Publicidade

Salmos 148

Sifa kwa utukufu mkuu wa Mungu

1 Haleluya.

Msifuni BWANA kutoka mbinguni;

Msifuni katika mahali palipo juu.

2 Dan 7:10;Ebr 1:7 Msifuni, enyi malaika wake wote;

Msifuni, majeshi yake yote.

3 Msifuni, jua na mwezi;

Msifuni, nyota zote zenye mwanga.

4 1 Fal 8:27 Msifuni, enyi mbingu za mbingu,

Nanyi maji mlioko juu ya mbingu.

5 Ebr 11:3 Na vilisifu jina la BWANA,

Kwa maana aliamuru, vikaumbwa.

6 Yer 33:25 Amevithibitisha hata milele na milele,

Ametoa amri wala haitapita.

7 Isa 43:20 Msifuni BWANA kutoka nchi,

Enyi nyangumi na vilindi vyote.

8 Moto na mvua ya mawe, theluji na mvuke,

Upepo wa dhoruba utimizao neno lake.

9 Isa 49:13 Milima na vilima vyote,

Miti yenye matunda na mierezi yote.

10 Hayawani, na wanyama wafugwao,

Vitambaavyo, na ndege wenye mbawa.

11 Mdo 17:28 Wafalme wa dunia, na watu wote,

Wakuu, na watawala wote wa dunia.

12 Vijana wa kiume, na wanawali,

Wazee, na watoto;

13 Isa 6:3;Flp 2:9 Na walisifu jina la BWANA,

Maana jina lake peke yake limetukuka;

Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.

14 Efe 2:17;1 Pet 2:9 Naye amewainulia watu wake pembe,

Sifa za watauwa wake wote;

Wana wa Israeli, watu walio karibu naye.

Haleluya.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-