Intimidade com Deus
A intimidade com Deus é o maior privilégio do cristão. Ele nos convida a nos aproximar, a conhecê-lo profundamente e a desfrutar de comunhão diária com o Criador do universo.
Aproximar-se de Deus
Chegai-vos a Deus e Ele se chegará a vós. Deus deseja intimidade, não religiosidade. Ele busca os que o buscam de todo coração.
Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili.
"Haya! Njooni, ninyi nyote wenye kiu,
njooni kwenye maji;
nanyi ambao hamna fedha,
njooni, nunueni na mle!
Njooni, nunueni divai na maziwa
bila fedha na bila gharama.
Kwa nini kutumia fedha kwa kitu ambacho si chakula,
na kutaabikia kitu kisichoshibisha?
Sikilizeni, nisikilizeni mimi na mle kilicho kizuri,
nazo nafsi zenu zitafurahia utajiri wa unono.
Tegeni sikio mje kwangu,
nisikieni mimi, ili nafsi zenu zipate kuishi.
Nitafanya agano la milele nanyi,
pendo la uaminifu nililomwahidi Daudi.
Tazama, nimemfanya kuwa shahidi wa mataifa,
kiongozi na jemadari wa mataifa.
Hakika utaita mataifa usiyoyajua,
nayo mataifa yale yasiyokujua yataharakisha kukujia,
kwa sababu ya Mwenyezi Mungu, Mungu wako,
yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli,
kwa maana amekutukuza."
Mtafuteni Mwenyezi Mungu maadamu anapatikana;
mwiteni maadamu yu karibu.
Kabla hawajaita, nitajibu,
nao wakiwa katika kunena, nitasikia.
‘Niite, nami nitakuitikia, nitakuonesha mambo makubwa, yasiyochunguzika na usiyoyajua.’
Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu," asema Mwenyezi Mungu, "ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.
Sede de Deus
Como a corça deseja as correntes de água, assim a minha alma suspira por ti, ó Deus. A intimidade nasce do desejo profundo.
Kama ayala anavyoonea shauku vijito vya maji,
ndivyo nafsi yangu inavyokuonea shauku, Ee Mungu.
Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai.
Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu?
Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu,
nakutafuta kwa moyo wote;
nafsi yangu inakuonea kiu,
mwili wangu unakuonea wewe shauku,
katika nchi kame na iliyochoka,
mahali pasipo maji.
Nimekuona katika mahali patakatifu
na kuuona uwezo wako na utukufu wako.
Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai,
midomo yangu itakuadhimisha.
Nitakusifu siku zote za maisha yangu,
na kwa jina lako nitainua mikono yangu.
Nafsi yangu itatoshelezwa,
kama kushiba vyakula vizuri;
kwa midomo iimbayo
kinywa changu kitakusifu wewe.
Kitandani mwangu ninakukumbuka wewe;
ninakuwaza makesha yote ya usiku.
Kwa sababu wewe ndiwe msaada wangu,
chini ya uvuli wa mabawa yako naimba.
Nafsi yangu inaambatana nawe,
mkono wako wa kuume hunishika.
Wale wanaotafuta uhai wangu wataangamizwa;
wataenda chini kwenye vilindi vya dunia.
Watatolewa wafe kwa upanga,
nao watakuwa chakula cha mbweha.
Bali mfalme atafurahi katika Mungu,
wale wote waapao kwa jina la Mungu watamsifu,
bali vinywa vya waongo vitanyamazishwa.
Unidade com o Pai
Jesus orou pela unidade dos seus com o Pai. A intimidade com Deus inclui confissão, perdão e alegria na comunhão.
Utukufu ule ulionipa nimewapa wao, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja. Mimi ndani yao na wewe ndani yangu: ili wawe wamekamilika katika umoja, na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma, nami nimewapenda wao kama unavyonipenda mimi.
Mwenyezi Mungu, Mungu wako, yu pamoja nawe,
yeye ni Shujaa mwenye nguvu anayeokoa.
Atakufurahia kwa furaha kubwa,
atakutuliza kwa pendo lake,
atakufurahia kwa kuimba."
Tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na wa haki, atatusamehe dhambi zetu na kutusafisha kutokana na udhalimu wote.