Criação
A criação revela a glória de Deus. Céus, terra, mares e tudo o que existe testemunham o poder criador. No princípio Deus criou — e tudo era muito bom.
No princípio
No princípio criou Deus os céus e a terra. O Espírito de Deus pairava sobre as águas. E Deus disse: haja luz.
Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia. Wakati huu dunia ilikuwa haina umbo, tena ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya vilindi vya maji, naye Roho wa Mungu alikuwa ametulia juu ya maji.
Ndipo Mungu akasema, "Tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini na ndege wa angani, na mifugo na wanyama pori wote, na dunia yote, na viumbe vyote vinavyotambaa ardhini."
Kwa hiyo Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake mwenyewe,
kwa mfano wa Mungu alimuumba;
mwanaume na mwanamke aliwaumba.
Mungu akaibariki siku ya saba, akaifanya takatifu, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika baada ya kazi zote za kuumba alizokuwa amefanya.
Bwana Mwenyezi Mungu akasema, "Si vyema huyu mtu awe peke yake. Nitamfanyia msaidizi wa kumfaa."
O poder criador
Pela palavra do Senhor foram feitos os céus. Tudo foi criado por Ele e para Ele — o visível e o invisível.
Kwa neno la Mwenyezi Mungu mbingu ziliumbwa,
jeshi lao la angani likaumbwa
kwa pumzi ya kinywa chake.
Kabla ya kuzaliwa milima
au hujaumba dunia na ulimwengu,
wewe ni Mungu tangu milele hata milele.
Njooni, tusujudu, tumwabudu,
tupige magoti mbele za Mwenyezi Mungu Muumba wetu,
Nayainua macho yangu natazama milima:
msaada wangu utatoka wapi?
Msaada wangu hutoka kwa Mwenyezi Mungu,
Muumba wa mbingu na dunia.
Msaada wetu ni katika jina la Mwenyezi Mungu,
Muumba wa mbingu na dunia.
Hii ndiyo siku Mwenyezi Mungu aliyoifanya,
tushangilie na kufurahi ndani yake.
Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;
uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.
Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa
kwa namna ya ajabu na ya kutisha;
kazi zako ni za ajabu,
ninajua hayo kikamilifu.
Criador e Sustentador
O Deus eterno não se cansa nem se fatiga. Dele, por Ele e para Ele são todas as coisas — a Ele seja a glória.
Je wewe, hufahamu?
Je wewe, hujasikia?
Mwenyezi Mungu ni Mungu wa milele,
Muumba wa miisho ya dunia.
Hatachoka wala kulegea,
wala hakuna hata mmoja
awezaye kuupima ufahamu wake.
"Ole wake yeye ashindanaye na Muumba wake,
yeye ambaye ni kigae tu kati ya vigae juu ya ardhi.
Je, udongo wa kufinyangia humwambia mfinyanzi,
‘Unatengeneza nini wewe?’
Je, kazi yako husema,
‘Hana mikono’?
"Ee Bwana Mungu Mwenyezi, umeumba mbingu na nchi kwa uwezo wako mkuu na kwa mkono ulionyooshwa. Hakuna jambo lililo gumu usiloliweza.
yeye ambaye hujenga jumba lake la kifalme katika mbingu
na kuisimika misingi yake juu ya dunia,
yeye aitaye maji ya bahari
na kuyamwaga juu ya nchi:
Mwenyezi Mungu ndilo jina lake.
Kwa maana vitu vyote vyatoka kwake,
viko kwake na kwa ajili yake.
Utukufu ni wake milele! Amen.
Kwa maana tangu kuumbwa kwa ulimwengu, asili ya Mungu asiyeonekana kwa macho, yaani uweza wake wa milele na asili yake ya uungu, imeonekana waziwazi, ikitambuliwa kutokana na yale aliyoyafanya ili wanadamu wasiwe na udhuru.
Kwa maana viumbe vyote vinangoja kwa shauku kudhihirishwa kwa watoto wa Mungu.
Nova criação
Se alguém está em Cristo, nova criatura é. O Criador faz novas todas as coisas — na natureza e na redenção.
Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Al-Masihi, amekuwa kiumbe kipya: ya kale yamepita; tazama, yamekuwa mapya.
Kwa maana sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tulioumbwa katika Al-Masihi Isa, ili tupate kutenda matendo mema, ambayo Mungu alitangulia kuyaandaa tupate kuishi katika hayo.
Kwa mapenzi yake mwenyewe alituzaa kwa neno la kweli, kusudi tuwe kama mazao ya kwanza katika viumbe vyake vyote.
Kwa kuwa kila nyumba hujengwa na mtu, lakini Mungu ni mjenzi wa kila kitu.
‘Kwa kuwa ndani yake tunaishi, tunatembea na kuwa na uzima wetu.’ Kama baadhi ya watunga mashairi wenu walivyosema, ‘Sisi ni uzao wake.’
Kisha nikasikia kila kiumbe mbinguni na duniani, chini ya nchi, na baharini, na vyote vilivyomo, vikiimba:
"Sifa na heshima na utukufu na uweza
ni vyake yeye aliyeketi juu ya hicho kiti cha enzi,
na kwa Mwana-Kondoo,
milele na milele!"