Livramento
Deus é o grande Libertador. Através da Bíblia, vemos Deus livrando seu povo de inimigos, de perigos e da morte. Quem clama ao Senhor, Ele ouve e liberta.
Deus ouve e livra
Clamaram ao Senhor na sua tribulação, e Ele os livrou das suas angústias. O Senhor é refúgio e a salvação dos que nele confiam.
Walilia, naye BWANA akasikia,
Akawaponya kutoka kwa taabu zao zote.
Ataniita nami nitamwitikia;
Nitakuwa pamoja naye taabuni,
Nitamwokoa na kumtukuza;
Atasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu nitakayemtumaini.
Maana Yeye atakuokoa kutoka kwa mtego wa mwindaji,
Na katika maradhi mabaya.
Mungu wetu ni Mungu wa kuokoa;
Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana.
Maana umeniponya nafsi yangu na mauti;
Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke?
Ili niende mbele za Mungu
Katika nuru ya walio hai.
Mwokoeni maskini na mhitaji;
Mwopoeni mikononi mwa wadhalimu.
Ee BWANA, uwe radhi kuniokoa,
Ee BWANA, unisaidie hima.
Kwa hiyo, hebu kila akuaminiye
Akuombe awapo katika dhiki.
Hakika maji makuu yafurikapo,
Hayatamfikia yeye.
Livramento poderoso
Deus livrou Daniel dos leões, os jovens hebreus do fogo e Israel do Egito. Seu braço não é curto para salvar.
Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuri liwakalo moto; naye atatuokoa mkononi mwako, Ee mfalme. Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.
Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu,
Na wale walionichukia;
Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi.
Ndipo hao wakasimama katikati ya shamba lile, wakalipigania, wakawaua Wafilisti; naye BWANA akafanya wokovu mkuu.
Ukiwatesa watu hao katika neno lolote, nao wakanililia mimi, hakika yangu nitasikia kilio chao,
Naam, tangu siku ya leo, mimi ndiye; wala hakuna awezaye kuokoa katika mkono wangu; mimi nitatenda kazi, naye ni nani awezaye kuizuia?
Redenção e restauração
Todo aquele que invocar o nome do Senhor será salvo. Deus livra do pecado, da morte e de todo mal aqueles que se humilham diante dele.
kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka.
Basi sasa, mbona unakawia? Simama, ubatizwe, ukaoshwe dhambi zako, ukiliitia jina lake.
na kumngojea Mwanawe kutoka mbinguni, ambaye alimfufua katika wafu, naye ni Yesu, mwenye kutuokoa kutoka kwa ghadhabu itakayokuja.
ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.
Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya.
Ahadi ya kupewa Roho Mtakatifu
Mkinipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele;
Tunajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo.
Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu zawadi njema, je! Si Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema zaidi wao wamwombao?
Yeye humwomba Mungu, naye akamtakabalia;
Hata auone uso wake kwa furaha;
Naye humrejeshea mtu haki yake.
Este artigo te tocou? Faça uma oração!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.