Deus é nosso refúgio
Deus é nosso refúgio e fortaleza, socorro bem presente nas angústias. Quando o mundo treme, o crente encontra paz sob as asas do Altíssimo.
Refúgio e fortaleza
Deus é nosso refúgio e fortaleza. Quem habita no abrigo do Altíssimo descansa à sombra do Todo-Poderoso.
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,
Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
Aketiye mahali pa siri pake Aliye Juu
Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.
Atasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu nitakayemtumaini.
Maana Yeye atakuokoa kutoka kwa mtego wa mwindaji,
Na katika maradhi mabaya.
Kwa manyoya yake atakufunika,
Chini ya mbawa zake utapata kimbilio;
Uaminifu wake ni ngao na kigao.
Wewe, BWANA, nguvu yangu, nakupenda sana;
BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu,
Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia,
Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
Namwita BWANA astahiliye kusifiwa,
Hivyo nitaokoka na adui zangu.
Mungu, unihifadhi mimi,
Kwa maana nakukimbilia Wewe.
BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu,
Nimwogope nani?
BWANA ni ngome ya uzima wangu,
Nimhofu nani?
Watenda mabaya waliponikaribia,
Wanile nyama yangu,
Watesi wangu na adui zangu,
Walijikwaa wakaanguka.
Jeshi lijapojipanga kupigana nami,
Moyo wangu hautaogopa.
Vita vijaponitokea,
Hata hapo nitatumainia BWANA.
Nimekukimbilia Wewe, BWANA,
Nisiaibike milele.
Kwa haki yako uniponye,
Unitegee sikio lako, uniokoe hima.
Uwe kwangu mwamba wa nguvu,
Ngome thabiti ya kuniokoa.
Ndiwe mwamba wangu na ngome yangu;
Kwa ajili ya jina lako uniongoze na unichunge.
Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri,
Maana Wewe ndiwe ngome yangu.
Mikononi mwako naiweka roho yangu;
Umenikomboa, Ee BWANA, Mungu wa kweli.
Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu,
Ngome imara ya wokovu wangu.
Maana wewe,
Ndiwe mwamba wangu na ngome yangu.
Proteção e segurança
O Senhor é a minha rocha e a minha fortaleza. Melhor é confiar no Senhor do que confiar no homem.
Ni heri kumkimbilia BWANA
Kuliko kuwatumainia wanadamu.
Ni heri kumkimbilia BWANA.
Kuliko kuwatumainia wakuu.
Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa utulivu.
Maana tumaini langu hutoka kwake.
Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu,
Ngome yangu, sitatikisika.
Kwa Mungu wokovu wangu,
Na utukufu wangu;
Mwamba wa nguvu zangu,
Na kimbilio langu ni kwa Mungu.
Enyi watu, mtumainini sikuzote,
Ifunueni mioyo yenu mbele zake;
Mungu ndiye kimbilio letu.
Ee nguvu zangu, nitakuimbia sifa,
Maana Ewe Mungu ndiwe ngome yangu,
Mungu wa fadhili zangu.
Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu,
Kizazi baada ya kizazi.
Kabla haijazaliwa milima, wala hujaiumba dunia,
Na tangu milele hata milele ndiwe Mungu.
BWANA atakuwa ngome kwake aliyeonewa,
Naam, ngome kwa nyakati za shida.
Nao wakujuao jina lako wakutumaini Wewe,
Maana Wewe, BWANA hukuwaacha wakutafutao.
Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako!
Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.
Em todo tempo
O Senhor é bom e é fortaleza no dia da angústia. A torre forte do nome do Senhor protege os seus em toda circunstância.
BWANA ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao.
Maana umekuwa ngome ya maskini,
Ngome ya mhitaji katika dhiki yake,
Mahali pa kukimbilia wakati wa tufani,
Na kivuli wakati wa joto;
Wakati kishindo cha watu wakatili kilipokuwa,
Kama dhoruba ipigayo ukuta.
Kumcha BWANA ni tumaini imara;
Watoto wake watakuwa na kimbilio.
Njia ya BWANA ni kimbilio lake mtu mkamilifu;
Bali ni uharibifu kwao watendao maovu.