Coragem
A coragem cristã não é ausência de medo — é confiança em Deus maior que todo temor. Sê forte e corajoso! é o chamado repetido do Senhor aos seus filhos.
Sê forte e corajoso
O Senhor é a minha luz e a minha salvação — de quem terei medo? Com coragem enfrentamos o mundo, porque Deus está conosco.
Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakuwa pamoja nawe popote utakapoenda."
Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakuwa pamoja nawe popote utakapoenda."
Kuweni imara na moyo wa ushujaa. Msiogope wala msifadhaike kwa sababu yao, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anaenda pamoja nanyi; kamwe hatawaacha wala hatawatupa ninyi."
Kuweni imara na moyo wa ushujaa. Msiogope wala msifadhaike kwa sababu yao, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anaenda pamoja nanyi; kamwe hatawaacha wala hatawatupa ninyi."
Mwenyezi Mungu mwenyewe atakutangulia naye atakuwa pamoja nawe; kamwe hatakuacha wala hatakutupa. Usiogope, wala usifadhaike."
Daudi pia akamwambia Sulemani mwanawe, "Uwe hodari na moyo mkuu, ukafanye kazi hii. Usiogope wala usifadhaike, kwa maana Bwana Mwenyezi Mungu, aliye Mungu wangu, yu pamoja nawe. Hatakuacha wala hatakupungukia, hadi kazi hii yote kwa ajili ya utumishi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu itakapokamilika.
Coragem em Cristo
Não vos deu Deus espírito de covardia. Sede fortes na fé! O perfeito amor lança fora todo medo.
Maana Mungu hakutupatia roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Maana Mungu hakutupatia roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.
Kesheni; simameni imara katika imani; kuweni mashujaa na hodari.
Kesheni; simameni imara katika imani; kuweni mashujaa na hodari.
Katika pendo hakuna hofu. Lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa sababu hofu inahusika na adhabu. Kila mwenye hofu hakukamilika katika pendo.
wala msitishwe na wale wanaowapinga. Hii ni ishara kwao kuwa wataangamia, lakini ninyi mtaokolewa, na hii ni kazi ya Mungu.
Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Kwa maana hamkupokea roho ya utumwa iletayo hofu tena, bali mlipokea Roho wa kufanywa wana, ambaye kwa yeye twalia, "Abba, Baba."
Não temas
Não temas, porque Eu sou contigo. Quando tiver medo, em ti confiarei. Deus é nosso escudo e fortaleza.
Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;
usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.
Nitakutia nguvu na kukusaidia;
nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.
Kwa maana Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wako,
nikushikaye mkono wako wa kuume
na kukuambia, Usiwe na hofu,
nitakusaidia.
Usiogope, kwa kuwa mimi nipo pamoja nawe,
nitawaleta watoto wako kutoka mashariki,
na kukukusanya kutoka magharibi.
"Usiogope, wewe hutaaibika.
Usiogope aibu, wewe hutaaibishwa.
Wewe utasahau aibu ya ujana wako,
wala hutakumbuka tena mashutumu ya ujane wako.
Wakati ninaogopa,
nitakutumaini wewe.
Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu,
katika Mungu ninatumaini, sitaogopa.
Mwanadamu mwenye kufa
atanitenda nini?
Mwenyezi Mungu ni nuru yangu na wokovu wangu,
nimwogope nani?
Mwenyezi Mungu ni ngome ya uzima wangu,
nimhofu nani?
Mngojee Mwenyezi Mungu;
uwe hodari na mwenye moyo mkuu,
na umngojee Mwenyezi Mungu.
Mngojee Mwenyezi Mungu;
uwe hodari na mwenye moyo mkuu,
na umngojee Mwenyezi Mungu.
Kuweni hodari na mjipe moyo,
ninyi nyote mnaomtumaini Mwenyezi Mungu.
Hata nikipita katikati
ya bonde la uvuli wa mauti,
sitaogopa mabaya,
kwa maana wewe upo pamoja nami;
fimbo yako na mkongojo wako
vyanifariji.
Conforto e encorajamento
O Deus de toda consolação nos consola em todas as tribulações. Coragem não falta a quem descansa em Deus.
Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Isa Al-Masihi, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote. Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu.
Lakini tunayo hazina hii katika vyombo vya udongo, ili ijulikane wazi kwamba uwezo huu wa ajabu unatoka kwa Mungu, wala si kwetu. Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa; twateswa lakini hatuachwi; twatupwa chini lakini hatupondwi. Siku zote twachukua katika mwili kufa kwake Isa ili uzima wa Isa uweze kudhihirishwa katika miili yetu. Kwa maana sisi tulio hai siku zote tumetolewa tufe kwa ajili ya Isa, ili uzima wake upate kudhihirishwa katika mwili wetu upatikanao na mauti.
Yalindeni maisha yenu msiwe na tabia ya kupenda fedha, bali mridhike na vile mlivyo navyo, kwa sababu Mungu amesema,
"Kamwe sitakuacha,
wala sitakupungukia."
Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri,
"Mwenyezi Mungu ni msaada wangu; sitaogopa.
Mwanadamu anaweza kunitenda nini?"
Basi, ni nani atakayewadhuru mkiwa wenye juhudi katika kutenda mema? Lakini hata ikiwalazimu kuteseka kwa ajili ya haki, mmebarikiwa. "Msiogope vitisho vyao, wala msiwe na wasiwasi."
Amani nawaachia; amani yangu nawapa. Amani hii ninayowapa si kama ile ulimwengu unatoa. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.
lakini walipomwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu. Wakapiga yowe, kwa sababu wote walipomwona waliogopa.
Mara Isa akasema nao, akawaambia, "Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!"