Deus nunca falha
Deus nunca falha. Nenhuma de suas promessas vem ao chão. O que Ele prometeu, Ele cumprirá. A fidelidade de Deus é o fundamento inabalável da nossa fé.
Promessas cumpridas
Nenhuma boa palavra falhou de todas as promessas que Deus fez. Ele é fiel e verdadeiro em tudo o que diz.
"Sasa mimi ninakaribia kwenda katika njia ya watu wote wa dunia. Mnajua kwa mioyo yenu na roho zenu kwamba hakuna ahadi zozote njema Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alizowaahidia, ambazo hazikutimia. Kila ahadi imetimizwa, hakuna hata moja ambayo haikutimia.
Hakuna hata mojawapo ya ahadi nzuri ya Mwenyezi Mungu kwa nyumba ya Israeli ambayo haikutimia; kila moja ilitimia.
"Ahimidiwe Mwenyezi Mungu, aliyewapa pumziko watu wake Israeli kama alivyokuwa ameahidi. Hakuna hata neno moja lililopunguka kati ya ahadi zote nzuri alizozitoa kupitia mtumishi wake Musa.
Mungu si mtu, hata aseme uongo,
wala yeye si mwanadamu, hata ajute.
Je, anasema, kisha asitende?
Je, anaahidi, asitimize?
Lakini mipango ya Mwenyezi Mungu inasimama imara milele,
makusudi ya moyo wake kwa vizazi vyote.
Fidelidade eterna
A Palavra do Senhor permanece para sempre. A tua palavra é muito pura e o teu servo a ama profundamente.
Inueni macho yenu mbinguni,
mkaitazame dunia chini;
mbingu zitatoweka kama moshi,
dunia itachakaa kama vazi,
na wakazi wake kufa kama inzi.
Bali wokovu wangu utadumu milele,
haki yangu haitakoma kamwe.
Ahadi zako zimejaribiwa kikamilifu,
mtumishi wako anazipenda.
Ufalme wako ni ufalme wa milele,
mamlaka yako hudumu vizazi vyote.
Mwenyezi Mungu ni mwaminifu kwa ahadi zake zote
na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
Mwenyezi Mungu huwategemeza wote waangukao,
na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao.
Mwenyezi Mungu aliye ndani yake ni mwenye haki,
hafanyi kosa.
Asubuhi kwa asubuhi hutoa haki yake,
kila kukipambazuka huitimiza,
bali mtu dhalimu hana aibu.
Kwa kuwa ufunuo huu unasubiri wakati uliokubalika;
unazungumzia mambo ya mwisho,
na kamwe hautakosea.
Iwapo utakawia, wewe usubiri;
kwa hakika utakuja na hautachelewa.
Segurança em Deus
Todas as promessas de Deus são sim e amém em Cristo. Fiel é Aquele que prometeu — Ele jamais nos decepcionará.
Kwa maana ahadi zote za Mungu zilizo katika Al-Masihi ni "Ndiyo". Kwa sababu hii, ni kwake yeye tunasema "Amen" kwa utukufu wa Mungu. Basi ni Mungu atufanyaye sisi pamoja nanyi kusimama imara katika Al-Masihi. Alitupaka mafuta kwa kututia muhuri wake na kutupatia Roho wake Mtakatifu mioyoni mwetu kuwa rehani kwa ajili ya kututhibitishia yote aliyotuahidi.
Tushike kwa uthabiti lile tumaini la ukiri wetu bila kuyumbayumba, kwa maana yeye aliyeahidi ni mwaminifu.
Ninyi pia mliingia ndani ya Al-Masihi mliposikia neno la kweli, Injili ya wokovu wenu. Baada ya kuamini, mlitiwa muhuri ndani yake, huyo Roho Mtakatifu wa Mungu mliyeahidiwa, yeye ambaye ni amana yetu ya kutuhakikishia urithi wetu hadi ukombozi wa wale walio milki ya Mungu, kwa sifa ya utukufu wake.
Kujaribiwa
Heri mtu anayevumilia wakati wa majaribu, kwa sababu akiisha kushinda hilo jaribio atapewa taji lile la uzima Mungu alilowaahidia wale wanaompenda.