Publicidade

Jesus Cristo

Por Bíblia Online

Jesus Cristo é o centro de toda a Escritura — Deus encarnado, Salvador do mundo, Senhor dos senhores. Nele habita corporalmente toda a plenitude da divindade.

A divindade de Cristo

No princípio era o Verbo, e o Verbo estava com Deus, e o Verbo era Deus. Jesus é Deus revelado em carne humana.

Neno alifanyika mwili

Hapo mwanzo alikuwako Neno, naye huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.

Neno alifanyika mwili

Hapo mwanzo alikuwako Neno, naye huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu.

Vitu vyote viliumbwa kupitia kwake, na hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa pasipo yeye.

Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.

Maana utimilifu wote wa Mungu unakaa ndani ya Al-Masihi katika umbile la mwili wa kibinadamu,

Maana utimilifu wote wa Mungu unakaa ndani ya Al-Masihi katika umbile la mwili wa kibinadamu, nanyi mmepewa ukamilifu ndani ya Al-Masihi, aliye mkuu juu ya kila nguvu na kila mamlaka.

Kuweni na nia ile ile aliyokuwa nayo Al-Masihi Isa:

Yeye, ingawa alikuwa na asili ya Mungu hasa,

hakuona kule kuwa sawa na Mungu

kuwa kitu cha kushikilia,

bali alijifanya si kitu,

akachukua hali hasa ya mtumwa,

naye akazaliwa katika umbo la mwanadamu.

Kuweni na nia ile ile aliyokuwa nayo Al-Masihi Isa:

Jesus, o Filho de Deus

Tu és o Cristo, o Filho do Deus vivo! Jesus revelou o Pai e demonstrou sua autoridade divina por palavras e obras.

Akawauliza, "Je, ninyi mnasema mimi ni nani?"

Simoni Petro akamjibu, "Wewe ndiwe Al-Masihi, Mwana wa Mungu aliye hai."

Naye Isa akamwambia, "Heri wewe, Simoni Bar-Yona, kwa maana hili halikufunuliwa kwako na mwanadamu, bali na Baba yangu aliye mbinguni.

"Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita jina Imanueli" (maana yake, "Mungu pamoja nasi").

Basi yule jemadari na wale waliokuwa pamoja naye wakimlinda Isa walipoona lile tetemeko na yale yote yaliyokuwa yametukia, waliogopa sana, wakapaza sauti na kusema, "Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu!"

Lakini Isa akakaa kimya, hakusema neno lolote.

Kuhani mkuu akamuuliza tena, "Je, wewe ndiwe Al-Masihi, Mwana wa Mungu Aliyebarikiwa?"

Isa akajibu, "Mimi ndimi. Nanyi mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni."

Yule malaika akawaambia, "Msistaajabu. Mnamtafuta Isa, Mnasiri, aliyesulubiwa. Amefufuka! Hayuko hapa. Tazameni mahali walipomlaza.

Isa abatizwa

Baada ya watu wote kubatizwa, Isa naye akabatizwa. Naye alipokuwa akiomba, mbingu zilifunguka. Roho Mtakatifu wa Mungu akashuka juu yake kwa umbo kama la hua, nayo sauti kutoka mbinguni ikasema: "Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana."

Eu Sou

Jesus disse: antes que Abraão existisse, Eu Sou. Ele se identificou com o nome divino revelado a Moisés na sarça ardente.

Isa akawaambia, "Amin, amin nawaambia, kabla Ibrahimu hajakuwa, Mimi niko."

Musa akamwambia Mungu, "Ikiwa nitawaendea Waisraeli na kuwaambia, Mungu wa baba zenu amenituma kwenu,nao wakiniuliza, Jina lake ni nani?Nitawaambia nini?"

Mungu akamwambia Musa, "Mimi niko ambaye niko; au, Mimi Ndiye. Hivyo ndivyo utakavyowaambia Waisraeli: Mimi niko amenituma kwenu.’ "

Mimi na Baba yangu tu umoja."

Isa akawajibu, "Baba yangu anafanya kazi yake daima hata siku hii ya leo, nami pia ninafanya kazi." Maneno haya yaliwaudhi sana viongozi wa Wayahudi. Wakajaribu kila njia wapate jinsi ya kumuua, kwani si kwamba alivunja Sabato tu, bali alikuwa akimwita Mungu Baba yake, hivyo kujifanya sawa na Mungu.

Maneno haya yaliwaudhi sana viongozi wa Wayahudi. Wakajaribu kila njia wapate jinsi ya kumuua, kwani si kwamba alivunja Sabato tu, bali alikuwa akimwita Mungu Baba yake, hivyo kujifanya sawa na Mungu.

Hakika kama vile Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, vivyo hivyo Mwana huwapa uzima wale anaopenda. Wala Baba hamhukumu mtu yeyote, lakini hukumu yote amempa Mwana, ili wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Yeyote asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyemtuma.

Amin, amin nawaambia, saa yaja, nayo saa ipo, wafu watakapoisikia sauti ya Mwana wa Mungu), wa kiroho, bali si wa kimwili., nao watakaoisikia watakuwa hai.

O Salvador e Senhor

Jesus é o caminho, a verdade e a vida. Não há outro nome dado entre os homens pelo qual devamos ser salvos.

Isa akawaambia, "Mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu hawezi kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu.

Isa akamjibu, "Filipo, nimekaa nanyi muda huu wote hata usinijue? Mtu yeyote aliyeniona mimi amemwona Baba. Sasa wawezaje kusema, Tuoneshe Baba? Je, huamini ya kuwa mimi niko ndani ya Baba, naye Baba yuko ndani yangu? Maneno ninayowaambia siyasemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba akaaye ndani yangu ndiye atendaye hizi kazi.

Isa akamwambia, "Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi;

Isa akamwambia, "Sikukuambia kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?"

Wala hakuna wokovu katika mwingine yeyote, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu linalopasa kutuokoa."

Walipokuwa wakiendelea na safari wakafika mahali palipokuwa na maji, yule towashi akamuuliza Filipo, "Tazama, hapa kuna maji. Kitu gani kitanizuia nisibatizwe?"

[ Filipo akamwambia, "Ukiamini kwa moyo wako wote, unaweza kubatizwa."

Akajibu, "Naamini kuwa Isa Al-Masihi ni Mwana wa Mungu."] Naye akaamuru lile gari lisimamishwe. Filipo na yule towashi wakateremka kwenye maji pamoja, naye Filipo akambatiza.

A supremacia de Cristo

Ele é o resplendor da glória de Deus e a expressão exata do seu ser. Toda a plenitude habita nele e por Ele tudo subsiste.

Mwana ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno lake lenye uweza. Baada ya kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Aliye Mkuu huko mbinguni. Kwa hiyo alifanyika bora kuliko malaika, kama jina alilorithi lilivyo bora kuliko lao.

Isa Al-Masihi ni Kuhani Mkuu kuliko wote

Kwa kuwa tunaye Kuhani Mkuu kuliko wote ambaye ameingia mbinguni, Isa Mwana wa Mungu), wa kiroho, bali si wa kimwili., basi na tushikamane sana kwa uthabiti na ule ukiri wa imani yetu. Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuliana na sisi katika udhaifu wetu, lakini tunaye mmoja ambaye alijaribiwa kwa kila namna, kama vile sisi tujaribiwavyo: lakini yeye hakutenda dhambi.

Basi na tumtazame sana Isa mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu, yeye ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahimili msalaba, bila kujali aibu ya huo msalaba, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

Kwa sababu hii ilibidi afanane na ndugu zake kwa kila hali, ili apate kuwa Kuhani Mkuu mwenye huruma na mwaminifu katika kumtumikia Mungu, ili pia apate kufanya upatanisho kwa ajili ya dhambi za watu.

Hakika alichukua udhaifu wetu

na akajitwika huzuni zetu;

tulidhania kuwa ameadhibiwa na Mungu,

naye akapigwa sana na kujeruhiwa.

Lakini alijeruhiwa kwa ajili ya makosa yetu,

alichubuliwa kwa ajili ya maovu yetu;

adhabu iliyotuletea sisi amani ilikuwa juu yake,

na kwa majeraha yake sisi tumepona.

Kwa maana, kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,

tumepewa mtoto wa kiume,

nao utawala utakuwa begani mwake.

Naye ataitwa

Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu,

Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.

Confessar a Cristo

Todo aquele que confessa que Jesus é o Filho de Deus, Deus permanece nele e ele em Deus. A fé em Cristo é a vitória.

Kila akiriye kwamba Isa ni Mwana wa Mungu, basi Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu.

Kila akiriye kwamba Isa ni Mwana wa Mungu, basi Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu.

Hivi ndivyo Mungu alivyoonesha pendo lake kwetu: Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kupitia kwake. Hili ndilo pendo: si kwamba tulimpenda Mungu, bali yeye alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili yeye awe dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu.

Hivi ndivyo Mungu alivyoonesha pendo lake kwetu: Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kupitia kwake.

Yeye atendaye dhambi ni wa ibilisi, kwa sababu ibilisi amekuwa akitenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu), wa kiroho, bali si wa kimwili. alidhihirishwa, ili aziangamize kazi za ibilisi.

Ni nani yule aushindaye ulimwengu? Ni yule tu aaminiye kwamba Isa ni Mwana wa Mungu), wa kiroho, bali si wa kimwili..

Huu ndio ushuhuda: kwamba Mungu ametupatia uzima wa milele, nao huo uzima umo katika Mwanawe. Aliye naye Mwana wa Mungu anao uzima, yeye asiye na Mwana wa Mungu hana uzima.

Kwa sababu, ukikiri kwa kinywa chako kwamba "Isa ni Bwana," na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka.

Viver em Cristo

Já não sou eu quem vive, mas Cristo vive em mim. Ele supre toda necessidade, dá paz e reina como Senhor.

Nimesulubiwa pamoja na Al-Masihi, wala si mimi tena ninayeishi, bali Al-Masihi ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani katika Mwana wa Mungu), wa kiroho, bali si wa kimwili., aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu.

Naye Mungu wangu atawajaza ninyi na kila mnachohitaji kwa kadiri ya utajiri wake katika utukufu ndani ya Al-Masihi Isa.

Amani ya Al-Masihi na itawale mioyoni mwenu, kwa kuwa ninyi kama viungo vya mwili mmoja mmeitiwa amani. Tena kuweni watu wa shukrani.

Kwa maana sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tulioumbwa katika Al-Masihi Isa, ili tupate kutenda matendo mema, ambayo Mungu alitangulia kuyaandaa tupate kuishi katika hayo.

mkiishi maisha ya upendo, kama vile Al-Masihi alivyotupenda sisi akajitoa kwa ajili yetu kuwa sadaka yenye harufu nzuri na dhabihu kwa Mungu.

Kama vile katika mwili mmoja tulivyo na viungo vingi, navyo viungo vyote havina kazi moja, vivyo hivyo na sisi tulio wengi, tu mwili mmoja katika Al-Masihi, nasi kila mmoja ni kiungo cha mwenzake.

Lakini Mungu apewe shukrani, yeye atupaye ushindi kupitia kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi.

Bali mtukuzeni Al-Masihi kama Bwana mioyoni mwenu. Siku zote mwe tayari kumjibu mtu yeyote atakayewauliza kuhusu sababu ya tumaini lililo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa heshima,

Kwa maana kuna Mungu mmoja na mpatanishi mmoja kati ya Mungu na wanadamu, yaani mwanadamu Al-Masihi Isa,

O Rei eterno

O Rei dos reis voltará em glória e majestade. Todo joelho se dobrará e toda língua confessará que Jesus Cristo é o Senhor.

Aliyepanda farasi mweupe

Kisha nikaona mbingu imefunguka na hapo mbele yangu akiwepo farasi mweupe, ambaye yeye aliyempanda aliitwa Mwaminifu na Kweli. Yeye huhukumu kwa haki na kufanya vita. Macho yake ni kama miali ya moto na juu ya kichwa chake kuna taji nyingi. Ana jina lililoandikwa ambalo hakuna mtu yeyote anayelijua isipokuwa yeye mwenyewe. Amevaa joho lililoloweshwa katika damu, na Jina lake ni Neno la Mungu. Majeshi ya mbinguni walikuwa wakimfuata, wakiwa wamepanda farasi weupe, hali wamevaa mavazi ya kitani safi, nyeupe na nzuri. Kinywani mwake hutoka upanga mkali ambao kwa huo atayaangusha mataifa. "Atayatawala kwa fimbo yake ya utawala ya chuma." Hulikanyaga shinikizo la ghadhabu ya Mungu Mwenyezi. Kwenye joho lake na paja lake pameandikwa jina hili:

Mfalme wa wafalme

na Bwana wa mabwana.

Neema ya Bwana Isa iwe na watakatifu wote. Amen.

Kisha akamwambia Tomaso, "Weka kidole chako hapa na uone mikono yangu, nyoosha mkono wako uguse ubavuni mwangu. Usiwe na shaka, bali uamini tu."

Tomaso akamwambia, "Bwana wangu na Mungu wangu!"

Kusudi la kitabu hiki

Isa alifanya miujiza mingine mingi mbele za wanafunzi wake, ambayo haikuandikwa katika kitabu hiki. Lakini hii imeandikwa ili mweze kuamini ya kuwa Isa ndiye Al-Masihi, Mwana wa Mungu, na kwa kumwamini mpate uzima katika jina lake.

Amri yangu ndiyo hii: Mpendane kama mimi nilivyowapenda ninyi.

Amin, amin nawaambia, yeyote anayempokea yule niliyemtuma anipokea mimi, naye anipokeaye mimi ampokea yeye aliyenituma mimi."

Nami ninawapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe, wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka mikono yangu. Baba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote, na hakuna awezaye kuwapokonya kutoka mikononi mwake. Mimi na Baba yangu tu umoja."

"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. Kwa maana Mungu hakumtuma Mwanawe kuuhukumu ulimwengu, bali kupitia kwake ulimwengu upate kuokolewa. Yeyote amwaminiye hahukumiwi, lakini asiyeamini amekwisha kuhukumiwa, kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.

Tena yeyote asiyeuchukua msalaba wake na kunifuata, hastahili kuwa wangu.

Kwa kuwa wanapokusanyika pamoja watu wawili au watatu kwa Jina langu, mimi niko papo hapo pamoja nao."

Isa akawatazama, akawaambia, "Kwa mwanadamu jambo hili haliwezekani, lakini kwa Mungu sivyo. Mambo yote yanawezekana kwa Mungu."

Isa akajibu, "Yasiyowezekana kwa wanadamu yanawezekana kwa Mungu."

Neema ya Bwana Isa Al-Masihi iwe pamoja na roho zenu. Amen.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-