Publicidade

Tomar uma decisão

Por Bíblia Online

Tomar decisões com sabedoria é um dos maiores desafios da vida. A Bíblia nos ensina a buscar a Deus em oração, na Palavra e no conselho, confiando que Ele dirige os nossos passos.

Buscar a Deus

Se algum de vós tem falta de sabedoria, peça a Deus. Ele dá generosamente e sem repreensão a todos os que pedem.

Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.

Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote.

Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote,

Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;

Katika njia zako zote mkiri yeye,

Naye atayanyosha mapito yako.

Katika njia zako zote mkiri yeye,

Naye atayanyosha mapito yako.

Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.

Conselho e direção

Onde não há conselho os planos se frustam. Toda Escritura é útil para nos guiar nas decisões da vida.

Pasipo mashauri taifa huanguka;

Bali kwa wingi wa washauri huja wokovu.

Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo;

Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.

Ajitengaye na wenzake hutafuta matakwa yake mwenyewe;

Hushindana na kila shauri jema.

Mpumbavu hapendezwi na ufahamu;

Ila moyo wake udhihirike tu.

Ajapo asiye haki, huja dharau pia;

Na pamoja na aibu huja lawama.

Maneno ya kinywa cha mtu ni kama maji ya vilindi;

Kijito kibubujikacho; chemchemi ya hekima.

Kukubali uso wake asiye haki si vizuri;

Wala kumpotosha mwenye haki hukumuni.

Midomo ya mpumbavu huingia katika fitina,

Na kinywa chake huita mapigo.

Kinywa cha mpumbavu ni uharibifu wake,

Na midomo yake ni mtego wa nafsi yake.

Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo;

Nayo hushukia pande za ndani za tumbo.

Yeye naye aliye mvivu katika kazi yake,

Ni ndugu yake aliye mharibifu.

Jina la BWANA ni ngome imara;

Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.

Mali ya mtu tajiri ni mji wake wa nguvu;

Ni kama ukuta mrefu katika mawazo yake.

Kabla ya uharibifu moyo wa mwanadamu hujivuna;

Na kabla ya heshima hutangulia unyenyekevu.

Yeye ajibuye kabla hajasikia,

Ni upumbavu na aibu kwake.

Roho ya mtu itastahimili udhaifu wake;

Bali roho iliyovunjika nani awezaye kuistahimili?

Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;

ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.

Walipofika kukabili Misia wakajaribu kuenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa,

Barnaba na Sauli wateuliwa

Na huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, nao ni Barnaba, na Simeoni aitwaye Nigeri, na Lukio Mkirene, na Manaeni aliyekuwa ndugu wa kulelewa wa mfalme Herode, na Sauli. Basi hawa walipokuwa wakimfanyia Bwana ibada na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Nitengeeni Barnaba na Sauli kwa kazi ile niliyowaitia. Ndipo wakiisha kufunga na kuomba, wakaweka mikono yao juu yao, wakawaacha waende zao.

Confiar e seguir

Seja o que for que façais, fazei tudo para a glória de Deus. O sábio ouve a Deus antes de agir.

Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.

Mfano wa Yesu

Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa subira katika yale mashindano yaliyowekwa mbele yetu,

Na huko Gibeoni BWANA akamtokea Sulemani katika ndoto ya usiku; Mungu akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo. Na sasa, Ee BWANA, Mungu wangu, umenitawaza niwe mfalme mimi mtumwa wako badala ya Daudi baba yangu; nami ni mtoto mdogo tu; sijui jinsi inipasavyo kutoka wala kuingia. Na mtumwa wako yuko katikati ya watu wako uliowachagua, watu wengi wasioweza kuhesabiwa, wala kufahamiwa idadi yao, kwa kuwa ni wengi. Kwa hiyo nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya; maana ni nani awezaye kuwahukumu watu hawa wako walio wengi?

Neno hili likawa jema machoni pa Bwana, ya kuwa Sulemani ameomba neno hili. Mungu akamwambia, Kwa kuwa umeomba neno hili, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi; wala hukutaka utajiri kwa nafsi yako; wala hukutaka roho za adui zako; bali umejitakia akili za kujua kuhukumu; basi, tazama, nimefanya kama ulivyosema. Tazama, nimekupa moyo wa hekima na wa akili; hata kabla yako hapakuwa na mtu kama wewe, wala baada yako hatainuka mtu kama wewe.

Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Mkufuru Mungu, ufe. Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-