Intimidade com Deus
A intimidade com Deus é o maior privilégio do cristão. Ele nos convida a nos aproximar, a conhecê-lo profundamente e a desfrutar de comunhão diária com o Criador do universo.
Aproximar-se de Deus
Chegai-vos a Deus e Ele se chegará a vós. Deus deseja intimidade, não religiosidade. Ele busca os que o buscam de todo coração.
Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
Haya, kila aonaye kiu, njoni majini,
Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle;
Naam, njoni, nunueni divai na maziwa,
Bila fedha na bila gharama.
Kwa nini mtoe fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula?
Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha?
Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema,
Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.
Tegeni masikio yenu, na kunijia;
Sikieni, na nafsi zenu zitaishi;
Nami nitafanya nanyi agano la milele,
Naam, rehema za Daudi zilizo imara.
Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa makabila ya watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa makabila ya watu. Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya BWANA, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza.
Mtafuteni BWANA, maadamu anapatikana,
Mwiteni, maadamu yuko karibu;
Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa bado wanena, nitasikia.
Niite, nami nitakuitikia, nami nitakuonesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua.
Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye.
Sede de Deus
Como a corça deseja as correntes de água, assim a minha alma suspira por ti, ó Deus. A intimidade nasce do desejo profundo.
Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji.
Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.
Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai,
Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?
Ee MUNGU, Mungu wangu, nitakutafuta mapema,
Nafsi yangu inakuonea kiu,
Mwili wangu wakuonea shauku,
Katika nchi kame na uchovu, isiyo na maji.
Ndivyo nilivyokutazama katika patakatifu,
Nizione nguvu zako na utukufu wako.
Maana fadhili zako ni njema kuliko uhai;
Midomo yangu itakusifu.
Ndivyo nitakavyokubariki maadamu ni hai;
Kwa jina lako nitaiinua mikono yangu.
Nafsi yangu itakinai kama kushiba mafuta na vinono;
Kinywa changu kitakusifu kwa midomo ya furaha.
Ninapokukumbuka kitandani mwangu,
Ninakutafakari usiku kucha.
Maana Wewe umekuwa msaada wangu,
Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia.
Nafsi yangu inaambatana nawe sana;
Mkono wako wa kulia unanitegemeza.
Bali waitafutao nafsi yangu, ili kuiangamiza,
Wataingia katika vilindi vya nchi.
Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga,
Watakuwa riziki za mbwamwitu.
Bali mfalme atamfurahia Mungu,
Kila aapaye kwa Yeye atashangilia,
Kwa maana vinywa vya waongo vitafumbwa.
Unidade com o Pai
Jesus orou pela unidade dos seus com o Pai. A intimidade com Deus inclui confissão, perdão e alegria na comunhão.
Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.
BWANA, Mungu wako, yuko katikati yako shujaa awezaye kuokoa;
Atakushangilia kwa furaha kuu,
Atakutuliza katika upendo wake,
Atakufurahia kwa kuimba.
Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote.