Publicidade

Ídolos

Por Bíblia Online

A Bíblia condena a idolatria com veemência. Um ídolo é qualquer coisa que ocupa o lugar de Deus no coração. Os cristãos são chamados a guardar-se dos ídolos e servir ao Deus vivo.

Guardai-vos dos ídolos

Filhinhos, guardai-vos dos ídolos. A cobiça é idolatria. Tudo que ocupa o trono de Deus no coração é um ídolo.

Watoto wapendwa, jilindeni nafsi zenu kutokana na sanamu. Amen.

Basi, ueni kabisa chochote kilicho ndani yenu cha asili ya kidunia: yaani uasherati, uchafu, tamaa mbaya, mawazo mabaya na ulafi, ambao ni ibada ya sanamu.

Kwa maana kupenda fedha ndiyo shina moja la maovu ya kila namna. Baadhi ya watu wakitamani fedha, wameiacha imani na kujichoma wenyewe kwa maumivu mengi.

Msijifanyizie miungu yoyote na kuilinganisha nami, msijitengenezee miungu ya fedha wala miungu ya dhahabu.

"Bali mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wenu,

niliyewaleta ninyi toka Misri.

Msimkubali Mungu mwingine ila mimi,

hakuna Mwokozi isipokuwa mimi.

O único Deus verdadeiro

O Senhor é Deus nos céus e na terra — não há outro. Escolham hoje a quem servir, mas eu e a minha casa serviremos ao Senhor.

Kubalini na mweke moyoni leo kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mungu mbinguni juu na duniani chini. Hakuna mwingine.

Ni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye.

Lakini msipoona vyema kumtumikia Mwenyezi Mungu, chagueni hivi leo mtakayemtumikia, kama ni miungu ile baba zenu waliitumikia ng’ambo ya Frati, au miungu ya Waamori, ambao mnakaa katika nchi yao. Lakini mimi na nyumba yangu, tutamtumikia Mwenyezi Mungu."

Je, hamjui kwamba wasio haki hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike: Waasherati, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wahanithi, wala walawiti, wala wezi, wala wenye tamaa mbaya, wala walevi, wala wanaodhihaki, wala wanyang’anyi hawataurithi ufalme wa Mungu.

Vencer a idolatria

Não tenhas comunhão com as obras das trevas. Revesti-vos da armadura de Deus para resistir às ciladas do diabo.

Msishiriki matendo ya giza yasiyofaa, bali yafichueni. Kwa maana ni aibu hata kutaja mambo yale ambayo wasiotii wanayafanya sirini.

Vaeni silaha zote za Mungu ili mweze kuzipinga hila za ibilisi.

Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde dhidi ya yule mwovu.

Hakuna silaha itakayofanyizwa dhidi yako

itakayofanikiwa,

nawe utauthibitisha kuwa mwongo

kila ulimi utakaokushtaki.

Huu ndio urithi wa watumishi wa Mwenyezi Mungu

na hii ndiyo haki yao inayotoka kwangu,"

asema Mwenyezi Mungu.

Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Aache uovu, atende mema,

aitafute amani na kuifuatilia.

Uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu ya dhambi ni sheria.

Seja o primeiro
Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-28_14-13-17-