Guardar o coração
Guardar o coração é o mandamento mais urgente de Provérbios. Sobre tudo o que se deve guardar, guarda o teu coração, porque dele procedem as fontes da vida.
Sobre tudo, guarda o coração
O coração é a nascente de tudo — pensamentos, desejos, decisões. Guardá-lo é proteger toda a vida espiritual e emocional.
Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindayo,
maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
Msemo 18
Mwanangu, nipe moyo wako,
macho yako na yafuate njia zangu,
Faida nyingine za hekima
Mwanangu, usisahau mafundisho yangu,
bali zitunze amri zangu moyoni mwako,
kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako
na kukuletea mafanikio.
Vivyo hivyo mtu mwema hutoa mambo mema kutoka hazina ya moyo wake, naye mtu mwovu hutoa mambo maovu kutoka hazina ya moyo wake. Kwa kuwa mtu hunena kwa kinywa chake yale yaliyoujaza moyo wake.
Coração puro e renovado
Cria em mim um coração puro, ó Deus. Os puros de coração verão a Deus — e o Espírito renova nosso interior.
Ee Mungu, uniumbie moyo safi,
uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.
Heri walio na moyo safi,
maana hao watamwona Mungu.
Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu,
nijaribu na ujue mawazo yangu.
Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu,
uniongoze katika njia ya milele.
Ee Mwenyezi Mungu, unijaribu, unipime,
uuchunguze moyo wangu
na mawazo yangu;
kwa maana upendo wako
uko mbele yangu daima,
nami natembea siku zote
katika kweli yako.
Ingawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku,
ingawa umenijaribu, hutaona chochote.
Nimeamua kwamba kinywa changu
hakitatenda dhambi.
Kuhusu matendo ya wanadamu:
kwa neno la midomo yako,
nimejiepusha na njia za wenye jeuri.
Hatua zangu zimeshikamana na njia zako;
nyayo zangu hazikuteleza.
Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti,
moyo wangu ni thabiti;
nitaimba na kusifu kwa nyimbo.
Guardar com a Palavra
Não vos conformeis com este mundo. A Palavra de Deus guardada no coração nos protege do pecado e nos direciona.
Msifuatishe tena mfano wa ulimwengu huu, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Ndipo mtaweza kujaribu ili kuthibitisha mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yanayopendeza na kamilifu machoni pake.
Usiache Kitabu hiki cha Torati kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi.
Ninakutafuta kwa moyo wangu wote,
usiniache niende mbali na amri zako.
Nimelificha neno lako moyoni mwangu
ili nisikutende dhambi.
Mpende Mwenyezi Mungu, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote. Amri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako.
akawaambia, "Yawekeni moyoni maneno yote ambayo nimewatangazia kwa makini siku hii ya leo, ili mpate kuwaagiza watoto wenu wayatii kwa bidii maneno yote ya sheria hii.
Vigilância e paz
A paz de Deus guarda nossos corações em Cristo Jesus. Chegai-vos a Deus, purificai os corações — e Ele estará convosco.
Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Nayo amani ya Mungu, inayopita fahamu zote, itailinda mioyo yenu na nia zenu katika Al-Masihi Isa.
Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili.
Ninyi nanyi vumilieni, tena simameni imara, kwa sababu kuja kwa Bwana Isa kumekaribia.
Kanuni za kuishi maisha matakatifu
Basi, kwa kuwa mmefufuliwa pamoja na Al-Masihi, yatafuteni yaliyo juu, Al-Masihi alikoketi mkono wa kuume wa Mungu.