Pular para o conteúdo
Publicidade

Língua

Por Bíblia Online

A língua tem poder de vida e de morte. A Bíblia compara a língua ao leme de um navio e à faísca que incendeia uma floresta. Dominar a língua é prova de maturidade espiritual.

O poder da língua

A morte e a vida estão no poder da língua. Quem a domina é varão perfeito, capaz de controlar todo o corpo.

Mauti na uzima viko katika uwezo wa ulimi,

nao wanaoupenda watakula matunda yake.

Sisi sote tunajikwaa katika mambo mengi. Ikiwa mtu yeyote hakosei kamwe katika yale anayosema, yeye ni mkamilifu, naye anaweza kuuzuia pia na mwili wake wote.

Tunapotia lijamu kwenye vinywa vya farasi ili kuwafanya watutii, tunaweza kuigeuza miili yao yote. Au chukua mfano wa meli: ingawa ni kubwa sana, nazo hupelekwa na upepo mkali, zinaelekezwa kwa usukani mdogo sana kokote wanakotaka nahodha. Vivyo hivyo ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili, lakini hujivuna majivuno makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa! Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu kati ya viungo vya mwili. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa Jehanamu.

Kwa maana kila aina ya wanyama, ndege, wanyama watambaao na viumbe vya baharini hufugika na hufugwa na binadamu, lakini hakuna mtu awezaye kuufuga ulimi. Ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.

Kwa ulimi tunamhimidi Mwenyezi Mungu na Baba yetu, na kwa huo twawalaani watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haistahili kuwa hivyo. Je, chemchemi moja inaweza kutoa katika tundu moja maji matamu na maji ya chumvi? Je, ndugu zangu, mtini unaweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Wala chemchemi ya maji ya chumvi haiwezi kutoa maji matamu.

Palavras sábias

A língua branda quebra até ossos. A palavra certa no tempo certo é como maçãs de ouro em salvas de prata.

Kwa uvumilivu mtawala aweza kushawishiwa,

nao ulimi laini unaweza kuvunja mfupa.

Maneno ya kipumbavu huchoma kama upanga,

bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.

Midomo isemayo kweli hudumu milele,

bali ulimi wa uongo hudumu kwa muda mfupi tu.

Dhambi haiondolewi kwa maneno mengi,

bali wenye busara huzuia ulimi wao.

Hata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima akinyamaza,

na mwenye ufahamu akiuzuia ulimi wake.

Disciplinar a fala

Quem guarda a boca e a língua guarda a sua alma de angústias. A religião sem controle da língua é vã.

Kama mtu akidhani ya kuwa anayo dini lakini hauzuii ulimi wake kwa hatamu, hujidanganya moyoni mwake, wala dini yake haifai kitu.

Maombi ya mtu mwenye uchungu

Nilisema, "Nitaziangalia njia zangu

na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi;

nitaweka lijamu kinywani mwangu

wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami."

Yeyote kati yenu anayependa uzima

na kutamani kuziona siku nyingi njema,

basi auzuie ulimi wake na mabaya,

na midomo yake kutokana na kusema uongo.

Kinywa cha mwenye haki hutamka hekima,

nao ulimi wake huzungumza lililo haki.

Torati ya Mungu wake imo moyoni mwake;

nyayo zake hazitelezi.

Ulimi wangu utanena haki yako

na sifa zako mchana kutwa.

Kabla neno halijafika katika ulimi wangu,

wewe walijua kikamilifu, Ee Mwenyezi Mungu.

Ee Mwenyezi Mungu, uniokoe kutoka midomo ya uongo

na ndimi za udanganyifu.

Mwenyezi Mungu na akatilie mbali midomo yote ya hila

na kila ulimi uliojaa majivuno,

ule unaosema, "Kwa ndimi zetu tutashinda;

midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?"

Ee Bwana, uwatahayarishe waovu

na uwachanganyishie semi zao,

maana nimeona jeuri na ugomvi mjini.

Toda língua confessará

Ao nome de Jesus todo joelho se dobrará e toda língua confessará que Jesus Cristo é Senhor, para glória de Deus Pai.

Kwa hiyo, Mungu alimtukuza juu sana,

na kumpa Jina lililo kuu kuliko kila jina,

ili kwa Jina la Isa, kila goti lipigwe,

la vitu vya mbinguni, na vya duniani,

na vya chini ya nchi,

na kila ulimi ukiri kwamba

Isa Al-Masihi ni Bwana,

kwa utukufu wa Mungu Baba Mwenyezi.

Karama ya upendo

Hata kama nikisema kwa lugha za wanadamu na za malaika, kama sina upendo, nimekuwa kengele inayolia au toazi linalovuma.

Lakini nawaambia, katika siku ya hukumu watu watatoa maelezo kuhusu kila neno walilonena lisilo la maana. Kwa maana kwa maneno yako utahesabiwa haki, na kwa maneno yako utahukumiwa."

Lakini Mwenyezi Mungu akashuka ili auone mji na mnara ambao wanadamu walikuwa wanaujenga. Mwenyezi Mungu akasema, "Ikiwa kama taifa moja wanaozungumza lugha moja wameanza kufanya hili, basi hakuna lolote watakalopanga kufanya ambalo halitawezekana kwao. Njooni, tushuke tuvuruge lugha yao ili wasielewane wao kwa wao."

Hivyo Mwenyezi Mungu akawatawanya kutoka mahali pale waende duniani kote; nao wakaacha kuujenga huo mji. Ndiyo maana pakaitwa Babeli, kwa sababu hapo ndipo Mwenyezi Mungu alipoivuruga lugha ya dunia nzima. Kutoka hapo Mwenyezi Mungu akawatawanya duniani kote.

Seja o primeiro

Este artigo te tocou? Faça uma oração!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.