Esperar em Deus
Esperar em Deus não é passividade — é confiança ativa no Senhor que age no tempo perfeito. Os que esperam nele não serão confundidos nem envergonhados.
Esperança em Deus
Descanse somente em Deus, ó minha alma, pois dele vem a minha esperança. Ele é rocha e salvação — não serei abalado.
Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa utulivu.
Maana tumaini langu hutoka kwake.
Utulie mbele za BWANA,
Nawe umngojee kwa subira;
Usihangaike juu ya afanikiwaye katika njia yake,
Wala mtu apangaye maovu.
Maana watenda mabaya watakatiliwa mbali,
Bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi.
Wewe umngoje BWANA,
Uishike njia yake,
Naye atakutukuza uirithi nchi,
Utawaona Wasio haki wakiangamizwa.
Nilimngoja BWANA kwa subira,
Akaniinamia na kusikia kilio changu.
Nimemngoja BWANA, roho yangu imengoja,
Na neno lake nimelitumainia.
Nafsi yangu inamngoja Bwana,
Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi,
Naam, walinzi waingojao asubuhi.
Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja;
Wataaibika watendao uhaini bila sababu.
Kwa kuwa nakungoja Wewe, BWANA,
Wewe utajibu, Ee Bwana, Mungu wangu.
Umtumainie BWANA, uwe imara,
Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.
Confiança na espera
O Senhor é bom para os que esperam nele. O olho não viu o que Deus preparou para os que o amam e o aguardam.
bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Ee BWANA, uturehemu; tumekungoja wewe; uwe wewe mkono wetu kila asububi, na wokovu wetu pia wakati wa taabu.
Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye.
Usiseme, Mimi nitalipa mabaya;
Mngojee BWANA, naye atakuokoa.
Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho. Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.
jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.
Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo;