Publicidade

Coração puro

Por Bíblia Online

Bem-aventurados os puros de coração, porque verão a Deus. A pureza de coração é alvo, privilégio e busca constante do cristão que deseja contemplar a face do Senhor.

Coração puro

Bem-aventurados os puros de coração. A pureza interior precede toda transformação externa e abre os olhos para ver a Deus.

Heri wenye moyo safi;

Maana hao watamwona Mungu.

Ni nani atakayepanda katika mlima wa BWANA?

Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?

Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe,

Asiyeiweka nafsi yake katika uongo,

Wala hakuapa kwa hila.

Atapokea baraka kwa BWANA,

Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.

Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu;

Uzifute hatia zangu zote.

Ee Mungu, uniumbie moyo safi,

Uifanye upya na kuithibiti roho yangu.

Usinitenge na uso wako,

Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.

Ombi la kuponywa kutoka kwa waonevu

Hakika Mungu ni mwema kwa Israeli,

Kwa hao walio safi mioyo yao.

Purificar-se

Todo o que tem essa esperança em Cristo se purifica. O amor procede de coração puro, boa consciência e fé sincera.

Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.

Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini tunajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.

Lakini lengo la agizo hili ni kuleta upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki.

Lakini zikimbie tamaa za ujanani; ukafuate haki, na imani, na upendo, na amani, pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.

Na hii ndiyo dua yangu, kwamba pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote; mpate kuyakubali yaliyo mema; ili mpate kuwa na mioyo safi, bila kosa, mpaka siku ya Kristo; akiwa mmejazwa matunda ya haki, kwa njia ya Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.

Yatendeni mambo yote pasipo manung’uniko wala mashindano, mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu, mkishika neno la uzima; nipate sababu ya kuona fahari katika siku ya Kristo, ya kuwa sikupiga mbio bure wala sikujitaabisha bure.

Mkiisha kujitakasa roho zenu kwa kuitii kweli, hata kuufikia upendano wa ndugu usio na unafiki, basi jitahidini kupendana kwa moyo safi.

Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe;

Bali BWANA huzipima roho za watu.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-