Dia das crianças
As crianças são preciosas aos olhos de Deus. Jesus as acolheu, abençoou e ensinou que delas é o Reino dos Céus — modelos de fé, pureza e humildade.
Jesus e as crianças
Deixai vir a mim as crianças. Jesus abraçou, abençoou e honrou as crianças como modelo de fé para os adultos.
Isa akasema, "Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana ufalme wa mbinguni ni wa wale walio kama hawa."
Aliye mkuu katika Ufalme wa mbinguni
Wakati huo, wanafunzi wakamjia Isa na kumuuliza, "Je, nani aliye mkuu kuliko wote katika ufalme wa mbinguni?"
Isa akamwita mtoto mdogo na kumsimamisha katikati yao. Naye akasema: "Amin, nawaambia, msipoongoka na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika ufalme wa mbinguni. Kwa hiyo mtu yeyote anyenyekeaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika ufalme wa mbinguni.
Mfano wa kondoo aliyepotea
"Chungeni ili msimdharau mmoja wa hawa wadogo. Kwa maana nawaambia, malaika wao mbinguni daima wanauona uso wa Baba yangu aliye mbinguni. [
Lakini viongozi wa makuhani na walimu wa Torati walipoona mambo ya ajabu aliyofanya, na kuwasikia watoto wakishangilia katika eneo la Hekalu, wakisema, "Hosana Mwana wa Daudi," walikasirika.
Wakamuuliza Isa, "Je, unasikia hayo hawa wanayosema?"
Akawajibu, "Naam; kwani hamkusoma,
" ‘Midomoni mwa watoto wachanga na wanaonyonya
umeamuru sifa’?"
Amin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe." Akawachukua watoto mikononi mwake, akawakumbatia, akaweka mikono yake juu yao, akawabariki.
Kisha akamchukua mtoto mdogo, akamsimamisha katikati yao. Akamkumbatia, akawaambia, "Mtu yeyote amkaribishaye mmoja wa hawa watoto wadogo kwa Jina langu, anikaribisha mimi. Naye anikaribishaye mimi, amkaribisha Baba yangu aliyenituma."
Instruir e proteger
Instrui a criança no caminho de Deus. Elas são herança do Senhor — presentes sagrados que devemos educar com amor.
Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea,
naye hataiacha hata akiwa mzee.
Watoto wako wote watafundishwa na Mwenyezi Mungu,
nayo amani ya watoto wako itakuwa kuu.
Watoto ni urithi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu,
uzao ni zawadi kutoka kwake.
Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, kwa maana hii inampendeza Bwana Isa.
Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa.
Mafundisho kuhusu watoto na wazazi
Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana Isa, kwa kuwa hili ni jema. "Waheshimu baba yako na mama yako," hii ndio amri ya kwanza yenye ahadi, "upate baraka na uishi siku nyingi duniani."
Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, bali waleeni kwa nidhamu na mafundisho ya Bwana Isa.
" ‘ "Mwenyezi Mungu akubariki
na kukulinda;
Mwenyezi Mungu akuangazie nuru ya uso wake
na kukufadhili;
Mwenyezi Mungu akugeuzie uso wake
na kukupa amani." ’