Publicidade

Salmos 38

Ombi la uponyaji kwa anayejuta kwa mateso

Zaburi ya Daudi, kwa matoleo ya kumbukumbu.

1 Ee BWANA, usinilaumu katika ghadhabu yako,

Wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako.

2 Kwa maana mishale yako imenichoma,

Na mkono wako umenipata.

3 Hamna uzima katika mwili wangu

Kwa sababu ya ghadhabu yako.

Wala hamna amani mifupani mwangu

Kwa sababu ya hatia zangu.

4 Maana dhambi zangu zimenifunika kichwa,

Kama mzigo mzito zimenilemea mno.

5 Majeraha yangu yananuka na kutunga usaha,

Kwa sababu ya upumbavu wangu.

6 Nimejipinda na kuinama sana,

Mchana kutwa ninaenda nikiomboleza.

7 Ayu 7:5 Maana viuno vyangu vimejaa homa,

Wala hamna uzima katika mwili wangu.

8 Nimedhoofika na kupondeka sana,

Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu.

9 Bwana, haja zangu zote ziko mbele zako,

Kuugua kwangu hakukusitirika kwako.

10 Moyo wangu unadundadunda,

Nguvu zangu zimenitoka;

Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka.

11 Lk 10:31 Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu;

Na jamaa zangu wanasimama mbali.

12 Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego;

Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya;

Na kufikiri hila mchana kutwa.

13 Lakini kama kiziwi sisikii,

Nami ni kama bubu asiyefumbua kinywa chake.

14 Naam, nimekuwa kama mtu asiyesikia,

Ambaye hamna ubishi kinywani mwake.

15 Yer 14:8 Kwa kuwa nakungoja Wewe, BWANA,

Wewe utajibu, Ee Bwana, Mungu wangu.

16 Maana nilisema, Wasije wakanifurahia;

Wale wanaojitukuza juu yangu Mguu wangu unapoteleza.

17 Kwa maana mimi ni karibu na kusita,

Na maumivu yangu yako mbele yangu daima.

18 Ayu 31:33;Zab 32:5;Mit 28:13;2 Kor 7:9 Kwa maana nitaungama uovu wangu,

Na kusikitika kwa dhambi zangu.

19 Lakini walio adui zangu bila sababu wana nguvu,

Nao wanaonichukia bure wamekuwa wengi.

20 1 Yoh 3:12;1 Pet 3:13 Naam, wakilipa mabaya kwa mema,

Huwa adui zangu kwa kuwa nilifuata lililo jema.

21 Zab 22:1,11 Wewe, BWANA, usiniache,

Mungu wangu, usijitenge nami.

22 Kut 15:2;Isa 12:2 Ufanye haraka kunisaidia,

Ee Bwana, wokovu wangu.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-