Esperar no Senhor
Esperar no Senhor é ato de fé e confiança. A Bíblia promete que os que esperam em Deus renovam as forças, recebem direção e experimentam a fidelidade divina no tempo certo.
Renovar as forças
Os que esperam no Senhor renovam as forças. Sobem como águias, correm e não se cansam, caminham e não se fatigam.
bali wale wamtumainio Mwenyezi Mungu
atafanya upya nguvu zao.
Watapaa juu kwa mabawa kama tai;
watapiga mbio wala hawatachoka,
watatembea kwa miguu wala hawatazimia.
Hata hivyo Mwenyezi Mungu anatamani kutupatia neema,
anainuka ili kuwaonesha huruma.
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni Mungu wa haki.
Wamebarikiwa wote wanaomngojea yeye!
Mngojee Mwenyezi Mungu;
uwe hodari na mwenye moyo mkuu,
na umngojee Mwenyezi Mungu.
Nami bado nina tumaini hili:
nitauona wema wa Mwenyezi Mungu
katika nchi ya walio hai.
Mngojee Mwenyezi Mungu;
uwe hodari na mwenye moyo mkuu,
na umngojee Mwenyezi Mungu.
Sala ya kusifu
Mwenyezi Mungu ni nuru yangu na wokovu wangu,
nimwogope nani?
Mwenyezi Mungu ni ngome ya uzima wangu,
nimhofu nani?
Waovu watakaposogea dhidi yangu
ili wale nyama yangu,
adui zangu na watesi wangu watakaponishambulia,
watajikwaa na kuanguka.
Hata jeshi linizingire pande zote,
moyo wangu hautaogopa;
hata vita vitokee dhidi yangu,
hata hapo nitakuwa na ujasiri.
Jambo moja ninamwomba Mwenyezi Mungu,
hili ndilo ninalolitafuta:
niweze kukaa nyumbani mwa Mwenyezi Mungu
siku zote za maisha yangu,
niutazame uzuri wa Mwenyezi Mungu
na kumtafuta hekaluni mwake.
Kwa kuwa siku ya shida,
atanihifadhi salama katika maskani yake,
atanificha uvulini mwa hema lake,
na kuniweka juu kwenye mwamba.
Kisha kichwa changu kitainuliwa
juu ya adui zangu wanaonizunguka.
Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe;
nitamwimbia Mwenyezi Mungu na kumsifu.
Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Mwenyezi Mungu,
unihurumie na unijibu.
Moyo wangu unasema kuhusu wewe,
"Utafute uso wake!"
Uso wako, Mwenyezi Mungu "Nitautafuta."
Usinifiche uso wako,
usimkatae mtumishi wako kwa hasira;
wewe umekuwa msaada wangu.
Usinikatae wala usiniache,
Ee Mungu Mwokozi wangu.
Hata baba yangu na mama yangu wakiniacha,
Mwenyezi Mungu atanipokea.
Nifundishe njia yako, Ee Mwenyezi Mungu,
niongoze katika njia iliyo nyoofu,
kwa sababu ya watesi wangu.
Usiniachilie kwa nia za adui zangu,
kwa maana mashahidi wa uongo
wameinuka dhidi yangu,
wakipumua ujeuri.
Nami bado nina tumaini hili:
nitauona wema wa Mwenyezi Mungu
katika nchi ya walio hai.
Mngojee Mwenyezi Mungu;
uwe hodari na mwenye moyo mkuu,
na umngojee Mwenyezi Mungu.
Espera paciente
Esperei com paciência no Senhor e Ele se inclinou para mim. Confie nele e descanse — Ele agirá no tempo certo.
Wimbo wa sifa
Nilimngoja Mwenyezi Mungu kwa saburi,
naye akanijia na kusikia kilio changu.
Akanipandisha kutoka shimo la uharibifu,
kutoka matope na utelezi;
akaiweka miguu yangu juu ya mwamba
na kunipa mahali imara pa kusimama.
Akaweka wimbo mpya kinywani mwangu,
wimbo wa sifa kwa Mungu wetu.
Wengi wataona na kuogopa
na kuweka tumaini lao kwa Mwenyezi Mungu.
Heri mtu yule amfanyaye Mwenyezi Mungu kuwa tumaini lake,
asiyewategemea wenye kiburi,
wale wenye kugeukia miungu ya uongo.
Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu,
umefanya mambo mengi ya ajabu.
Mambo uliyopanga kwa ajili yetu
hakuna awezaye kukuhesabia;
kama ningesema na kuyaelezea,
yangekuwa mengi mno kuyatangaza.
Dhabihu na sadaka hukuvitaka,
lakini umefungua masikio yangu;
sadaka za kuteketezwa na sadaka za dhambi
hukuzihitaji.
Ndipo niliposema, "Mimi hapa, nimekuja:
imeandikwa kunihusu katika kitabu.
Ee Mungu wangu,
natamani kuyafanya mapenzi yako;
sheria yako iko ndani ya moyo wangu."
Nimehubiri haki katika kusanyiko kubwa,
sikufunga mdomo wangu,
Ee Mwenyezi Mungu, kama ujuavyo.
Sikuficha haki yako moyoni mwangu;
ninasema juu ya uaminifu wako na wokovu wako.
Sikuficha upendo wako na kweli yako
mbele ya kusanyiko kubwa.
Ee Mwenyezi Mungu, usinizuilie huruma zako,
upendo wako na kweli yako daima vinilinde.
Kwa maana taabu zisizohesabika zimenizunguka,
dhambi zangu zimenikamata, hata nisiweze kuona.
Zimekuwa nyingi kuliko nywele za kichwa changu,
nao moyo unazimia ndani yangu.
Ee Mwenyezi Mungu, uwe radhi kuniokoa;
Ee Mwenyezi Mungu, njoo hima unisaidie.
Wote wanaotafuta kuniua,
waaibishwe na kufadhaishwa;
wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,
wafukuzwe mbali kwa aibu.
Sisi tunamngojea Mwenyezi Mungu kwa matumaini,
yeye ni msaada wetu na ngao yetu.
Mioyo yetu humshangilia,
kwa maana tunalitumainia jina lake takatifu.
Upendo wako usio na mwisho ukae juu yetu, Ee Mwenyezi Mungu,
tunapoliweka tumaini letu kwako.
Namngojea Mwenyezi Mungu, nafsi yangu inangojea,
katika neno lake naweka tumaini langu.
Nafsi yangu inamngojea Bwana
kuliko walinzi waingojeavyo asubuhi,
naam, kuliko walinzi
waingojeavyo asubuhi.
Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake,
tumaini langu latoka kwake.
Mngojee Mwenyezi Mungu,
na uishike njia yake.
Naye atakutukuza uirithi nchi,
waovu watakapokatiliwa mbali,
utaliona hilo.
Confiança e perseverança
Confie no Senhor de todo o coração. Sede pacientes na tribulação — o Senhor é fiel e cumprirá todas as suas promessas.
Mtumaini Mwenyezi Mungu kwa moyo wako wote
wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
katika njia zako zote mkiri yeye,
naye atayanyoosha mapito yako.
Si hivyo tu, bali twafurahi pia katika mateso, kwa sababu tunajua kuwa mateso huleta saburi, nayo saburi huleta uthabiti wa moyo, na uthabiti wa moyo huleta tumaini,
mkiwa mmetiwa nguvu kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu yake yenye utukufu, ili mpate kuwa na wingi wa saburi na uvumilivu. Nanyi kwa furaha
Uvumilivu katika mateso
Kwa hiyo, ndugu zangu, vumilieni hadi kuja kwake Bwana Isa. Tazameni jinsi mkulima angojavyo ardhi itoe mavuno yake yaliyo ya thamani, na jinsi anavyovumilia kwa ajili ya kupata mvua ya kwanza na ya mwisho. Ninyi nanyi vumilieni, tena simameni imara, kwa sababu kuja kwa Bwana Isa kumekaribia.
Kama mnavyojua, tunawahesabu wale waliovumilia kuwa wabarikiwa. Mmesikia habari za uvumilivu wake Ayubu, na mmeona kile ambacho hatimaye Mwenyezi Mungu alimtendea. Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma, na amejaa rehema.
Basi kwa kuwa mmejitakasa nafsi zenu kwa kuitii ile kweli hata mkawa na upendo wa ndugu usio na unafiki, basi pendaneni kwa dhati kutoka moyoni. Kwa maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu inayoharibika, bali kwa mbegu isiyoharibika, kupitia kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu milele. Maana,
"Wanadamu wote ni kama majani,
nao utukufu wao wote ni kama maua ya kondeni;
majani hunyauka na maua huanguka,
lakini neno la Mwenyezi Mungu ladumu milele."
Hili ndilo neno lililohubiriwa kwenu.
Mwenyezi Mungu hakawii kuitimiza ahadi yake, kama watu wengine wanavyokudhani kukawia. Badala yake, yeye anawavumilia ninyi, maana hataki mtu yeyote aangamie, bali kila mtu afikilie toba.
Mfano wa wanawali kumi
"Wakati huo, ufalme wa mbinguni utakuwa kama wanawali kumi waliochukua taa zao na kwenda kumlaki bwana arusi. Watano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara. Wale wapumbavu walichukua taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba, lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo. Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala.
"Usiku wa manane pakawa na kelele: ‘Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje mkamlaki!’
"Ndipo wale wanawali wote wakaamka na kuzitengeneza taa zao. Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni mafuta yenu kidogo; taa zetu zinazimika.’
"Lakini wale wenye busara wakawajibu, ‘Sivyo, hayatutoshi sisi na ninyi pia. Afadhali mwende kwa wauzao mkajinunulie mafuta yenu.’
"Nao walipokuwa wakienda kununua mafuta, bwana arusi akafika. Wale wanawali waliokuwa tayari wakaingia ndani pamoja naye kwenye karamu ya arusi na mlango ukafungwa.
"Baadaye wale wanawali wengine nao wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!’
"Lakini yeye bwana arusi akawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!’
"Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa.