Coração puro
Bem-aventurados os puros de coração, porque verão a Deus. A pureza de coração é alvo, privilégio e busca constante do cristão que deseja contemplar a face do Senhor.
Coração puro
Bem-aventurados os puros de coração. A pureza interior precede toda transformação externa e abre os olhos para ver a Deus.
Heri walio na moyo safi,
maana hao watamwona Mungu.
Nani awezaye kuupanda mlima wa Mwenyezi Mungu?
Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake?
Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe,
yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake
au kuapa kwa kitu cha uongo.
Huyo atapokea baraka kutoka kwa Mwenyezi Mungu,
na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake.
Ufiche uso wako usizitazame dhambi zangu,
na uufute uovu wangu wote.
Ee Mungu, uniumbie moyo safi,
uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.
Usinitupe kutoka mbele zako
wala kuniondolea Roho wako Mtakatifu.
Haki ya Mwenyezi Mungu
Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli,
kwa wale ambao mioyo yao ni safi.
Purificar-se
Todo o que tem essa esperança em Cristo se purifica. O amor procede de coração puro, boa consciência e fé sincera.
Kila mmoja mwenye matumaini haya ndani yake hujitakasa, kama vile yeye alivyo mtakatifu.
Wapendwa, sasa tu wana wa Mungu, lakini bado haijadhihirika tutakavyokuwa, lakini twajua kwamba yeye atakapodhihirishwa, tutafanana naye, kwa maana tutamwona kama alivyo. Kila mmoja mwenye matumaini haya ndani yake hujitakasa, kama vile yeye alivyo mtakatifu.
Kusudi la maagizo haya ni upendo unaotoka katika moyo safi, dhamiri safi na imani ya kweli.
Zikimbie tamaa mbaya za ujana, ufuate haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana Isa kwa moyo safi.
Haya ndio maombi yangu: kwamba upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote, ili mpate kutambua yale yaliyo mema, mkawe safi, wasio na hatia hadi siku ya Al-Masihi, mkiwa mmejawa na matunda ya haki yapatikanayo kupitia kwa Isa Al-Masihi, kwa utukufu na sifa za Mungu.
Fanyeni mambo yote bila kunung’unika wala kushindana, ili msiwe na lawama wala hatia, bali mwe wana wa Mungu wasio na kasoro katika kizazi chenye ukaidi na kilichopotoka, ambacho ndani yake ninyi mnang’aa kama mianga ulimwenguni. Mkilishika neno la uzima, ili nipate kuona fahari siku ya Al-Masihi kwamba sikupiga mbio wala kujitaabisha bure.
Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli hata mkawa na upendo wa ndugu usio na unafiki, basi pendaneni kwa dhati kutoka moyoni.
Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe,
bali makusudi hupimwa na Mwenyezi Mungu.