Dívidas
As dívidas podem escravizar, mas a Bíblia nos ensina princípios de sabedoria financeira: não se endividar imprudentemente, pagar o que se deve e confiar em Deus como provedor.
O devedor é servo do credor
O rico domina sobre o pobre, e o que toma emprestado é servo do que empresta. A Bíblia convida à liberdade financeira.
Tajiri humtawala maskini,
Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.
Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao,
Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.
Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka;
Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa.
Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
Princípios financeiros
Pagai a todos o que lhes é devido. Deus promete que o justo não será desamparado e que a bênção virá sobre os obedientes.
Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.
Msiwiwe na mtu chochote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
Asiye haki hukopa wala halipi,
Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu.
Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, haketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia?
Mpe kila akuombaye, na akunyang’anyaye vitu vyako, usitake akurudishie.
Utusamehe deni zetu,
kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
Contentamento
Seja o vosso viver sem ganância, contentando-vos com o que tendes. O Senhor é suficiente — não nos desamparará.
Msiwe na tabia ya kupenda fedha; muwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kamwe, wala sitakuacha.
Kwani BWANA, Mungu wako, atakubarikia, kama alivyokuahidi; nawe utakopesha mataifa mengi, lakini hutakopa; tena utayatawala mataifa mengi, usitawaliwe na wao.