Dificuldades
As dificuldades são parte da vida, mas Deus é refúgio certo em todo tempo de angústia. A Bíblia promete que nenhuma adversidade pode separar os filhos de Deus do seu amor.
Deus é refúgio
Deus é nosso refúgio e fortaleza, socorro bem presente nas angústias. Nada poderá nos separar do amor de Cristo.
Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,
msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa,
na milima ianguke kilindini cha bahari,
hata maji yake yakinguruma na kuumuka,
na milima itetemeke kwa mawimbi yake.
Nitasema kumhusu Mwenyezi Mungu, "Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu, ninayemtumaini."
Enyi watu, mtumainini yeye wakati wote,
miminieni mioyo yenu kwake,
kwa kuwa Mungu ni kimbilio letu.
Mwenyezi Mungu ni kimbilio la wanaodhulumiwa,
ni ngome imara wakati wa shida.
Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe,
kwa maana wewe Mwenyezi Mungu,
hujawaacha kamwe wanaokutafuta.
Wewe unatawala bahari yenye msukosuko;
mawimbi yake yanapoinuka, wewe unayatuliza.
Yeye ni mkuu kuliko ngurumo ya maji makuu,
ni mkuu kuliko mawimbi ya bahari:
Mwenyezi Mungu aishiye juu sana ni mkuu.
Akatuliza dhoruba kwa mnong’ono,
mawimbi ya bahari yakatulia.
Ni nani atakayetutenga na upendo wa Al-Masihi? Je, ni shida au taabu au mateso au njaa au uchi au hatari au upanga? Kama ilivyoandikwa:
"Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa;
tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa."
Lakini katika mambo haya yote tu zaidi ya washindi kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua kwa hakika ya kuwa sio mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuja, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chochote zitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Al-Masihi Isa, Bwana wetu.
Provisão nas dificuldades
O Senhor provê mesmo nos tempos mais difíceis. Ele sustentou Elias, protegeu Israel e cuida dos seus com fidelidade eterna.
Kwa kuwa kile chungu hakikuisha unga na ile chupa ya mafuta haikukauka sawasawa na lile neno la Mwenyezi Mungu lililonenwa na Ilya.
Alitandaza wingu kama kifuniko,
na moto kuwamulikia usiku.
Waliomba, naye akawaletea kware,
akawashibisha kwa mkate wa mbinguni.
Alipasua mwamba, maji yakabubujika,
yakatiririka jangwani kama mto.
Nilikuwa kijana na sasa ni mzee,
lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa
au watoto wao wakiombaomba chakula.
Mwenyezi Mungu anazifahamu siku za wanyofu,
na urithi wao utadumu milele.
Siku za maafa hawatanyauka,
siku za njaa watafurahia wingi wa vitu.
Kwa maana nitamimina maji juu ya nchi yenye kiu,
na vijito vya maji juu ya ardhi iliyokauka;
nitamimina Roho wangu Mtakatifu juu ya watoto wako,
nayo baraka yangu juu ya wazao wako.
Umekuwa kimbilio la watu maskini,
kimbilio la mhitaji katika taabu yake,
hifadhi wakati wa dhoruba
na kivuli wakati wa hari.
Kwa maana pumzi ya wakatili
ni kama dhoruba ipigayo ukuta
Utakuwa sitara na kivuli kutokana na joto la mchana, na kuwa mahali pa kujificha kutokana na dhoruba na mvua.
Unapopita kwenye maji makuu,
nitakuwa pamoja nawe,
unapopita katika mito ya maji,
hayatakugharikisha.
Utakapopita katika moto,
hutaungua,
miali ya moto haitakuunguza.
Força nas provas
Em tudo somos atribulados, mas não esmagados. O Senhor é bom e é fortaleza no dia da angústia — Ele conhce os seus.
Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa; twateswa lakini hatuachwi; twatupwa chini lakini hatupondwi.
Mwenyezi Mungu ni Mwema,
kimbilio wakati wa taabu.
Huwatunza wale wanaomtegemea,
Huyafungia maji kwenye mawingu yake,
hata hivyo mawingu hayapasuki kwa uzito wake.
Huufunika uso wa mwezi mpevu,
akitandaza mawingu juu yake.
Amechora mstari wa upeo juu ya maji,
ameweka mpaka wa nuru na giza.
Utalindwa kutokana na kichapo cha ulimi,
wala hutakuwa na sababu ya kuogopa maangamizi yatakapokujia.
Naye Isa akawaambia, "Kwa nini mnaogopa, enyi wa imani haba?" Kisha akaamka na kukemea dhoruba na mawimbi, nayo bahari ikatulia kabisa.
Wale watu wakashangaa, wakisema, "Ni mtu wa namna gani huyu? Hata upepo na mawimbi vinamtii!"
Basi ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya shambani, ambayo leo yapo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavika ninyi vizuri zaidi, enyi wa imani haba? Kwa hiyo msiwe na wasiwasi, mkisema, ‘Tutakula nini?’ au ‘Tutakunywa nini?’ au ‘Tutavaa nini?’
Yule mwanamke akakimbilia jangwani, ambako Mungu alikuwa amemtayarishia mahali ili apate kutunzwa huko kwa muda wa siku elfu moja mia mbili na sitini.
Tazama nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na juu ya nguvu zote za adui; wala hakuna kitu chochote kitakachowadhuru.