Gratidão ao Senhor
A gratidão ao Senhor é resposta de amor diante da bondade divina. Louvar a Deus com cântico e magnificá-lo com ação de graças — isso é o que agrada ao Senhor.
Agradecer ao Senhor
Deus transformou nosso lamento em dança. Ele é digno de toda gratidão, em todo tempo e em toda circunstância.
Uligeuza maombolezo yangu kuwa kucheza,
ulinivua gunia ukanivika shangwe,
ili moyo wangu uweze kukusifu na usikae kimya.
Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, nitakushukuru milele.
Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,
nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani.
Ingieni malangoni mwake kwa shukrani
na katika nyua zake kwa kusifu,
mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.
Lakini wote wanaokutafuta
washangilie na kukufurahia,
wale wanaoupenda wokovu wako siku zote waseme,
"Mwenyezi Mungu ni mkuu!"
Gratidão constante
Em tudo dai graças. Tudo o que Deus criou é bom, quando recebido com ação de graças e paz no coração.
shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndio mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Al-Masihi Isa.
Kwa maana kila kitu alichokiumba Mungu ni chema, wala hakuna kitu chochote cha kukataliwa kama kikipokewa kwa shukrani, kwa sababu kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba.
Amani ya Al-Masihi na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani.
Lakini mimi nitakutolea dhabihu,
kwa sauti za shukrani na shangwe.
Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza.
Wokovu watoka kwa Mwenyezi Mungu."