Pular para o conteúdo
Publicidade

Estudar a Bíblia

Por Bíblia Online

Estudar a Bíblia é mergulhar na mente de Deus. A Palavra é lâmpada para os pés, espada do Espírito e alimento para a alma. O cristão que estuda cresce em sabedoria e maturidade.

A importância do estudo

Os bereanos eram mais nobres porque examinavam as Escrituras diariamente. Estudar a Bíblia é mandamento e privilégio.

Hawa Waberoya walikuwa waungwana kuliko wale wa Thesalonike, kwa kuwa waliupokea ule ujumbe kwa shauku kubwa na kuyachunguza Maandiko kila siku ili kuona kama yale Paulo aliyosema yalikuwa kweli.

Jitahidi kujionesha kwa Mungu kuwa umekubaliwa naye, mtendakazi asiye na sababu ya kuona aibu, ukilitumia kwa usahihi neno la kweli.

na jinsi tangu utoto umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yanaweza kukuhekimisha upate wokovu kupitia kwa imani katika Al-Masihi Isa. Maandiko yote yamevuviwa na Mungu, na yafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kwa kuwaongoza na kwa kuwafundisha katika haki, ili mtu wa Mungu awe amekamilishwa, apate kutenda kila kazi njema.

Fanya bidii kusoma Maandiko hadharani, kuhubiri na kufundisha, hadi nitakapokuja.

Ninyi mnachunguza Maandiko mkidhani ya kuwa ndani yake mna uzima wa milele. Maandiko haya ndio yanayonishuhudia mimi.

Meditar e guardar

Não se aparte a lei do Senhor da tua boca. Medita nela de dia e de noite para que cumpras tudo o que nela está escrito.

Usiache Kitabu hiki cha Torati kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi.

Nuru katika Torati ya Mwenyezi Mungu

Neno lako ni taa ya miguu yangu

na mwanga katika njia yangu.

Kuipenda Torati ya Mwenyezi Mungu

Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu.

Ninaitafakari mchana kutwa.

Amri zako zimenipa hekima kuliko adui zangu,

kwa kuwa nimezishika daima.

Nina akili kuliko walimu wangu wote,

kwa kuwa ninatafakari kuhusu sheria zako.

Kutii Torati ya Mwenyezi Mungu

Kijana aisafishe njia yake jinsi gani?

Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.

Ninakutafuta kwa moyo wangu wote,

usiniache niende mbali na amri zako.

Nimelificha neno lako moyoni mwangu

ili nisikutende dhambi.

Uhimidiwe, Ee Mwenyezi Mungu;

nifundishe maagizo yako.

Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote

zinazotoka katika kinywa chako.

Ninafurahia kufuata sheria zako

kama mtu afurahiaye mali nyingi.

Ninatafakari maagizo yako

na kuziangalia njia zako.

Ninafurahia maagizo yako,

wala sitalipuuza neno lako.

Nitakusifu kwa moyo mnyofu

ninapojifunza sheria zako za haki.

Estudo diligente

Esdras preparou o coração para buscar e ensinar a lei. O estudo exige disciplina, constância e coração aberto.

Ezra alianza safari yake kutoka Babeli siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza, naye akawasili Yerusalemu siku ya kwanza ya mwezi wa tano, kwa kuwa mkono wa neema wa Mungu wake ulikuwa juu yake. Kwa maana Ezra alikuwa amejitoa kwa moyo wote kujifunza na kushika Torati ya Mwenyezi Mungu na kuwafundisha Waisraeli amri na sheria zake.

Mpende Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. Wafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo. Zifunge kama alama juu ya mkono wako, na uzifunge juu ya paji la uso wako. Ziandike kwenye miimo ya milango ya nyumba yako na juu ya malango yako.

Atakapokuwa amekalia kiti cha ufalme wake, ajiandikie kwenye kitabu nakala ya sheria kwa ajili yake mwenyewe kutoka zile sheria za makuhani ambao ni Walawi. Atakuwa na nakala hiyo, naye ataisoma siku zote za maisha yake ili ajifunze kumheshimu Mwenyezi Mungu, Mungu wake, na kufuata kwa uangalifu maneno yote ya sheria hii na amri hizi, naye asijione kuwa ni bora kuliko ndugu zake na kuipotosha sheria. Ndipo yeye na wazao wake watatawala katika ufalme wake kwa muda mrefu katika Israeli.

Mithali za Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli:

Kwa kupata hekima na nidhamu;

kwa kufahamu maneno ya busara;

kwa kujipatia nidhamu na busara,

kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea;

huwapa busara wajinga,

maarifa na akili kwa vijana;

wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao,

wenye kupambanua na wapate mwongozo;

kwa kufahamu mithali na mifano,

misemo na vitendawili vya wenye hekima.

Faida nyingine za hekima

Mwanangu, usisahau mafundisho yangu,

bali zitunze amri zangu moyoni mwako,

kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako

na kukuletea mafanikio.

Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;

mshike, maana yeye ni uzima wako.

Kwa maana amri hii ni taa,

mafundisho haya ni mwanga,

na maonyo ya nidhamu

ni njia ya uzima,

Proteção e crescimento

Quem ignora a Palavra perece. Toda Escritura é útil — crescei na graça e no conhecimento do nosso Senhor.

watu wangu wanaangamizwa

kwa kukosa maarifa.

"Kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa,

mimi nami nitakukataa wewe

usiwe kuhani kwangu mimi;

kwa kuwa umeacha kuijali Torati ya Mungu wako

mimi nami sitawajali watoto wako.

Kwa sheria na kwa ushuhuda! Kama hawatasema sawasawa na neno hili, hawana mwanga wa mapambazuko.

Isa akawajibu, "Je, hampotei kwa sababu hamfahamu Maandiko wala uweza wa Mungu?

Kwa maana kila kitu kilichoandikwa zamani, kiliandikwa kutufundisha, ili kwa saburi na faraja tunayopata katika Maandiko tuwe na tumaini.

Basi, ninyi wapendwa, kwa kuwa mmekwisha kujua mambo haya, jilindeni msije mkachukuliwa na kosa la watu hao waasi na kuanguka kutoka kwa uthabiti wenu. Bali kueni katika neema na katika kumjua Bwana na Mwokozi wetu Isa Al-Masihi.

Utukufu una yeye sasa na milele! Amen.

Kwa habari ya wokovu huu, wale manabii waliosema kuhusu neema ambayo ingewafikia ninyi, walitafuta kwa bidii na kwa uangalifu mkubwa. Walijaribu kujua ni wakati upi na ni mazingira yapi ambayo Roho wa Al-Masihi, aliyekuwa ndani yao, alionesha alipotabiri mateso ya Al-Masihi na utukufu ambao ungefuata.

Seja o primeiro