Pular para o conteúdo
Publicidade

Jesus me ama

Por Bíblia Online

Jesus me ama — essa certeza transforma vidas. O amor de Cristo não depende do nosso merecimento, mas da sua natureza. Ele nos amou primeiro, e nada pode nos separar desse amor.

Ele me amou primeiro

Nós amamos porque Ele nos amou primeiro. O amor de Deus se manifestou em nos enviar seu Filho como propiciação pelos nossos pecados.

Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza.

Hili ndilo pendo: si kwamba tulimpenda Mungu, bali yeye alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili yeye awe dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu.

Tazameni ni pendo kuu namna gani alilotupatia Baba, kwamba sisi tuitwe wana wa Mungu! Na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.

Kwa namna hii twaweza kulijua pendo la Mungu: Kwa sababu Isa Al-Masihi aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Nasi imetupasa kuutoa uhai kwa ajili ya hao ndugu.

"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Al-Masihi alikufa kwa ajili yetu.

Amor inseparável

Nem a morte, nem a vida, nem qualquer outra criatura poderá nos separar do amor de Deus em Cristo Jesus nosso Senhor.

Kwa maana nimekwisha kujua kwa hakika ya kuwa sio mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuja, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chochote zitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Al-Masihi Isa, Bwana wetu.

Ni nani atakayetutenga na upendo wa Al-Masihi? Je, ni shida au taabu au mateso au njaa au uchi au hatari au upanga? Kama ilivyoandikwa:

"Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa;

tumehesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa."

Lakini katika mambo haya yote tu zaidi ya washindi kwa yeye aliyetupenda.

na kutoka kwa Isa Al-Masihi, aliye shahidi mwaminifu, mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, mtawala wa wafalme wa dunia.

Kwake yeye anayetupenda na aliyetuweka huru kutoka dhambi zetu kwa damu yake, na akatufanya sisi kuwa ufalme na makuhani, ili tumtumikie Mungu wake ambaye ni Baba yake. Utukufu na uwezo ni vyake milele na milele! Amen.

Kuenenda katika nuru

Kwa hiyo, mfuateni Mungu kama watoto wanaopendwa, mkiishi maisha ya upendo, kama vile Al-Masihi alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu.

Celebrar o amor de Jesus

O amor de Jesus é motivo de cântico e louvor. De manhã cantarei teu amor e à noite proclamarei tua misericórdia.

Ee uliye Nguvu zangu, ninakuimbia sifa.

Wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu,

Mungu unayenipenda.

Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma na mwenye neema;

si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.

Yeye hatalaumu siku zote,

wala haweki hasira yake milele,

yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu

wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu.

Kama vile mbingu zilivyo juu ya dunia,

ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha;

kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,

ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi.

Hakuna mtu mwenye upendo mkuu kuliko huu, mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.

Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Isa Al-Masihi, kwamba ingawa alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikubali kuwa maskini, ili kwa umaskini wake ninyi mpate kuwa matajiri.

Seja o primeiro