Publicidade

Coração quebrantado

Por Bíblia Online

Deus está perto dos que têm o coração quebrantado. A Bíblia consola os aflitos: o sacrifício que Deus aceita é o espírito quebrantado e um coração contrito — jamais desprezará.

Mwenyezi Mungu yu karibu na waliovunjika moyo,

na huwaokoa waliopondeka roho.

Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika;

moyo uliovunjika wenye toba,

ee Mungu, hutaudharau.

Anawaponya waliovunjika mioyo

na kuvifunga vidonda vyao.

Mwili na moyo wangu vyaweza kushindwa,

bali Mungu ni nguvu ya moyo wangu

na fungu langu milele.

Kwa maana hili ndilo asemalo Aliye juu,

yeye aliyeinuliwa sana,

yeye aishiye milele,

ambaye jina lake ni Mtakatifu:

"Ninaishi mahali palipoinuka

na patakatifu,

lakini pia pamoja na yeye aliye na roho iliyotubu,

na mwenye roho ya unyenyekevu,

ili kuzihuisha roho za wanyenyekevu

na kuihuisha mioyo yao waliotubu.

Je, mkono wangu haukuumba vitu hivi vyote,

hivyo vikapata kuwepo?"

asema Mwenyezi Mungu.

"Mtu huyu ndiye ninayemthamini:

yeye ambaye ni mnyenyekevu

na mwenye roho yenye toba,

atetemekaye asikiapo neno langu.

Mwaka wa upendeleo wa Mwenyezi Mungu

Roho wa Bwana Mungu Mwenyezi yu juu yangu,

kwa sababu Mwenyezi Mungu amenipaka mafuta

kuwahubiria maskini habari njema.

Amenituma kuwafariji waliovunjika moyo,

kuwatangazia mateka uhuru wao,

na hao waliofungwa

habari za kufunguliwa kwao;

kutangaza mwaka wa Mwenyezi Mungu uliokubaliwa,

na siku ya kisasi ya Mungu wetu,

kuwafariji wote wanaoomboleza,

na kuwapa mahitaji

wale wanaohuzunika katika Sayuni,

ili kuwapa taji za uzuri badala ya majivu,

mafuta ya furaha badala ya maombolezo,

vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa.

Nao wataitwa mialoni ya haki,

pando la Mwenyezi Mungu,

ili kuonesha utukufu wake.

"Heri walio maskini wa roho,

maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Heri wale wanaohuzunika,

maana hao watafarijiwa.

Heri walio wapole,

maana hao watairithi nchi.

Kwa maana huzuni ya kiungu huleta toba iletayo wokovu, wala haina majuto. Lakini huzuni ya kidunia husababisha mauti. Tazameni jinsi huzuni hii ya kiungu ilivyoleta faida ndani yenu: bidii mliyo nayo, juhudi mliyofanya kujitetea, uchungu wenu, hofu yenu, upendo wenu, shauku yenu na jinsi mlivyokuwa tayari kutoa adhabu inayostahili. Kwa kila njia mmejithibitisha kuwa safi katika jambo hilo.

Lakini aliniambia, "Neema yangu inakutosha, kwa kuwa uweza wangu hukamilika katika udhaifu." Kwa hiyo nitajisifu kwa furaha zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili uweza wa Al-Masihi ukae juu yangu.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-