Jovens
Deus tem planos maravilhosos para os jovens. A Bíblia os convida a consagrar a juventude ao Senhor, crescer em sabedoria e ser exemplo para todos em fé, palavra, conduta e amor.
Ninguém despreze a tua mocidade
Paulo exortou Timóteo: sê exemplo dos fiéis na palavra, no procedimento, no amor, no espírito, na fé e na pureza.
Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.
Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi;
Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri na kuishi siku nyingi katika dunia.
Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,
Lembrar do Criador na juventude
Lembra-te do teu Criador nos dias da tua mocidade. A sabedoria ganha cedo produz frutos duradouros na vida inteira.
Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako,
Kabla hazijaja siku zilizo mbaya,
Wala haijakaribia miaka utakaposema,
Mimi sina furaha katika hiyo.
Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako,
Kabla hazijaja siku zilizo mbaya,
Wala haijakaribia miaka utakaposema,
Mimi sina furaha katika hiyo.
Kabla jua, na nuru, na mwezi,
Na nyota, havijatiwa giza;
Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;
Siku ile walinzi wa nyumba watakapotetemeka;
Hapo wenye nguvu watakapojiinamisha;
Na wasagao kukoma kwa kuwa ni haba;
Na hao wachunguliao madirishani kutiwa giza;
Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na kinachotamaniwa na macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni.
Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini mwako; kwa maana ujana ni ubatili, na utu uzima pia.
Heri kijana maskini mwenye hekima
Kuliko mfalme mzee mpumbavu
ambaye hajui tena kupokea maonyo.
Força e promessa
Os jovens renovam suas forças quando esperam no Senhor. Deus levanta jovens com visões e sonhos para transformar o mundo.
Hata vijana watazimia na kuchoka, na vijana wanaume wataanguka; bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, wa kiume na wa kike, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.
Basi, kwa habari za hao vijana wanne, Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Danieli naye alikuwa na ufahamu katika maono yote, na ndoto. Hata mwisho wa siku zile alizoziagiza mfalme za kuwaingiza, mkuu wa matowashi akawaingiza mbele ya mfalme Nebukadneza. Naye mfalme akazungumza nao; na miongoni mwao wote hawakuonekana waliokuwa kama Danieli, na Hanania, na Mishaeli, na Azaria; kwa hiyo wakasimama mbele ya mfalme.
Fahari ya vijana ni nguvu zao,
Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.
Hata mtoto hujijulisha kwa matendo yake;
Kwamba kazi yake ni safi, kwamba ni adili.
Guardar o caminho
Como purificará o jovem seu caminho? Guardando-o segundo a tua Palavra. A Escritura na juventude guarda do pecado a vida inteira.
Jinsi gani kijana aisafishe njia yake?
Kwa kutii, akilifuata neno lako.
Moyoni mwangu nimeliweka neno lako,
Nisije nikakutenda dhambi.
Maana ndiwe tegemeo langu, Ee Bwana MUNGU,
Tumaini langu tokea ujana wangu.
Vijana wa kiume, na wanawali,
Wazee, na watoto;
Na walisifu jina la BWANA,
Maana jina lake peke yake limetukuka;
Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.
Mithali za Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli.
Kujua hekima na adabu; kutambua maneno ya ufahamu; kufundishwa matendo ya busara, katika haki na hukumu na adili. Kuwapa wajinga werevu, na kijana maarifa na tahadhari;
Sikia, mwanangu, uwe na hekima,
Na kuuongoza moyo wako katika njia njema.
Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo;
Miongoni mwao walao nyama kwa pupa.
Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini,
Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.
Msikilize baba yako aliyekuzaa,
Wala usimdharau mama yako akiwa mzee.
Coragem e vocação
Deus chamou jovens como Jeremias e Josué para grandes missões. A juventude não é desculpa — é oportunidade de servir poderosamente.
Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto. Lakini BWANA akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru. Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema BWANA.
Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za baadaye. Nanyi mtaniita, mtakwenda na kuniomba, nami nitawasikiliza. Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote. Nami nitaonekana kwenu, asema BWANA, nami nitawarudisha watu wenu waliofungwa, nami nitawakusanya ninyi, nikiwatoa katika mataifa yote, na katika mahali pote, nilikowafukuza, asema BWANA; nami nitawaleta tena, hadi mahali ambapo kutoka hapo niliwafanya mchukuliwe mateka.
Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda kulingana na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kulia, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako. Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda kulingana na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. Je! Si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na moyo wa ushujaa; usiogope wala usifadhaike; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yu pamoja nawe kila uendako.
Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.
Basi nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake;
Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mmemjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mna nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, nanyi mmemshinda yule mwovu.
Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.
Ni vema mwanadamu aichukue nira
Wakati wa ujana wake.