Pular para o conteúdo
Publicidade

Ezekieli 15

Mzabibu usiofaa

1 Neno la BWANA likanijia, kusema, 2 Zab 80:8;Hos 10:1 Mwanadamu, mzabibu una sifa gani kuliko mti mwingine, au tawi la mzabibu lililokuwa kati ya miti ya msituni? 3 Je! Mti wake waweza kutwaliwa, ili kufanya kazi yoyote? Watu waweza kufanya chango kwa huo, ili kutundika chombo chochote? 4 Yn 15:6 Tazama, watupwa motoni kuwa kuni moto unapoziteketeza ncha zake zote mbili, nao umeteketea katikati, je! Wafaa kwa kazi yoyote? 5 Tazama, ulipokuwa mzima, haukufaa kwa kazi yoyote; sembuse ukiisha kuliwa na moto, na kuteketea; je! Waweza kufaa kwa kazi yoyote? 6 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kama mzabibu kati ya miti ya msituni, niliyoupa moto uwe kuni, ndivyo nitakavyowatoa wakaao Yerusalemu. 7 Law 17:10;Zab 34:16;Yer 21:10;48:43,44;Isa 24:18;Amo 5:19;Eze 6:7;7:4 Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoukaza uso wangu juu yao. 8 Nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, kwa sababu wamekosa, asema Bwana MUNGU.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também