Meditação
A meditação na Palavra de Deus é prática espiritual essencial. Diferente da meditação oriental, a meditação bíblica é reflexão profunda sobre as Escrituras — ruminar a Palavra dia e noite.
Meditar na Palavra dia e noite
Bem-aventurado o homem que medita na lei do Senhor de dia e de noite. Ele é como árvore plantada junto a ribeiros de águas.
Heri mtu yule ambaye haendi
katika shauri la watu waovu,
wala hasimami katika njia ya wenye dhambi,
au kuketi katika baraza la wenye mizaha.
Bali huifurahia Torati ya Mwenyezi Mungu,
naye huitafakari hiyo Torati usiku na mchana.
Usiache Kitabu hiki cha Torati kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi.
Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu.
Ninaitafakari mchana kutwa.
Amri zako zimenipa hekima kuliko adui zangu,
kwa kuwa nimezishika daima.
Nina akili kuliko walimu wangu wote,
kwa kuwa ninatafakari kuhusu sheria zako.
Nina ufahamu kuliko wazee,
kwa kuwa ninayatii mausia yako.
Ninatafakari maagizo yako
na kuziangalia njia zako.
Ninafurahia maagizo yako,
wala sitalipuuza neno lako.
kwa kuwa ninazifurahia amri zako
kwa sababu ninazipenda.
Ninaziinulia amri zako ambazo ninazipenda mikono yangu,
nami ninatafakari juu ya maagizo yako.
Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada;
nimeweka tumaini langu katika neno lako.
Sikufumba macho yangu usiku kucha,
ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako.
Frutos da meditação
A meditação produz entendimento, alegria e adoração. Quem medita na Palavra encontra direção, paz e renovação espiritual.
Maneno ya kinywa changu
na mawazo ya moyo wangu,
yapate kibali mbele zako, Ee Mwenyezi Mungu,
Mwamba wangu na Mkombozi wangu.
Kinywa changu kitasema maneno ya hekima,
usemi wa moyo wangu utatoa ufahamu.
Nitayakumbuka matendo ya Mwenyezi Mungu;
naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani.
Nitazitafakari kazi zako zote
na kuyawaza matendo yako makuu.
Nakumbuka siku za zamani;
natafakari juu ya kazi zako zote,
naangalia juu ya kazi
ambazo mikono yako imezifanya.
Ee Mungu, hekaluni mwako
tunatafakari upendo wako usiokoma.
Nitamwimbia Mwenyezi Mungu maisha yangu yote;
nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi.
Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye,
ninapofurahi katika Mwenyezi Mungu.