Homem de Deus
O homem de Deus é aquele que busca a justiça, a piedade, a fé e o amor. A Bíblia apresenta modelos de homens íntegros que andaram com Deus e marcaram a história.
Características do homem de Deus
O homem de Deus foge das paixões e segue a justiça, a piedade, a fé, o amor, a perseverança e a mansidão.
Mambo mazuri ya imani
Lakini wewe, mtu wa Mungu, yakimbie mambo haya yote. Fuata haki, utauwa, imani, upendo, saburi na upole.
Mtu yeyote asikudharau kwa kuwa wewe ni kijana, bali uwe kielelezo kizuri kwa waumini katika usemi, mwenendo, upendo, imani na usafi.
Maneno ya mwisho
Kesheni; simameni imara katika imani; kuweni mashujaa na hodari. Fanyeni kila kitu katika upendo.
Amekuonesha yaliyo mema, ee mwanadamu.
Mwenyezi Mungu anataka nini kwako?
Ila kutenda kwa haki na kupenda rehema,
na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako.
Exemplos bíblicos
Noé era justo e íntegro entre seus contemporâneos. Jó era homem reto que temia a Deus e se desviava do mal.
Hivi ndivyo vizazi vya Nuhu.
Nuhu alikuwa mtu wa haki, na mkamilifu miongoni mwa watu wa wakati wake, tena alitembea na Mungu.
Ayubu na jamaa yake
Katika nchi ya Usi paliishi mtu ambaye aliitwa Ayubu. Mtu huyu alikuwa hana hatia, naye alikuwa mkamilifu; alimcha Mungu na kuepukana na uovu.
Alikuja mtu mmoja aliyetumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yahya. Alikuja kama shahidi apate kuishuhudia hiyo nuru, ili kupitia kwake watu wote waweze kuamini.
Mtu wa ufahamu huitazama hekima,
lakini macho ya mpumbavu huhangaika
hadi kwenye miisho ya dunia.
Viver como filho de Deus
Quem faz a vontade de Deus é eleito. Medite na Palavra e ande nos caminhos do Senhor como verdadeiro discípulo.
Bali wote waliompokea, yaani wale walioliamini jina lake, aliwapa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu. Hawa hawakuzaliwa kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali wamezaliwa kwa mapenzi ya Mungu.
Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii.
Kutii Torati ya Mwenyezi Mungu
Kijana aisafishe njia yake jinsi gani?
Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.
Ninakutafuta kwa moyo wangu wote,
usiniache niende mbali na amri zako.
Nimelificha neno lako moyoni mwangu
ili nisikutende dhambi.
Uhimidiwe, Ee Mwenyezi Mungu;
nifundishe maagizo yako.
Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote
zinazotoka katika kinywa chako.
Ninafurahia kufuata sheria zako
kama mtu afurahiaye mali nyingi.
Ninatafakari maagizo yako
na kuziangalia njia zako.
Ninafurahia maagizo yako,
wala sitalipuuza neno lako.
Furaha ya kweli
Heri mtu yule ambaye haendi
katika shauri la watu waovu,
wala hasimami katika njia ya wenye dhambi,
au kuketi katika baraza la wenye mizaha.
Bali huifurahia Torati ya Mwenyezi Mungu,
naye huitafakari hiyo Torati usiku na mchana.
Mtu huyo ni kama mti uliopandwa
kando ya vijito vya maji,
ambao huzaa matunda kwa majira yake
na majani yake hayanyauki.
Lolote afanyalo hufanikiwa.
Huzuni ya waovu
Sivyo walivyo waovu!
Wao ni kama makapi
yanayopeperushwa na upepo.
Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu,
wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.
Kwa maana Mwenyezi Mungu huziangalia njia za mwenye haki,
bali njia za waovu zitaangamia.
Mlifundishwa kuuvua mwenendo wenu wa zamani, utu wenu wa kale, ulioharibiwa na tamaa zake za udanganyifu, ili mfanywe upya katika roho ya nia zenu, na mkajivike utu mpya, ulioumbwa sawasawa na mfano wa Mungu katika haki ya kweli na utakatifu.