Publicidade

O Deus do impossível

Por Bíblia Online

Deus é o Deus do impossível. Para Ele não há nada difícil demais. O que parece impossível aos olhos humanos é perfeitamente possível para o Criador do universo.

Nada é impossível

Para Deus nada é impossível. Ele faz infinitamente mais do que podemos pedir ou imaginar — esse é o nosso Deus.

Lakini Isa akawatazama, akawaambia, "Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini mambo yote yanawezekana kwa Mungu."

Isa akawatazama, akawaambia, "Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu sivyo. Mambo yote yanawezekana kwa Mungu."

Isa akajibu, "Yasiyowezekana kwa wanadamu yanawezekana kwa Mungu."

Mariamu akamuuliza huyo malaika, "Maadamu mimi ni bikira, jambo hili litawezekanaje?"

Malaika akamjibu, "Roho wa Mungu atakujilia juu yako, nazo nguvu zake Yeye Aliye Juu Sana zitakufunika kama kivuli. Kwa hiyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mtakatifu, naye ataitwa Mwana wa Mungu), wa kiroho, bali si wa kimwili.. Tazama, jamaa yako Elizabeti amechukua mimba katika uzee wake, na huu ni mwezi wake wa sita, yeye aliyeitwa tasa. Kwa maana kwa Mungu hakuna lisilowezekana."

Mariamu akasema, "Tazama, mimi ni mtumishi wa Mwenyezi Mungu. Na iwe kwangu kama ulivyosema." Kisha malaika akaondoka, akamwacha.

Ndipo Mwenyezi Mungu akamwambia Ibrahimu, "Kwa nini Sara amecheka na kusema, Kweli nitazaa mtoto nami sasa ni mzee?Je, kuna jambo lolote gumu lisilowezekana kwa Mwenyezi Mungu? Nitakurudia majira kama haya mwaka ujao, naye Sara atakuwa na mwana."

"Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote,

wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika.

"Ee Bwana Mungu Mwenyezi, umeumba mbingu na nchi kwa uwezo wako mkuu na kwa mkono ulionyooshwa. Hakuna jambo lililo gumu usiloliweza.

Fé no impossível

Se tiverdes fé como um grão de mostarda... Os impossíveis de Deus são convites ao exercício da fé audaciosa.

Akawajibu, "Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Ninawaambia kweli, mkiwa na imani ndogo kama punje ya haradali, mtauambia mlima huu, Ondoka hapa uende pale,nao utaondoka. Wala hakutakuwa na jambo lisilowezekana kwenu. [

Isa akamwambia, "Ati, Kama unaweza kufanya jambo lolote? Yote yawezekana kwake yeye aaminiye."

Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote mtakayoyaomba mkisali, aminini kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu.

Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: "Mambo haya yanaweza kuonekana ya ajabu kwa mabaki ya watu wakati huo, lakini yaweza kuwa ya ajabu kwangu?" asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.

Bwana wetu ni mkuu na mwenye uwezo mwingi,

ufahamu wake hauna kikomo.

Baada ya huyu mtu kutolewa kwenu kwa mpango wa Mungu uliokusudiwa kwa kujua kwake Mungu tangu zamani, ninyi mlimuua kwa kumsulubisha msalabani, kwa mikono ya watu waovu. Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu akamwondolea uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana yeye kushikiliwa na nguvu za mauti.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-