Publicidade

Sinais do fim dos tempos

Por Bíblia Online

A Bíblia descreve sinais que precederão a volta de Jesus. Guerras, falsos mestres, sinais cósmicos e a pregação do evangelho a todas as nações — tudo aponta para o fim dos tempos.

Sinais proféticos

Este evangelho do Reino será pregado em todo o mundo e então virá o fim. Os sinais dos últimos tempos já se manifestam.

Injili hii ya ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utakapokuja.

Kuja kwa Mwana wa Adamu

"Mara baada ya dhiki ya siku zile,

" jua litatiwa giza,

nao mwezi hautatoa nuru yake;

nazo nyota zitaanguka kutoka angani,

na nguvu za anga zitatikisika.

"Ndipo itakapotokea ishara ya Mwana wa Adamu angani, na makabila yote ya dunia yataomboleza. Nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya angani, katika uwezo na utukufu mkuu. Naye atawatuma malaika wake kwa sauti kuu ya tarumbeta, nao watawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwisho mwingine.

"Basi kesheni, kwa sababu hamjui ni siku gani atakapokuja Bwana wenu. Lakini fahamuni jambo hili: Kama mwenye nyumba angejua ni wakati gani wa usiku ambao mwizi atakuja, angekesha na hangekubali nyumba yake kuvunjwa. Kwa hiyo ninyi pia hamna budi kuwa tayari, kwa sababu Mwana wa Adamu atakuja saa msiyotazamia.

nanyi wafundisheni kuyashika mambo yote niliyowaamuru ninyi. Hakika mimi niko pamoja nanyi siku zote, hadi mwisho wa nyakati."

Hakuna ajuaye siku wala saa

"Kwa habari ya siku ile na saa hakuna yeyote ajuaye, hata malaika walio mbinguni wala Mwana, ila Baba peke yake.

Os últimos dias

Nos últimos dias virão tempos difíceis, homens amantes de si mesmos. Mas derramarei o meu Espírito sobre toda a carne.

Hatari za siku za mwisho

Lakini yakupasa ufahamu jambo hili: kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari. Kwa maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kumkufuru Mungu, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio watakatifu, wasio na upendo, wasiopenda kupatanishwa, wasingiziaji, wasiozuia tamaa zao, wakatili, wasiopenda mema, wasaliti, wakaidi, waliojaa majivuno, wanaopenda anasa kuliko kumpenda Mungu: wakiwa na mfano wa utauwa kwa nje, lakini wakizikana nguvu za Mungu. Jiepushe na watu kama hao.

" Katika siku za mwisho, asema Mungu,

nitamimina Roho wangu

juu ya wote wenye mwili.

Wana wenu wa kiume na wa kike watatabiri,

vijana wenu wataona maono,

na wazee wenu wataota ndoto.

Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake,

katika siku zile nitamimina Roho wangu,

nao watatabiri.

Nami nitaonesha maajabu juu mbinguni,

na ishara chini duniani:

damu, moto, na mawimbi ya moshi.

Jua litakuwa giza

na mwezi utakuwa mwekundu kama damu,

kabla ya kuja siku ile kuu ya Mwenyezi Mungu

iliyo tukufu.

Na kila mtu atakayeliitia

jina la Mwenyezi Mungu, ataokolewa.

Siku ya Mwenyezi Mungu

"Hata itakuwa, baada ya hayo,

nitamimina Roho wangu Mtakatifu juu ya wote wenye mwili.

Wana wenu wa kiume na wa kike watatabiri,

wazee wenu wataota ndoto,

na vijana wenu wataona maono.

Hata juu ya watumishi wangu, wanaume kwa wanawake,

katika siku zile nitamimina Roho wangu Mtakatifu.

Nyakati za mwisho

"Katika wakati huo Mikaeli, mtawala mkuu ambaye huwalinda watu wako, atainuka. Kutakuwako wakati wa taabu ambao haujatokea tangu mwanzo wa mataifa hadi wakati huo. Lakini wakati huo, watu wako, kila mmoja ambaye jina lake litakutwa limeandikwa kwenye kitabu, ataokolewa. Wengi ambao wamelala kwenye mavumbi wataamka, baadhi yao kwa uzima wa milele, wengine kwa aibu na kudharauliwa milele. Wale wenye hekima watang’aa kama mwanga wa mbingu, nao wale ambao huwaongoza wengi kutenda haki, watang’aa kama nyota milele na milele.

Esperança e prontidão

O dia do Senhor virá como ladrão. Mas nós não somos das trevas — estejamos sóbrios, vigiliando e esperando.

Kulingana na neno la Bwana Isa mwenyewe, tunawaambia kwamba sisi ambao bado tuko hai, tuliobaki hadi kuja kwake Bwana Isa, hakika hatutawatangulia waliolala katika mauti. Kwa maana Bwana Isa mwenyewe atashuka kutoka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, na sauti ya tarumbeta ya Mungu. Nao waliokufa wakiwa katika Al-Masihi watafufuka kwanza. Baada ya hilo sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili kumlaki Bwana Isa hewani, hivyo tutakuwa pamoja na Bwana Isa milele. Kwa hiyo farijianeni kwa maneno haya.

Kwa hiyo basi, tusilale kama watu wengine wanavyolala, bali tukeshe na kuwa na kiasi. Kwa kuwa wote wanaolala, hulala usiku, na wale wanaolewa, hulewa usiku. Lakini kwa kuwa sisi ni wana wa mchana, basi tuwe na kiasi, tukijivika imani na upendo kama dirii kifuani na tumaini letu la wokovu kama chapeo. Kwa maana Mungu hakutuita ili tupate ghadhabu bali tupate wokovu kupitia kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi.

Himizo la kukesha

"Jihadharini mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na fadhaa za maisha haya, nayo siku ile ikawakuta ninyi bila kutazamia kama mtego unasavyo. Hivyo ndivyo siku hiyo itakavyowapata wanadamu wote wanaoishi katika uso wa dunia yote. Kesheni daima na mwombe ili mweze kuokoka na yale yote yatakayotokea na kusimama mbele ya Mwana wa Adamu."

Lakini wapendwa, msisahau neno hili: kwamba kwa Mwenyezi Mungu, siku moja ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku moja. Mwenyezi Mungu hakawii kuitimiza ahadi yake, kama watu wengine wanavyokudhani kukawia. Badala yake, yeye anawavumilia ninyi, maana hataki mtu yeyote aangamie, bali kila mtu afikilie toba.

Lakini siku ya Mwenyezi Mungu itakuja kama mwizi. Ndipo mbingu zitatoweka kwa kishindo kikuu; navyo vitu vya asili vitateketezwa kwa moto, nayo dunia na kila kitu kilicho ndani yake kitaunguzwa.

Kwa kuwa vitu vyote vitaharibiwa namna hii, je, ninyi imewapasa kuwa watu wa namna gani? Inawapasa kuishi maisha matakatifu na ya kumcha Mungu, mkingojea na kuhimiza kuja kwa hiyo siku ya Mungu. Siku hiyo italeta mbingu kuchomwa moto na kutoweka, na vitu vya asili vitayeyuka kwa moto. Lakini kufuatana na ahadi yake, sisi tunatazamia mbingu mpya na dunia mpya, ambayo haki hukaa ndani yake.

Sikilizeni, nawaambia siri: Sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa: ghafula, kufumba na kufumbua, parapanda ya mwisho itakapolia. Kwa kuwa parapanda italia, nao wafu watafufuliwa na miili isiyoharibika, nasi tutabadilishwa.

Mbingu mpya na dunia mpya

"Tazama, nitaumba

mbingu mpya na dunia mpya.

Mambo ya zamani hayatakumbukwa,

wala hayatakuja akilini.

Lakini furahini na kushangilia daima

katika hivi nitakavyoumba,

kwa kuwa nitaumba Yerusalemu uwe wa kupendeza,

nao watu wake wawe furaha.

Nami nitaifurahia Yerusalemu

na kuwafurahia watu wangu;

sauti ya maombolezo na ya kilio

haitasikika humo tena.

Siku ya Mwenyezi Mungu

"Hakika siku inakuja, itawaka kama tanuru. Wote wenye kiburi na watenda maovu watakuwa mabua makavu, na siku ile inayokuja itawawasha moto," asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. "Hakuna mzizi wala tawi litakalosalia kwao. Bali ninyi mnaoliheshimu Jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mabawa yake. Nanyi mtatoka nje na kurukaruka kama ndama aliyeachiwa kutoka zizini.

Mbingu mpya na nchi mpya

Kisha nikaona "mbingu mpya na nchi mpya", kwa maana mbingu ya kwanza na nchi ya kwanza vimekwisha kupita, wala hapakuwa na bahari tena. Nikauona Mji Mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, ukiwa umeandaliwa kama bibi arusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe. Nami nikasikia sauti kubwa kutoka kile kiti cha enzi ikisema, "Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Atafuta kila chozi kutoka macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita."

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-