"Endelea kutangaza zaidi kwamba: Hivi ndivyo asemavyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: Miji yangu itafurika tena ustawi na Mwenyezi Mungu atamfariji tena Sayuni na kumchagua Yerusalemu.’ "

Maono ya pili: Pembe nne na mafundi wanne

Kisha nikatazama juu, na pale mbele yangu nikaona pembe nne! Nikamuuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, "Ni nini hizi?"

Akanijibu, "Hizi ni zile pembe zilizowatawanya Yuda, Israeli na Yerusalemu."

Kisha Mwenyezi Mungu akanionesha mafundi wanne. Nikauliza, "Hawa wanakuja kufanya nini?"

Akanijibu, "Hizi ndizo pembe zilizowatawanya Yuda ili asiwepo atakayeweza kuinua kichwa chake, lakini mafundi wamekuja kuzitia hofu na kuzitupa chini hizi pembe za mataifa ambayo yaliinua pembe zao dhidi ya nchi ya Yuda na kuwatawanya watu wake."

Wale ninaowapenda, ninawakemea na kuwaadibisha. Hivyo uwe na bidii ukatubu.

Basi, ueni kabisa chochote kilicho ndani yenu cha asili ya kidunia: yaani uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya na ulafi, ambao ni ibada ya sanamu.

Wala msivitoe viungo vya miili yenu vitumike kama vyombo vya uovu vya kutenda dhambi, bali jitoeni kwa Mungu, kama watu waliotolewa kutoka mautini kuingia uzimani. Nanyi vitoeni viungo vya miili yenu kwake kama vyombo vya haki.

Chukulianeni mizigo

Ndugu zangu, ikiwa mtu amepatikana akitenda dhambi, basi ninyi mnaoishi kwa Roho wa Mungu mnapaswa kumrejesha mtu huyo kwa upole. Lakini jihadharini, ili ninyi wenyewe msije mkajaribiwa.

Kwa hiyo, ondoleeni mbali uchafu wote na uovu ambao umezidi kuwa mwingi, mkalipokee kwa unyenyekevu lile Neno lililopandwa ndani yenu ambalo laweza kuokoa nafsi zenu.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-