Pular para o conteúdo
Publicidade

Livramento

Por Bíblia Online

Deus é o grande Libertador. Através da Bíblia, vemos Deus livrando seu povo de inimigos, de perigos e da morte. Quem clama ao Senhor, Ele ouve e liberta.

Deus ouve e livra

Clamaram ao Senhor na sua tribulação, e Ele os livrou das suas angústias. O Senhor é refúgio e a salvação dos que nele confiam.

Wenye haki hulia, naye Bwana huwasikia,

huwaokoa katika taabu zao zote.

Ataniita, nami nitamjibu;

nitakuwa pamoja naye katika taabu,

nitamwokoa na kumheshimu.

Nitasema kumhusu Bwana, "Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu,

Mungu wangu, ambaye ninamtumaini."

Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji,

na maradhi ya kuambukiza ya kuua.

Mungu wetu ni Mungu aokoaye,

Bwana Mwenyezi hutuokoa na kifo.

Kwa kuwa umeniokoa toka kwenye mauti

na miguu yangu kwenye kujikwaa,

ili niweze kuenenda mbele za Mungu

katika nuru ya uzima.

Mwokoeni mnyonge na mhitaji,

wakomboeni kutoka mkononi mwa mwovu.

Ee Bwana, uwe radhi kuniokoa;

Ee Bwana, njoo hima unisaidie.

Kwa hiyo kila mtu mcha Mungu akuombe

wakati unapopatikana,

hakika maji makuu yatakapofurika

hayatamfikia yeye.

Livramento poderoso

Deus livrou Daniel dos leões, os jovens hebreus do fogo e Israel do Egito. Seu braço não é curto para salvar.

Ikiwa tutatupwa ndani ya tanuru iwakayo moto, Mungu tunayemtumikia anaweza kutuokoa na moto, naye atatuokoa kutoka mkononi mwako, ee mfalme. Lakini hata ikiwa hatatuokoa, ee mfalme, tunataka ufahamu kwamba, hatutaitumikia miungu yako wala kuiabudu sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha."

Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi,

kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.

Lakini Eleazari na Daudi wakasimama imara katikati ya lile shamba, nao wakalishindania na wakawaua Wafilisti. Naye Bwana akawapa ushindi mkubwa.

Kama ukifanya hivyo nao wakinililia, hakika nitasikia kilio chao.

Naam, tangu siku za kale, Mimi ndiye.

Hakuna hata mmoja awezaye kuokoa

kutoka mkononi wangu.

Mimi ninapotenda,

ni nani awezaye kutangua?"

Redenção e restauração

Todo aquele que invocar o nome do Senhor será salvo. Deus livra do pecado, da morte e de todo mal aqueles que se humilham diante dele.

Kwa maana, "Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokolewa."

Sasa basi, mbona unakawia? Inuka, ukabatizwe na dhambi zako zikasafishwe, ukiliita Jina lake.

na ili kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu: yaani, Yesu, yeye aliyetuokoa kutoka ghadhabu inayokuja.

kama watu wangu, wanaoitwa kwa Jina langu, watajinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuacha njia zao mbaya, basi nitasikia toka mbinguni na kuwasamehe dhambi yao na nitaiponya nchi yao.

Nanyi mkiomba lolote kwa Jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba apate kutukuzwa katika Mwana. Kama mkiniomba lolote kwa Jina langu nitalifanya.

Yesu Aahidi Roho Mtakatifu

"Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele.

Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii.

Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu ninyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu ninyi wenye nia mbili.

Ikiwa ninyi basi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao?

Humwomba Mungu, akapata kibali kwake,

huuona uso wa Mungu na kushangilia kwa furaha;

Mungu humrudisha katika hali yake ya uadilifu.

Seja o primeiro

Este artigo te tocou? Faça uma oração!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.