Dia dos pais
O Dia dos Pais celebra o amor e o sacrifício paterno. A Bíblia honra os pais como provedores, protetores e guias espirituais que moldam as próximas gerações.
O pai que educa
Instrui a criança no caminho em que deve andar. O pai justo educa com amor, firmeza e o exemplo de uma vida íntegra.
Mfundishe mtoto njia impasayo kuiendea,
naye hataiacha hata akiwa mzee.
Yeye asiyetumia fimbo yake hampendi mwanawe,
bali yeye ampendaye
huwa mwangalifu kumwadibisha.
Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama,
wamebarikiwa watoto wake baada yake.
Baba wa mwenye haki ana furaha kubwa,
naye aliye na mwana mwenye hekima humfurahia.
Yeye amchaye Mwenyezi Mungu ana ngome salama,
na kwa watoto wake itakuwa kimbilio.
Honra e alegria
Honra a teu pai e tua mãe. Os filhos são herança do Senhor, e a família que serve a Deus junta é inabalável.
Waheshimu baba yako na mama yako, ili upate kuishi siku nyingi katika nchi anayokupa Mwenyezi Mungu, Mungu wako.
Watoto ni urithi unaotoka kwa Mwenyezi Mungu,
uzao ni zawadi kutoka kwake.
Kama mishale mikononi mwa shujaa
ndivyo walivyo wana awazaao mtu katika ujana wake.
Heri mtu ambaye podo lake
limejazwa nao.
Hawataaibishwa wanaposhindana
na adui zao langoni.
Lakini msipoona vyema kumtumikia Mwenyezi Mungu, chagueni hivi leo mtakayemtumikia, kama ni miungu ile baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Frati, au miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Mwenyezi Mungu."
Maneno ya mwisho
Kesheni; simameni imara katika imani; kuweni mashujaa na hodari.
Basi akaondoka, akaenda kwa baba yake.
"Lakini alipokuwa bado yuko mbali, baba yake akamwona, moyo wake ukajawa na huruma. Akamkimbilia mwanawe, akamkumbatia na kumbusu.
"Yule mwana akamwambia baba yake, ‘Baba, nimekosa mbele za Mungu na mbele yako. Sistahili kuitwa mwanao tena.’
"Lakini baba yake akawaambia watumishi, ‘Leteni upesi joho lililo bora sana, tieni pete kidoleni mwake na viatu miguuni mwake. Leteni ndama aliyenona, mkamchinje ili tuwe na karamu, tule na kufurahi.