Pular para o conteúdo
Publicidade

Ezekieli 25

Tangazo juu ya Amoni

1 Yer 49:1-6;Eze 21:28-32;Amo 1:13-15;Sef 2:8-11 Neno la BWANA likanijia, kusema, 2 Yer 49:1;Amo 1:13;Sef 2:9 Mwanadamu, uwaelekezee wana wa Amoni uso wako, ukatabiri juu yao. 3 Mit 17:5 Uwaambie hao wana wa Amoni, Lisikieni neno la Bwana MUNGU; Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu umesema, Aha! Juu ya patakatifu pangu, palipotiwa unajisi; na juu ya nchi ya Israeli, ilipoharibiwa; na juu ya nyumba ya Israeli, walipokwenda kifungoni; 4 Mwa 45:18 basi, kwa sababu hiyo, nitakutia katika mikono ya wana wa mashariki uwe milki yao, nao watajenga kambi yao ndani yako, kufanya maskani zao ndani yako; watakula matunda yako, na kunywa maziwa yako. 5 2 Sam 12:26;Isa 13:21;Eze 21:20;Sef 2:14 Nami nitafanya Raba kuwa banda la ngamia, na wana wa Amoni kuwa mahali pa kulaza makundi; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. 6 Maana Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu umepiga makofi, na kupiga mshindo kwa miguu yako, na kufurahi juu ya nchi ya Israeli, jeuri yote ya roho yako; 7 basi, tazama, nimenyosha mkono wangu juu yako, nami nitakutoa uwe mateka ya mataifa; nami nitakukatilia mbali na makabila ya watu, nami nitakuangamiza, usiwe katika nchi hizo; nitakukomesha; nawe utajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.

Utabiri juu ya Moabu

8 Kum 2:4,5; Isa 15:1—16:14;25:10-12;Yer 48:1-47;Amo 2:1-3;Sef 2:8-11 Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu Moabu na Seiri husema, Tazama, nyumba ya Israeli ni sawasawa na mataifa yote; 9 basi, tazama, nitawafunulia wana wa mashariki ubavu wa Moabu toka miji yake, toka miji yake iliyo mipakani mwake, utukufu wa nchi hiyo, Beth-yeshimothi, na Baal-meoni, na Kiriathaimu, 10 pamoja na wana wa Amoni, nami nitawatoa kuwa milki, ili wana wa Amoni wasikumbukwe kati ya mataifa, 11 nami nitatoa hukumu juu ya Moabu; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA.

Utabiri juu ya Edomu

12 2 Nya 28:17;Zab 137:7;Omb 4:22;Isa 34:5-17;63:1-6;Yer 49:7-22;Eze 35:1-15;Amo 1:11-12;Oba 1-14;Mal 1:2-5 Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa Edomu wametenda kinyume cha nyumba ya Yuda, kwa kujilipiza kisasi, nao wamekosa sana, na kujilipiza kisasi juu yao; 13 kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Nitanyosha mkono wangu juu ya Edomu, nitakatilia mbali nayo wanadamu na wanyama; nami nitaifanya kuwa ukiwa toka Temani; na mpaka Dedani wataanguka kwa upanga. 14 Isa 11:14 Nami nitaweka kisasi changu juu ya Edomu, kwa mkono wa watu wangu Israeli; nao watatenda mambo katika Edomu, kwa kadiri ya hasira yangu, na ghadhabu yangu, nao watakijua kisasi changu, asema Bwana MUNGU.

Utabiri juu ya Filistia

15 Isa 14:29-31;Yer 47:1-7;25:20;Yoe 3:4-8;Amo 1:6-8;Sef 2:4-7;Zek 9:5-7 Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa Wafilisti wametenda mambo kwa kujilipiza kisasi, nao wamejilipiza kisasi kwa moyo wa ujeuri, ili kupaangamiza kwa uadui wa daima; 16 1 Sam 30:14 kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, nitanyosha mkono wangu juu ya Wafilisti, nami nitawakatilia mbali Wakerethi, na kuwaharibu wabakio pande za pwani. 17 Zab 9:16;Isa 26:11;Eze 6:7 Nami nitajilipiza kisasi kikuu, nikiwakemea kwa ukali; nao watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapojilipiza kisasi juu yao.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também