Pular para o conteúdo
Publicidade

Incentivo

Por Bíblia Online

A Bíblia é fonte inesgotável de incentivo. Em cada página, Deus nos encoraja a não temer, a perseverar e a confiar que Ele está conosco e é maior que qualquer adversidade.

Deus é por nós

Se Deus é por nós, quem será contra nós? O Senhor fortalece, sustenta e guia seus filhos em cada batalha e desafio.

Upendo wa Mwenyezi Mungu

Tuseme nini basi kuhusu haya? Ikiwa Mungu yuko upande wetu, ni nani awezaye kuwa kinyume chetu?

Hivyo usiogope, kwa maana niko pamoja nawe;

usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako.

Nitakutia nguvu na kukusaidia;

nitakutegemeza kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

bali wale wamtumainio Mwenyezi Mungu

atafanya upya nguvu zao.

Watapaa juu kwa mabawa kama tai;

watapiga mbio wala hawatachoka,

watatembea kwa miguu wala hawatazimia.

Naweza kuyafanya mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.

Kuweni imara na moyo wa ushujaa. Msiogope wala msifadhaike kwa sababu yao, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anaenda pamoja nanyi; kamwe hatawaacha wala hatawatupa ninyi."

Maana Mungu hakutupatia roho ya woga, bali roho ya nguvu, ya upendo na ya moyo wa kiasi.

Esperança e perseverança

A tribulação produz perseverança, a perseverança produz caráter, e o caráter produz esperança que não decepciona.

Si hivyo tu, bali twafurahi pia katika mateso, kwa sababu tunajua kuwa mateso huleta saburi, nayo saburi huleta uthabiti wa moyo, na uthabiti wa moyo huleta tumaini, wala tumaini halitukatishi tamaa, kwa sababu Mungu amekwisha kumimina pendo lake mioyoni mwetu kupitia kwa Roho wa Mungu ambaye ametupatia.

Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kubwa mno.

Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuambia ibilisi atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji la uzima.

"Nimewaambia mambo haya ili mpate kuwa na amani mkiwa ndani yangu. Ulimwenguni mtapata dhiki. Lakini jipeni moyo, kwa maana mimi nimeushinda ulimwengu."

Kwa hiyo, hatukati tamaa. Ingawa utu wetu wa nje unachakaa, utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku. Kwa maana dhiki yetu nyepesi iliyo ya kitambo inatutayarisha kwa ajili ya utukufu wa milele unaozidi kuwa mwingi kupita kiasi. Kwa hivyo hatuangalii yale yanayoonekana, bali yale yasiyoonekana. Kwa maana yale yanayoonekana ni ya kitambo tu, bali yale yasiyoonekana ni ya milele.

Isa akamwambia, "Ati, Kama unaweza kufanya jambo lolote? Yote yawezekana kwake yeye aaminiye."

Deus cuida de nós

Entrega o teu caminho ao Senhor. Lança sobre Ele as tuas ansiedades, porque Ele tem cuidado de nós diariamente.

Mkabidhi Mwenyezi Mungu njia yako,

mtumaini yeye, naye atatenda hili:

Kama Mwenyezi Mungu akipendezwa na njia ya mtu,

yeye huimarisha hatua zake,

ajapojikwaa, hataanguka,

kwa maana Mwenyezi Mungu

humtegemeza kwa mkono wake.

Mtwike Mwenyezi Mungu fadhaa zako,

naye atakutegemeza,

hatamwacha kamwe mwenye haki wake aanguke.

Kuomba msaada dhidi ya wadanganyifu

Katika dhiki yangu namwita Mwenyezi Mungu,

naye hunijibu.

Sitaogopa makumi elfu ya adui,

wanaojipanga dhidi yangu kila upande.

Futuro e promessas

Eu sei os planos que tenho para vocês — planos de paz e não de mal, para dar-lhes futuro e esperança.

Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu," asema Mwenyezi Mungu, "ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.

Mwenyezi Mungu, Mungu wako, yu pamoja nawe,

yeye ni Shujaa mwenye nguvu anayeokoa.

Atakufurahia kwa furaha kubwa,

atakutuliza kwa pendo lake,

atakufurahia kwa kuimba."

Lakini Isa akawatazama, akawaambia, "Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini mambo yote yanawezekana kwa Mungu."

Lakini ni kama ilivyoandikwa:

"Hakuna jicho limepata kuona,

wala sikio limepata kusikia,

wala hayakuingia moyoni mwa mwanadamu yeyote,

mambo ambayo Mungu amewaandalia

wale wanaompenda":

Lakini Shama akasimama imara katikati ya lile shamba. Akalipigania na kuwaua Wafilisti, naye Mwenyezi Mungu akawapa ushindi mkubwa.

Seja o primeiro