Pular para o conteúdo
Publicidade

Dia dos avós

Por Bíblia Online

Os avós são tesouros vivos de sabedoria e fé. A Bíblia honra os mais velhos e celebra a transmissão de fé entre gerações — dos avós aos netos e destes aos que virão.

A bênção dos avós

A coroa dos velhos são os filhos dos filhos. A misericórdia de Deus é de geração em geração sobre os que o temem.

Wana wa wana ni taji la wazee,

nao wazazi ni fahari ya watoto wao.

Lakini kutoka milele hata milele

upendo wa Mwenyezi Mungu uko kwa wale wamchao,

nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:

Nilikuwa kijana na sasa ni mzee,

lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa

au watoto wao wakiombaomba chakula.

Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine,

watasimulia matendo yako makuu.

Kwa maana Mwenyezi Mungu ni mwema

na fadhili zake zadumu milele;

uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.

Força e fidelidade

Mesmo na velhice darão frutos. Os cabelos brancos são coroa de glória. Deus não abandona seus filhos na idade avançada.

Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda,

watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu,

wakitangaza, "Mwenyezi Mungu ni mkamilifu;

yeye ni Mwamba wangu,

na ndani yake hamna uovu."

Mvi ni taji la utukufu;

hupatikana kwa maisha ya uadilifu.

Hata wakati wa uzee wenu na mvi, Mimi ndiye,

Mimi ndiye nitakayewasaidia ninyi.

Nimewahuluku, nami nitawabeba,

nitawahudumia ninyi na kuwaokoa.

Hata vijana huchoka na kulegea,

nao vijana wanaume hujikwaa na kuanguka,

bali wale wamtumainio Mwenyezi Mungu

atafanya upya nguvu zao.

Watapaa juu kwa mabawa kama tai;

watapiga mbio wala hawatachoka,

watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

Mwe waangalifu na makini ili msije mkasahau mambo ambayo mliyaona kwa macho yenu, wala kuyaacha yaondoke mioyoni mwenu siku zote za uhai wenu. Mwafundishe hayo watoto wenu na watoto wao baada yao.

Seja o primeiro