Maria
Maria, mãe de Jesus, é honrada nas Escrituras como a mulher escolhida por Deus para trazer ao mundo o Salvador. Sua fé, humildade e obediência são exemplo para todos os cristãos.
A escolhida de Deus
O anjo Gabriel anunciou a Maria que ela seria mãe do Filho do Altíssimo. Ela respondeu com fé: 'Faça-se em mim segundo a tua palavra.'
Kuzaliwa kwa Isa kwatabiriwa
Mwezi wa sita baada ya Elizabeti kupata mimba, Mungu alimtuma malaika Jibraili aende Galilaya katika mji wa Nasiri, kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu mmoja jina lake Yusufu wa nyumba ya Daudi. Jina la huyu mwanamwali bikira ni Mariamu. Naye malaika akaja kwake akamwambia: "Salamu, wewe uliyebarikiwa, Mwenyezi Mungu yu pamoja nawe!"
Ndipo malaika akamwambia, "Usiogope, Mariamu; umepata kibali kwa Mungu. Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto wa kiume na utamwita jina Isa. Yeye atakuwa mkuu, naye ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Mwenyezi Mungu atampa kiti cha utawala cha Daudi baba yake. Ataimiliki nyumba ya Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho."
Kuzaliwa kwa Isa
Kuzaliwa kwake Isa Al-Masihi kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alikuwa ameposwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Mariamu alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu wa Mungu.
O Magnificat
Maria cantou: 'Minha alma engrandece ao Senhor!' Seu cântico exalta a misericórdia, o poder e a fidelidade de Deus.
Wimbo wa Mariamu
Naye Mariamu akasema:
"Moyo wangu wamwadhimisha Mwenyezi Mungu,
nayo roho yangu inamfurahia
Mungu Mwokozi wangu,
kwa kuwa ameangalia kwa fadhili
unyonge wa mtumishi wake.
Hakika tangu sasa vizazi vyote vitaniita aliyebarikiwa,
kwa maana yeye Mwenye Nguvu
amenitendea mambo ya ajabu:
jina lake ni takatifu.
Rehema zake hudumu kizazi hadi kizazi,
kwa wale wanaomcha.
Kwa kuwa ametenda mambo ya ajabu kwa mkono wake;
amewatawanya wale wenye kiburi
ndani ya mioyo yao.
Amewashusha watawala toka kwenye viti vyao vya utawala,
lakini amewainua wanyenyekevu.
Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri,
bali matajiri amewafukuza mikono mitupu.
Amemsaidia mtumishi wake Israeli,
kwa kukumbuka ahadi yake ya kumrehemu
Ibrahimu na uzao wake milele,
kama alivyowaahidi baba zetu."
Hivyo Yusufu akapanda kutoka mji wa Nasiri ulioko Galilaya kwenda Yudea, hadi Bethlehemu, mji wa Daudi, kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo na wa nyumba ya Daudi. Alienda huko kujiandikisha pamoja na Mariamu, aliyekuwa amemposa, na alikuwa mjamzito. Wakiwa Bethlehemu, wakati wa Mariamu wa kujifungua ukawa umetimia, naye akamzaa mwanawe, kifungua mimba. Akamfunika nguo za kitoto na kumlaza katika hori la kulia ng’ombe, kwa sababu hapakuwa na nafasi katika nyumba ya wageni.
Lakini Mariamu akayaweka mambo haya yote moyoni mwake na kuyatafakari.
Kisha Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, "Mtoto huyu amewekwa kwa makusudi ya kuanguka na kuinuka kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ambayo watu watanena dhidi yake, ili mawazo ya mioyo mingi yadhihirike. Nao upanga utauchoma moyo wako."
Yusufu na Mariamu mama yake walipomwona walishangaa. Mama yake akamuuliza, "Mwanangu, mbona umetufanyia hivi? Tazama, mimi na baba yako tumekuwa tukikutafuta kwa wasiwasi mkubwa kila mahali."
Isa akawaambia, "Kwa nini kunitafuta? Hamkujua kwamba imenipasa kuwa katika nyumba ya Baba yangu?"
Lakini wao hawakuelewa maana ya lile alilowaambia.
Ndipo akashuka pamoja nao hadi Nasiri, naye alikuwa mtiifu kwao. Lakini mama yake akayaweka moyoni mwake mambo haya yote.
Mãe fiel até o fim
Maria acompanhou Jesus desde o nascimento até a cruz. Ela estava entre os discípulos no Pentecostes, fiel em oração.
Divai ilipokwisha, mama yake Isa akamwambia, "Wameishiwa na divai."
Isa akamwambia, "Mama, kwa nini unanihusisha? Saa yangu haijawadia."
Mama yake akawaambia wale watumishi, "Fanyeni lolote atakalowaambia."
Karibu na msalaba wa Isa walikuwa wamesimama mama yake, na dada wa mamaye, na Mariamu mke wa Klopa, na Mariamu Magdalene. Isa alipomwona mama yake mahali pale, na yule mwanafunzi aliyempenda akiwa amesimama karibu, Isa akamwambia mama yake, "Mama, huyu hapa ndiye mwanao." Kisha akamwambia yule mwanafunzi, "Nawe huyu hapa ndiye mama yako." Tangu wakati huo yule mwanafunzi akamchukua mama yake Isa nyumbani mwake.
Mama yake na ndugu zake Isa
Kisha wakaja ndugu zake Isa pamoja na mama yake. Wakiwa wamesimama nje, wakamtuma mtu kumwita. Umati wa watu walikuwa wameketi kumzunguka, nao wakamwambia, "Mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta."
Akawauliza, "Mama yangu na ndugu zangu ni nani?"
Kisha akawatazama wale watu waliokuwa wameketi kumzunguka pande zote, akasema, "Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu. Mtu yeyote anayetenda mapenzi ya Mungu, huyo ndiye kaka yangu, na dada yangu, na mama yangu."
Huyu si yule mwana wa seremala? Mama yake si yeye aitwaye Mariamu, nao ndugu zake si Yakobo, Yusufu, Simoni na Yuda? Nao dada zake wote, hawako hapa pamoja nasi? Mtu huyu amepata wapi basi mambo haya yote?"
Hawa wote waliungana pamoja katika maombi. Pia walikuwepo wanawake kadhaa, na Mariamu mama yake Isa, na ndugu zake Isa.
Este artigo te tocou? Faça uma oração!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.