Publicidade

Encorajamento

Por Bíblia Online

O encorajamento é uma das vocações mais lindas do cristão. A Bíblia transborda de palavras de ânimo: não temas, levanta-te, Eu sou contigo. Deus nos encoraja para encorajarmos outros.

Não temas

Deus diz repetidamente: não temas, Eu sou contigo. Ele fortalece, sustenta e caminha ao nosso lado em cada desafio.

Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;

usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.

Nitakutia nguvu na kukusaidia;

nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

Unapopita kwenye maji makuu,

nitakuwa pamoja nawe,

unapopita katika mito ya maji,

hayatakugharikisha.

Utakapopita katika moto,

hutaungua,

miali ya moto haitakuunguza.

Kwa kuwa wewe ni wa thamani na wa kuheshimiwa machoni pangu,

nami kwa kuwa ninakupenda,

nitatoa watu badala yako

na mataifa badala ya maisha yako.

Usiogope, kwa kuwa mimi nipo pamoja nawe,

nitawaleta watoto wako kutoka mashariki,

na kukukusanya kutoka magharibi.

"Usiogope, wewe hutaaibika.

Usiogope aibu, wewe hutaaibishwa.

Wewe utasahau aibu ya ujana wako,

wala hutakumbuka tena mashutumu ya ujane wako.

Hukumu na wokovu

"Nilijifunua kwa watu wale ambao hawakuniulizia.

Nimeonekana na watu wale ambao hawakunitafuta.

Kwa taifa lile ambalo halikuliita Jina langu,

nilisema, Niko hapa, niko hapa.

bali wale wamtumainio Mwenyezi Mungu

atafanya upya nguvu zao.

Watapaa juu kwa mabawa kama tai;

watapiga mbio wala hawatachoka,

watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

Kisha nikasikia sauti ya Bwana ikisema, "Nimtume nani? Ni nani atakayeenda kwa ajili yetu?"

Nami nikasema, "Mimi hapa. Nitume mimi!"

Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakuwa pamoja nawe popote utakapoenda."

Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, atakuwa pamoja nawe popote utakapoenda."

Ndipo hao watu wakajibu, "Hili jambo liwe mbali nasi la kumsahau Mwenyezi Mungu na kuitumikia miungu mingine! Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, mwenyewe ndiye alitutoa sisi na baba zetu akatupandisha kutoka Misri, kutoka nchi ile ya utumwa, na kutenda zile ishara kubwa mbele ya macho yetu. Ndiye aliyetulinda katika safari yetu yote na kutokana na mataifa yote ambayo tulipita katikati yao.

Kuweni imara na moyo wa ushujaa. Msiogope wala msifadhaike kwa sababu yao, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anaenda pamoja nanyi; kamwe hatawaacha wala hatawatupa ninyi."

Mwenyezi Mungu mwenyewe atakutangulia naye atakuwa pamoja nawe; kamwe hatakuacha wala hatakutupa. Usiogope, wala usifadhaike."

Deus está conosco

Se Deus é por nós, quem será contra nós? Tudo posso naquele que me fortalece. Ele nos encoraja pela sua presença.

Upendo wa Mwenyezi Mungu

Tuseme nini basi kuhusu haya? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani awezaye kuwa kinyume chetu?

Kwa maana hamkupokea roho ya utumwa iletayo hofu tena, bali mlipokea Roho wa kufanywa wana, ambaye kwa yeye twalia, "Abba, Baba."

Kila mmoja wetu inampasa kumpendeza jirani yake kwa mambo mema, ili kumjenga katika imani.

Mungu atoaye saburi na faraja awajalie ninyi roho ya umoja miongoni mwenu mnapomfuata Al-Masihi Isa,

Ninatamani sana kuwaona ili nipate kuwapa karama za rohoni ili mwe imara, au zaidi, ninyi pamoja nami tuweze kutiana moyo katika imani sisi kwa sisi.

Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Nina hakika kwamba yeye aliyeianza kazi njema mioyoni mwenu, ataiendeleza na kuikamilisha hata siku ya Al-Masihi Isa.

Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Al-Masihi, amekuwa kiumbe kipya: ya kale yamepita; tazama, yamekuwa mapya.

Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa utu wetu wa nje unachakaa, utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku.

Kwa maana dhiki yetu nyepesi iliyo ya kitambo inatutayarisha kwa ajili ya utukufu wa milele unaozidi kuwa mwingi kupita kiasi.

Lakini tunayo hazina hii katika vyombo vya udongo, ili ijulikane wazi kwamba uwezo huu wa ajabu unatoka kwa Mungu, wala si kwetu. Twataabika kila upande lakini hatuangamizwi; twaona wasiwasi lakini hatukati tamaa; twateswa lakini hatuachwi; twatupwa chini lakini hatupondwi. Siku zote twachukua katika mwili kufa kwake Isa ili uzima wa Isa uweze kudhihirishwa katika miili yetu. Kwa maana sisi tulio hai siku zote tumetolewa tufe kwa ajili ya Isa, ili uzima wake upate kudhihirishwa katika mwili wetu upatikanao na mauti.

Huduma ya upatanisho

Basi, kwa kuwa tunajua kumcha Mwenyezi Mungu, tunajitahidi kuwavuta wengine. Lakini Mungu anatufahamu dhahiri, nami natumaini kwamba tu dhahiri katika dhamiri zenu pia. Sio kwamba tunajaribu kujistahilisha kwenu tena, lakini tunataka kuwapa nafasi ili mwone fahari juu yetu, mweze kuwajibu hao wanaoona fahari kuhusu mambo yanayoonekana badala ya mambo yaliyo moyoni. Kama tumerukwa na akili, ni kwa ajili ya Mungu; kama tuna akili timamu, ni kwa ajili yenu. Kwa kuwa upendo wa Al-Masihi unatutia nguvu, kwa sababu tunasadiki kuwa mmoja alikufa kwa ajili ya wote, kwa hiyo wote walikufa. Naye alikufa kwa ajili ya watu wote, ili wote wanaoishi wasiishi tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa na kufufuliwa tena kwa ajili yao.

Hivyo tangu sasa hatumwangalii mtu yeyote kwa mtazamo wa kibinadamu. Ingawa wakati fulani tulimwangalia Al-Masihi kwa namna ya kibinadamu, hatumwangalii tena hivyo. Kwa hiyo mtu akiwa ndani ya Al-Masihi, amekuwa kiumbe kipya: ya kale yamepita; tazama, yamekuwa mapya. Haya yote yanatokana na Mungu, ambaye ametupatanisha sisi na nafsi yake kupitia kwa Isa Al-Masihi, na kutupatia sisi huduma ya upatanisho: kwamba Mungu alikuwa ndani ya Al-Masihi akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake mwenyewe, akiwa hawahesabii watu dhambi zao. Naye ametukabidhi sisi ujumbe huu wa upatanisho. Kwa hiyo sisi ni mabalozi wa Al-Masihi, kana kwamba Mungu anawasihi kupitia kwa vinywa vyetu. Nasi twawaomba sana ninyi kwa niaba ya Al-Masihi: mpatanishwe na Mungu. Kwa maana Mungu alimfanya yeye asiyekuwa na dhambi kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kufanywa haki ya Mungu kupitia kwake Al-Masihi.

Kwa kuwa kama nia ya kutoa ipo, kitolewacho kinakubalika kulingana na kile mtu alicho nacho, wala si kwa kile ambacho hana.

Mungu wa faraja yote

Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Isa Al-Masihi, Baba wa huruma na Mungu wa faraja yote. Yeye hutufariji katika taabu zetu, ili tuweze kuwafariji walio katika taabu yoyote kwa faraja ambayo sisi wenyewe tumepokea kutoka kwa Mungu.

Ânimo nas lutas

No mundo tereis aflições, mas tende bom ânimo — Eu venci o mundo. O Senhor é refúgio seguro em toda tribulação.

"Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu."

"Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu."

Amani nawaachia; amani yangu nawapa. Amani hii ninayowapa si kama ile ulimwengu unatoa. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.

Amani nawaachia; amani yangu nawapa. Amani hii ninayowapa si kama ile ulimwengu unatoa. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiogope.

Katika pendo hakuna hofu. Lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa sababu hofu inahusika na adhabu. Kila mwenye hofu hakukamilika katika pendo.

Promessas de conforto

Vinde a mim os cansados e sobrecarregados. Lança sobre Ele tuas ansiedades, pois Ele cuida de ti.

Isa awaita waliolemewa na mizigo

"Njooni kwangu, ninyi nyote mnaotaabika na kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho. Afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika Jehanamu.

Mtwike Mwenyezi Mungu fadhaa zako,

naye atakutegemeza,

hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.

Hata nikipita katikati

ya bonde la uvuli wa mauti,

sitaogopa mabaya,

kwa maana wewe upo pamoja nami;

fimbo yako na mkongojo wako

vyanifariji.

Hata nikipita katikati

ya bonde la uvuli wa mauti,

sitaogopa mabaya,

kwa maana wewe upo pamoja nami;

fimbo yako na mkongojo wako

vyanifariji.

Sala ya kusifu

Mwenyezi Mungu ni nuru yangu na wokovu wangu,

nimwogope nani?

Mwenyezi Mungu ni ngome ya uzima wangu,

nimhofu nani?

Mngojee Mwenyezi Mungu;

uwe hodari na mwenye moyo mkuu,

na umngojee Mwenyezi Mungu.

Kuweni hodari na mjipe moyo,

ninyi nyote mnaomtumaini Mwenyezi Mungu.

Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea;

nitakushauri na kukuangalia.

Mwenyezi Mungu yuko pamoja nasi

Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,

msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.

Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa,

na milima ianguke kilindini cha bahari,

hata maji yake yakinguruma na kuumuka,

na milima itetemeke kwa mawimbi yake.

Wakati ninaogopa,

nitakutumaini wewe.

Katika Mungu, ambaye neno lake ninalisifu,

katika Mungu ninatumaini, sitaogopa.

Mwanadamu mwenye kufa

atanitenda nini?

Wema wa Bwana Mungu wetu uwe juu yetu;

uzithibitishe kazi za mikono yetu:

naam, uzithibitishe kazi za mikono yetu.

Mwenyezi Mungu mlinzi wetu

Nayainua macho yangu natazama milima:

msaada wangu utatoka wapi?

Msaada wangu hutoka kwa Mwenyezi Mungu,

Muumba wa mbingu na dunia.

Nimemweka Mwenyezi Mungu mbele yangu daima.

Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,

sitatikisika.

Mwenyezi Mungu ni kimbilio la wanaodhulumiwa,

ni ngome imara wakati wa shida.

Wote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe,

kwa maana wewe Mwenyezi Mungu,

hujawaacha kamwe wanaokutafuta.

Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye anajishughulisha sana na mambo yenu.

Katika haya yote mnafurahi sana, ijapokuwa kwa muda mfupi sasa mmehuzunishwa kwa majaribu ya aina nyingi.

Kuvumilia mateso

Basi, ni nani atakayewadhuru mkiwa wenye juhudi katika kutenda mema? Lakini hata ikiwalazimu kuteseka kwa ajili ya haki, mmebarikiwa. "Msiogope vitisho vyao, wala msiwe na wasiwasi."

Encorajar uns aos outros

Encorajai-vos mutuamente e edificai-vos uns aos outros. Não desanimemos — a bondade do Senhor é nova a cada manhã.

Kwa hiyo farijianeni na kujengana, kama vile mnavyofanya sasa.

Kwa hiyo farijianeni na kujengana, kama vile mnavyofanya sasa.

Tuangaliane na kuhimizana sisi kwa sisi katika upendo na katika kutenda mema. Wala tusiache kukutana pamoja, kama wengine walivyo na desturi, bali tuhimizane sisi kwa sisi kadiri tuonavyo Siku ile inakaribia.

Yalindeni maisha yenu msiwe na tabia ya kupenda fedha, bali mridhike na vile mlivyo navyo, kwa sababu Mungu amesema,

"Kamwe sitakuacha,

wala sitakupungukia."

Kwa hiyo tunaweza kusema kwa ujasiri,

"Mwenyezi Mungu ni msaada wangu; sitaogopa.

Mwanadamu anaweza kunitenda nini?"

Kwa hiyo, ndugu zangu wapendwa, simameni imara. Msitikisike. Mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana Isa, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu katika Bwana Isa si bure.

Maneno ya mwisho

Kesheni; simameni imara katika imani; kuweni mashujaa na hodari.

Maneno ya mwisho

Kesheni; simameni imara katika imani; kuweni mashujaa na hodari.

Maana Mungu hakutupatia roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.

Daudi pia akamwambia Sulemani mwanawe, "Uwe hodari na moyo mkuu, ukafanye kazi hii. Usiogope wala usifadhaike, kwa maana Bwana Mwenyezi Mungu, aliye Mungu wangu, yu pamoja nawe. Hatakuacha wala hatakupungukia, hadi kazi hii yote kwa ajili ya utumishi wa Hekalu la Mwenyezi Mungu itakapokamilika.

Mwenyezi Mungu, Mungu wako, yu pamoja nawe,

yeye ni Shujaa mwenye nguvu anayeokoa.

Atakufurahia kwa furaha kubwa,

atakutuliza kwa pendo lake,

atakufurahia kwa kuimba."

Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu," asema Mwenyezi Mungu, "ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.

Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida,

bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu.

Isa akawaambia, "Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu." Mara wakaacha nyavu zao, wakamfuata.

Deus chama pelo nome

Ao longo da Bíblia, Deus chamou seus servos pelo nome — Abraão, Moisés, Samuel, Paulo — encorajando cada um pessoalmente.

Mungu akanena na Israeli katika maono usiku na kusema, "Yakobo! Yakobo!"

Akamjibu, "Mimi hapa."

Malaika wa Mungu akaniita katika ndoto, Yakobo.Nikamjibu, Mimi hapa.

Lakini malaika wa Mwenyezi Mungu akamwita kutoka mbinguni, akamwambia, "Ibrahimu! Ibrahimu!"

Akajibu, "Mimi hapa."

Mwenyezi Mungu alipoona kuwa amegeuka ili aone, Mungu akamwita kutoka ndani ya kile kichaka, "Musa! Musa!"

Naye Musa akajibu, "Mimi hapa."

lakini Eli akamwita na kumwambia, "Samweli mwanangu."

Samweli akamjibu, "Mimi hapa."

Huko Dameski kulikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Anania. Bwana Isa alimwita katika maono, "Anania!"

Akajibu, "Mimi hapa Bwana."

Mariamu akasema, "Tazama, mimi ni mtumishi wa Mwenyezi Mungu. Na iwe kwangu kama ulivyosema." Kisha malaika akaondoka, akamwacha.

Mnajua kwamba shomoro watano huuzwa kwa senti mbili? Lakini Mungu hamsahau hata mmoja wao. Naam, hata nywele za vichwa vyenu zote zimehesabiwa. Hivyo msiogope, kwa maana ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-