Milagres de Jesus
Os Evangelhos registram dezenas de milagres realizados por Jesus — curas, ressurreições, domínio sobre a natureza e libertações. Cada milagre revelava sua divindade e compaixão.
Curas de cegos e surdos
Jesus devolveu a visão aos cegos e a audição aos surdos, manifestando seu poder sobre toda enfermidade e deficiência.
Isa awaponya Vipofu
Isa alipokuwa akiondoka mahali pale, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti na kusema, "Mwana wa Daudi)., tuhurumie!"
Alipoingia mle nyumbani wale vipofu wakamjia. Naye Isa akawauliza, "Mnaamini kwamba ninaweza kufanya jambo hili?"
Wakamjibu, "Ndiyo, Bwana."
Ndipo Isa akagusa macho yao na kusema, "Iwe kwenu sawasawa na imani yenu." Macho yao yakafunguka. Isa akawaonya vikali, akisema, "Chungeni mtu yeyote asijue kuhusu jambo hili." Lakini wao wakaenda na kueneza habari zake katika eneo lile lote.
Isa awaponya vipofu wawili
Isa na wanafunzi wake walipokuwa wakiondoka Yeriko, umati mkubwa wa watu wakamfuata. Vipofu wawili walikuwa wameketi kando ya barabara. Waliposikia kwamba Isa alikuwa anapita, wakapaza sauti wakisema, "Bwana Isa, Mwana wa Daudi)., tuhurumie!"
Umati wa watu wakawakemea na kuwaambia wanyamaze, lakini wao wakazidi kupaza sauti wakisema, "Bwana Isa, Mwana wa Daudi, tuhurumie."
Isa akasimama na kuwaita, akawauliza, "Mnataka niwafanyie nini?"
Wakamjibu, "Bwana, tunataka kuona."
Isa akawahurumia na kuwagusa macho yao. Mara macho yao yakapata kuona, nao wakamfuata.
Isa amponya Kipofu huko Bethsaida
Wakafika Bethsaida na baadhi ya watu wakamleta mtu mmoja kipofu wakamsihi Isa amguse. Isa akamshika mkono huyo kipofu akampeleka nje ya kijiji. Baada ya kuyatemea mate macho ya yule kipofu na kumwekea mikono, Isa akamuuliza, "Unaona chochote?"
Yule kipofu akaangalia, akasema, "Ninaona watu, wanaonekana kama miti inayotembea."
Isa akamwekea tena mikono machoni. Kisha macho yake yakafunguka, kuona kwake kukarejea naye akaona kila kitu dhahiri. Isa akamtuma nyumbani mwake, akamwambia, "Hata kijijini usiingie."
Isa amponya mtu aliyekuwa kiziwi na bubu
Kisha Isa akaondoka sehemu za Tiro, akapita katikati ya Sidoni, hadi Bahari ya Galilaya na kuingia eneo la Dekapoli. Huko, watu wakamletea Isa mtu mmoja kiziwi, ambaye pia alikuwa na kigugumizi, wakamwomba aweke mkono wake juu ya huyo mtu.
Isa akampeleka yule kiziwi kando, mbali na watu, akatia vidole vyake masikioni mwa yule mtu. Kisha akatema mate na kuugusa ulimi wa yule mtu. Ndipo Isa akatazama mbinguni, akashusha pumzi kwa nguvu, akamwambia, "Efatha!" (yaani, "Funguka!") Mara masikio yake yakafunguka na ulimi wake ukaachiliwa, akaanza kuongea sawasawa.
Isa akawaamuru wasimwambie mtu yeyote habari hizi. Lakini kadiri alivyowakanya, ndivyo walivyozidi kutangaza kwa bidii. Walistaajabu mno. Wakasema, "Amefanya mambo yote vizuri mno! Amewawezesha viziwi wasikie na bubu waseme!"
Isa amponya kipofu Bartimayo
Kisha wakafika Yeriko. Isa alipokuwa akiondoka mjini na wanafunzi wake pamoja na umati mkubwa wa watu, kipofu mmoja, jina lake Bartimayo (maana yake "mwana wa Timayo"), alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada. Aliposikia kuwa ni Isa Al-Nasiri aliyekuwa anapita, akaanza kupaza sauti akisema, "Isa, Mwana wa Daudi)., nihurumie!"
Watu wengi wakamkemea, wakamwambia akae kimya, lakini yeye akazidi kupaza sauti, akisema, "Mwana wa Daudi, nihurumie!"
Isa akasimama na kusema, "Mwiteni."
Hivyo wakamwita yule mtu kipofu, wakamwambia, "Jipe moyo! Inuka, anakuita." Akiwa analivua lile joho lake, alisimama na kumwendea Isa.
Isa akamuuliza, "Unataka nikufanyie nini?"
Yule kipofu akajibu, "Mwalimu, nataka kuona."
Isa akamwambia, "Nenda zako, imani yako imekuponya." Mara akapata kuona, akamfuata Isa njiani.
Isa amponya kipofu karibu na Yeriko
Isa alipokuwa anakaribia Yeriko, kipofu mmoja alikuwa ameketi kando ya njia akiomba msaada. Kipofu huyo aliposikia umati wa watu wakipita, akauliza nini kilikuwa kikitendeka. Wakamwambia, "Isa Al-Nasiri anapita."
Akapaza sauti, akasema, "Isa, Mwana wa Daudi)., nihurumie!"
Wale waliokuwa wametangulia mbele wakamkemea, wakamwambia akae kimya. Lakini yeye akapaza sauti zaidi, "Mwana wa Daudi, nihurumie!"
Isa akasimama, akawaamuru wamlete huyo mtu kwake. Alipokaribia, Isa akamuuliza, "Unataka nikufanyie nini?"
Akajibu, "Bwana, nataka kuona."
Isa akamwambia, "Basi upate kuona. Imani yako imekuponya." Akapata kuona mara hiyo, akamfuata Isa, huku akimsifu Mungu. Watu wote walipoona mambo hayo, nao wakamsifu Mungu.
Isa amponya mtu aliyezaliwa kipofu
Isa alipokuwa akipita, akamwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wake wakamuuliza, "Mwalimu, ni nani aliyetenda dhambi; ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?"
Isa akawajibu, "Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake. Yanipasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi. Wakati niko ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu."
Baada ya kusema haya, akatema mate ardhini, akatengeneza tope kwa mate na kumpaka yule kipofu machoni. Kisha akamwambia, "Nenda ukanawe katika Bwawa la Siloamu" (Siloamu maana yake ni Kutumwa). Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona.
Curas de paralíticos e enfermos
Paralíticos caminharam, leprosos ficaram limpos e todo tipo de doença foi curada pelo toque e pela palavra de Jesus.
Mtu mmoja mwenye ukoma akaja na kupiga magoti mbele yake, akasema, "Bwana, ukitaka, unaweza kunitakasa."
Isa akanyoosha mkono wake akamgusa yule mtu, akamwambia, "Nataka. Takasika!" Mara yule mtu akatakasika ukoma wake. Kisha Isa akamwambia, "Hakikisha humwambii mtu yeyote. Lakini nenda ukajioneshe kwa kuhani, na utoe sadaka aliyoamuru Musa, ili kuwa ushuhuda kwao."
Wakati huo huo wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye mkeka. Isa alipoiona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, "Mwanangu, jipe moyo mkuu. Dhambi zako zimesamehewa."
Kwa ajili ya jambo hili, baadhi ya walimu wa Torati wakasema mioyoni mwao, "Huyu mtu anakufuru!"
Lakini Isa akiyafahamu mawazo yao, akawaambia, "Kwa nini mnawaza maovu mioyoni mwenu? Je, ni lipi lililo rahisi zaidi: kusema, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uende’? Lakini nataka mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu ana mamlaka duniani kusamehe dhambi." Ndipo akamwambia yule aliyepooza, "Inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani mwako." Yule mtu akasimama, akaenda nyumbani mwake.
na huko alikuwepo mtu aliyepooza mkono. Wakitafuta sababu ya kumshtaki Isa, wakamuuliza, "Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?"
Isa akawaambia, "Ni nani miongoni mwenu, mwenye kondoo wake ambaye huyo kondoo akitumbukia shimoni siku ya Sabato hatamtoa? Mtu ana thamani kubwa kuliko kondoo. Kwa hiyo ni halali kutenda mema siku ya Sabato."
Ndipo akamwambia yule mtu, "Nyoosha mkono wako." Akaunyoosha, nao ukaponywa ukawa mzima kama ule mwingine.
Mama mkwe wa Simoni alikuwa kitandani, ana homa, nao wakamweleza Isa habari zake. Hivyo Isa akamwendea, akamshika mkono na kumwinua. Kisha homa ikamwacha, naye akaanza kuwahudumia.
Isa amtakasa mtu mwenye ukoma
Mtu mmoja mwenye ukoma alimjia Isa, akapiga magoti, akimwomba, "Ukitaka, unaweza kunitakasa."
Isa, akiwa amejawa na huruma, akaunyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, "Nataka. Takasika!" Mara ukoma ukamtoka, naye akatakasika.
Ndipo baadhi ya watu wakaja wakamletea Isa mtu aliyepooza, akiwa amebebwa na watu wanne. Kwa kuwa hawakuweza kumfikisha kwa Isa kwa sababu ya umati wa watu, walitoboa tundu kwenye paa juu ya mahali Isa alikuwa, wakamshusha mtu aliyepooza akiwa amelalia mkeka wake. Isa alipoiona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, "Mwanangu, dhambi zako zimesamehewa."
Basi baadhi ya walimu wa Torati waliokuwa wameketi pale wakawaza mioyoni mwao, "Kwa nini mtu huyu anasema hivi? Huyu anakufuru! Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?"
Mara moja Isa akatambua rohoni mwake kile walichokuwa wanawaza mioyoni mwao, naye akawaambia, "Kwa nini mnawaza hivyo mioyoni mwenu? Je, ni lipi lililo rahisi zaidi: kumwambia huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uchukue mkeka wako, uende’? Lakini ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani ya kusamehe dhambi": Isa akamwambia yule aliyepooza, "Nakuambia, inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani kwako." Yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama, akachukua mkeka wake, akatembea machoni pao wote! Jambo hili likawashangaza wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, "Hatujapata kuona jambo kama hili kamwe!"
Isa amponya mtu aliyepooza mkono
Isa akaingia tena ndani ya sinagogi, na kulikuwa na mtu aliyepooza mkono. Wakawa wanamwangalia waone kama atamponya huyo mtu siku ya Sabato, ili wapate sababu ya kumshtaki. Isa akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, "Njoo hapa mbele ya watu wote."
Kisha Isa akawauliza, "Je, ni lipi lililo halali siku ya Sabato: Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuua?" Lakini wao wakanyamaza.
Isa akawatazama kwa hasira watu waliomzunguka pande zote, akahuzunika sana kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, "Nyoosha mkono wako." Akaunyoosha, nao ukawa umeponywa kabisa!
Isa amtakasa mtu mwenye ukoma
Ikawa siku moja Isa alipokuwa katika mji fulani, mtu mmoja mwenye ukoma mwili mzima akamjia. Alipomwona Isa, alianguka chini hadi uso wake ukagusa ardhi, akamsihi akisema, "Bwana, ukitaka, unaweza kunitakasa."
Isa akanyoosha mkono wake, akamgusa yule mtu, akamwambia, "Nataka. Takasika!" Na mara ukoma wake ukatakasika.
Wakaja watu wamembeba mgonjwa aliyepooza kwenye mkeka. Wakajaribu kumwingiza ndani ili wamweke mbele ya Isa. Walipokuwa hawawezi kufanya hivyo kwa sababu ya umati wa watu, wakapanda juu ya paa, wakaondoa baadhi ya matofali, wakamteremsha yule mgonjwa kwa mkeka wake hadi katikati ya umati ule pale mbele ya Isa.
Isa alipoiona imani yao, akamwambia yule mgonjwa, "Rafiki, dhambi zako zimesamehewa."
Mafarisayo na wale walimu wa Torati wakaanza kuuliza, "Ni nani mtu huyu anayesema maneno ya kukufuru? Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?"
Isa akijua mawazo yao akawauliza, "Kwa nini mnawaza hivyo mioyoni mwenu? Je, ni lipi lililo rahisi zaidi, kumwambia, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uende’? Lakini ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi." Akamwambia yule aliyepooza, "Nakuambia, inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani mwako." Mara yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama mbele yao wote, akachukua mkeka wake, akaenda zake nyumbani, huku akimtukuza Mungu.
Isa amponya mtu aliyepooza mkono
Ikawa siku nyingine ya Sabato, Isa aliingia ndani ya sinagogi na akawa anafundisha. Huko palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kuume ulikuwa umepooza. Mafarisayo na walimu wa Torati walikuwa wakitafuta sababu ya kumshtaki Isa. Kwa hivyo wakawa wanamwangalia sana ili waone kama ataponya katika siku ya Sabato. Lakini Isa alijua mawazo yao, hivyo akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, "Inuka usimame mbele ya watu wote." Hivyo yule mtu akainuka, akasimama mbele yao wote.
Ndipo Isa akawaambia wale walimu wa Torati na Mafarisayo, "Nawauliza ninyi, ni lipi lililo halali siku ya Sabato? Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuyaangamiza?"
Akawatazama watu wote waliokuwepo, kisha akamwambia yule mtu, "Nyoosha mkono wako!" Akaunyoosha, na mkono wake ukawa umeponywa kabisa.
Isa amponya mtumishi wa jemadari
Baada ya Isa kumaliza kusema haya yote kwa watu waliokuwa wanamsikiliza, akaingia Kapernaumu. Mtumishi wa jemadari mmoja Mrumi, ambaye bwana wake alimthamini sana, alikuwa mgonjwa sana karibu na kufa. Jemadari huyo aliposikia habari za Isa, aliwatuma wazee wa Wayahudi kwake, wakamwomba aje kumponya mtumishi wa huyo jemadari. Wale wazee walipofika kwa Isa, wakamsihi sana amsaidie yule jemadari wakisema, "Mtu huyu anastahili wewe umfanyie jambo hili, kwa sababu analipenda taifa letu tena ametujengea sinagogi." Hivyo Isa akaongozana nao.
Lakini alipokuwa hayuko mbali na nyumbani, yule jemadari akatuma rafiki zake kumwambia Isa, "Bwana, usijisumbue, kwani mimi sistahili wewe kuingia chini ya dari yangu. Ndiyo maana sikujiona hata ninastahili kuja kwako wewe. Lakini sema neno tu, naye mtumishi wangu atapona. Kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtu niliyewekwa chini ya mamlaka, nikiwa na askari chini yangu. Nikimwambia huyu, ‘Nenda,’ yeye huenda; na mwingine nikimwambia, ‘Njoo,’ yeye huja. Nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hivi,’ yeye hufanya."
Isa aliposikia maneno haya, alishangazwa naye sana. Akageukia umati ule wa watu waliokuwa wanamfuata, akawaambia, "Sijaona imani kubwa namna hii hata katika Israeli." Nao wale watu waliokuwa wametumwa kwa Isa waliporudi nyumbani walimkuta yule mtumishi amepona.
Wakati huo huo akaja mwanamke mmoja aliyekuwa na pepo mchafu, naye alikuwa amepinda mgongo kwa muda wa miaka kumi na nane, wala alikuwa hawezi kunyooka wima. Isa alipomwona, akamwita, akamwambia, "Mwanamke, uwe huru, umepona ugonjwa wako." Isa alipomwekea mikono yake, akasimama wima mara moja, akaanza kumtukuza Mungu.
Isa nyumbani mwa Farisayo
Siku moja ya Sabato, Isa alipoenda kula chakula kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo, watu walikuwa wakimchunguza kwa makini. Hapo mbele yake palikuwa na mtu mmoja mwenye ugonjwa wa kuvimba mwili. Isa akawauliza wale Mafarisayo na walimu wa Torati, "Je, ni halali kuponya watu siku ya Sabato au la?" Wakakaa kimya. Hivyo Isa akamshika yule mgonjwa mkono na kumponya, akamruhusu aende zake.
Isa atakasa watu kumi wenye ukoma
Isa alipokuwa njiani akienda Yerusalemu, alipitia mpakani mwa Samaria na Galilaya. Alipokuwa akiingia kwenye kijiji kimoja, watu kumi waliokuwa na ukoma wakakutana naye. Wakasimama mbali, wakapaza sauti, wakasema, "Isa, Bwana, tuhurumie!"
Alipowaona akawaambia, "Nendeni mkajioneshe kwa makuhani." Nao walipokuwa njiani wakienda, wakatakasika.
Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa Isa, akimsifu Mungu kwa sauti kuu. Akajitupa miguuni mwa Isa akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria.
Isa akauliza, "Je, hawakutakaswa wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa? Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumshukuru Mungu isipokuwa huyu mgeni?" Isa akamwambia, "Inuka na uende zako, imani yako imekuponya."
Isa amponya mtu kwenye Bwawa la Bethzatha
Baada ya haya, kulikuwa na Sikukuu ya Wayahudi, naye Isa akapanda kwenda Yerusalemu. Huko Yerusalemu, karibu na mlango uitwao Mlango wa Kondoo, palikuwa na bwawa moja lililoitwa Bethzatha kwa Kiebrania, ambalo lilikuwa limezungukwa na makumbi matano. Hapa palikuwa na idadi kubwa ya wasiojiweza, yaani vipofu, viwete, na waliopooza [wakingojea maji yatibuliwe. Kwa maana malaika alikuwa akishuka wakati fulani, akayatibua maji. Yule angekuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya maji kutibuliwa alipona ugonjwa wowote aliokuwa nao]. Mtu mmoja aliyekuwa ameugua kwa miaka thelathini na nane alikuwa hapo. Isa alipomwona akiwa amelala hapo, na akijua amekuwa katika hali hiyo kwa muda mrefu, akamwambia, "Je, wataka kuponywa?"
Yule mgonjwa akamjibu, "Bwana, mimi sina mtu wa kuniingiza bwawani maji yanapotibuliwa. Nami ninapotaka kutumbukia bwawani, mtu mwingine huingia kabla yangu."
Isa akamwambia, "Inuka! Chukua mkeka wako na uende." Mara yule mtu akapona, akachukua mkeka wake, akaanza kutembea.
Basi siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato.
Hivyo Isa akafika tena Kana ya Galilaya, kule alikuwa amebadili maji kuwa divai. Kulikuwa na afisa mmoja wa mfalme, ambaye mwanawe alikuwa mgonjwa huko Kapernaumu. Huyo mtu aliposikia kwamba Isa alikuwa amewasili Galilaya kutoka Yudea, alimwendea na kumsihi aende akamponye mwanawe, aliyekuwa mgonjwa karibu ya kufa.
Isa akamwambia, "Ninyi watu msipoona ishara na miujiza kamwe hamtaamini."
Yule afisa wa mfalme akamwambia, "Bwana, tafadhali shuka kabla mwanangu hajafa."
Isa akamjibu, "Nenda zako, mwanao yu hai."
Yule afisa akaamini yale maneno Isa aliyomwambia, akaenda zake. Alipokuwa bado yuko njiani, akakutana na watumishi wake, wakamwambia kwamba mwanawe yu mzima. Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, "Jana saa saba, ndipo homa iliisha."
Ndipo baba wa huyo mtoto akakumbuka kuwa huo ndio wakati Isa alikuwa amemwambia, "Mwanao yu hai." Kwa hiyo yeye na wote wa nyumbani mwake wakamwamini Isa.
Hii ilikuwa ishara ya pili ambayo Isa alifanya aliporudi Galilaya kutoka Yudea.
A mulher com fluxo de sangue
Uma mulher que sofria há doze anos tocou a orla do manto de Jesus e foi curada instantaneamente pela sua fé.
Wakati huo huo, mwanamke mmoja, aliyekuwa na ugonjwa wa kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na mbili, akaja nyuma ya Isa, akagusa upindo wa vazi lake, kwa maana alisema moyoni mwake, "Nikigusa tu vazi lake, nitaponywa."
Isa akageuka, naye alipomwona akamwambia, "Binti, jipe moyo, imani yako imekuponya." Naye yule mwanamke akapona kuanzia saa hiyo.
Hapo palikuwa na mwanamke aliyekuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa miaka kumi na mbili. Mwanamke huyu alikuwa ameteseka sana kwa mikono ya matabibu wengi, na kutumia kila kitu alichokuwa nacho. Lakini badala ya kupona, hali yake ilizidi kuwa mbaya. Alikuwa amesikia habari za Isa, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, kwa maana alisema moyoni mwake, "Nikiligusa vazi lake tu, nitaponywa." Mara kutoka damu kwake kukakoma, naye akajisikia mwilini mwake amepona kabisa.
Palikuwa na mwanamke mmoja aliyekuwa na tatizo la kutokwa damu kwa muda wa miaka kumi na mbili, [na alikuwa amegharimia mali yake yote kwa matibabu] lakini hakuna yeyote aliyeweza kumponya. Huyo mwanamke akaja kwa nyuma ya Isa na kugusa upindo wa vazi lake. Mara kutokwa damu kwake kukakoma.
Isa akauliza, "Ni nani aliyenigusa?"
Watu wote walipokana, Petro akasema, "Bwana, umati huu wa watu wanakusonga na kukusukuma kila upande."
Lakini Isa akasema, "Kuna mtu aliyenigusa, kwa maana nimetambua kuwa nguvu zimenitoka."
Yule mwanamke alipofahamu ya kuwa hawezi kuendelea kujificha, alikuja akitetemeka, akaanguka miguuni mwa Isa. Akaeleza mbele ya watu wote kwa nini alimgusa na jinsi alivyoponywa mara moja. Basi Isa akamwambia, "Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani."
Ressurreições
Jesus ressuscitou mortos — a filha de Jairo, o filho da viúva de Naim e Lázaro. Ele é Senhor sobre a morte.
Isa amponya mwanamke na kumfufua msichana
Isa alipokuwa akiwaambia mambo haya, kiongozi wa sinagogi akaingia, akapiga magoti mbele yake, akamwambia, "Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini njoo uweke mkono wako juu yake, naye ataishi." Isa akaondoka akafuatana naye, nao wanafunzi wake pia wakaandamana naye.
Isa alipofika nyumbani mwa yule kiongozi wa sinagogi na kuwaona waombolezaji wakipiga filimbi za maombolezo na watu wengi wakipiga kelele, akawaambia, "Ondokeni! Kwa maana binti huyu hakufa, bali amelala." Wakamcheka kwa dhihaka. Lakini watu walipokwisha kutolewa nje, akaingia mle ndani na kumshika yule binti mkono, naye akaamka.
Kisha mmoja wa viongozi wa sinagogi aliyeitwa Yairo akafika pale. Naye alipomwona Isa, akapiga magoti miguuni pake, akamsihi akisema, "Binti yangu mdogo ni mgonjwa mahututi. Tafadhali nakusihi, njoo uweke mikono yako juu yake ili apate kupona, naye ataishi." Hivyo Isa akaenda pamoja naye.
Umati mkubwa wa watu wakamfuata, nao watu wakawa wanamsonga.
Walipofika nyumbani mwa yule kiongozi wa sinagogi, Isa akaona ghasia, watu wakilia na kuomboleza kwa sauti kubwa. Alipokwisha kuingia ndani, akawaambia, "Kwa nini mnafanya ghasia na kulia? Mtoto hajafa, bali amelala tu." Wale watu wakamcheka.
Baada ya kuwafukuza wote nje, Isa akaenda na baba na mama wa yule mtoto, pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao, wakaingia ndani hadi pale alipokuwa mtoto yule. Akamshika mtoto mkono, akamwambia, "Talitha koum!" (maana yake, "Msichana, nakuambia: amka!") Mara yule msichana akasimama, akaanza kutembea (alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili). Walipoona haya, wakastaajabu sana.
Isa akawauliza, "Niwafananishe na nini watu wa kizazi hiki? Wanafanana na nini? Wao ni kama watoto waliokaa sokoni wakiitana wao kwa wao, wakisema:
" ‘Tuliwapigia filimbi,
lakini hamkucheza;
tuliwaimbia nyimbo za maombolezo,
lakini hamkulia.’
Kwa maana Yahya alikuja, alikuwa hali mkate wala hanywi divai, nanyi mkasema, ‘Yeye ana pepo mchafu.’ Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa, nanyi mnasema: ‘Tazameni huyu mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na "wenye dhambi." ’ Lakini hekima huthibitishwa kuwa kweli na watoto wake wote."
Isa apakwa mafuta na mwanamke mwenye dhambi
Basi Farisayo mmoja alimwalika Isa kwake ale chakula. Hivyo Isa akaenda nyumbani mwa yule Farisayo na kuketi mezani. Palikuwa na mwanamke mmoja katika mji ule aliyekuwa mwenye dhambi. Alipopata habari kwamba Isa alikuwa akila chakula nyumbani mwa yule Farisayo, akaleta chupa ya marhamu yenye manukato.
Kisha mtu mmoja, jina lake Yairo, aliyekuwa kiongozi wa sinagogi, akaja na kuanguka miguuni mwa Isa, akimwomba afike nyumbani mwake, kwa kuwa binti yake wa pekee, mwenye umri wa miaka kumi na mbili, alikuwa anakufa.
Isa alipokuwa akienda, umati wa watu wakamsonga sana.
Isa alipokuwa bado anasema, akaja mtumishi kutoka nyumbani mwa Yairo, yule kiongozi wa sinagogi, kumwambia, "Binti yako amekwisha kufa. Usiendelee kumsumbua Mwalimu."
Isa aliposikia jambo hili, akamwambia Yairo, "Usiogope. Amini tu, naye binti yako atapona."
Walipofika nyumbani mwa Yairo, hakumruhusu mtu yeyote aingie ndani naye isipokuwa Petro, Yohana na Yakobo, pamoja na baba na mama wa yule binti. Wakati ule ule watu wote walikuwa wakilia na kuomboleza kwa ajili ya huyo binti. Isa akawaambia, "Acheni kulia. Huyu binti hajafa, ila amelala."
Wao wakamcheka kwa dharau, wakijua kuwa amekwisha kufa. Isa akamshika yule binti mkono na kuita, "Binti, amka!" Roho yake ikamrudia, naye akainuka mara moja. Akaamuru apewe kitu cha kula. Wazazi wake wakastaajabu sana, lakini Isa akawakataza wasimwambie mtu yeyote kuhusu yale yaliyotukia.
Kifo cha Lazaro
Basi mtu mmoja, jina lake Lazaro, alikuwa mgonjwa. Yeye alikuwa akiishi Bethania, kijiji cha Mariamu na Martha dada yake. (Huyu Mariamu, ambaye Lazaro kaka yake alikuwa mgonjwa, ndiye alimpaka Bwana Isa mafuta na kuifuta miguu yake kwa nywele zake.) Hivyo hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Isa kumwambia, "Bwana, yule umpendaye ni mgonjwa."
Lakini Isa aliposikia hayo, akasema, "Ugonjwa huu hautaleta mauti, bali ni wa kudhihirisha utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu apate kutukuzwa kutokana na ugonjwa huu." Isa aliwapenda Martha, Mariamu na Lazaro ndugu yao. Hata hivyo, baada ya kusikia kwamba Lazaro ni mgonjwa, alikawia huko alikokuwa kwa siku mbili zaidi.
Ndipo akawaambia wanafunzi wake, "Haya, turudi Yudea."
Wanafunzi wake wakamwambia, "Mwalimu, Wayahudi walikuwa wanataka kukupiga mawe, nawe unataka kurudi huko?"
Isa akawajibu, "Si kuna saa kumi na mbili za mchana katika siku moja? Wanaotembea mchana hawawezi kujikwaa, kwa maana wanaona kwa nuru ya ulimwengu huu. Lakini wale wanaotembea usiku hujikwaa kwa sababu hawana nuru ndani yao."
Baada ya kusema haya, Isa akawaambia, "Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini naenda kumwamsha."
Wanafunzi wakamwambia, "Bwana, kama amelala usingizi ataamka." Hata hivyo, Isa alikuwa anazungumzia kuwa Lazaro amekufa, lakini wanafunzi wake hawakuelewa, walidhani kwamba anasema Lazaro amelala usingizi tu.
Kwa hiyo Isa akawaambia waziwazi, "Lazaro amekufa.
Domínio sobre a natureza
Jesus acalmou a tempestade, andou sobre as águas e multiplicou pães. A natureza obedece à voz do seu Criador.
Isa atuliza dhoruba
Naye alipoingia kwenye mashua, wanafunzi wake wakamfuata. Ghafula, kukatokea dhoruba kali baharini hata mashua ikaanza kufunikwa na mawimbi, lakini Isa alikuwa amelala usingizi. Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, "Bwana, tuokoe! Tunazama!"
Naye Isa akawaambia, "Kwa nini mnaogopa, enyi wa imani haba?" Kisha akaamka na kukemea dhoruba na mawimbi, nayo bahari ikatulia kabisa.
Wale watu wakashangaa, wakisema, "Ni mtu wa namna gani huyu? Hata upepo na mawimbi vinamtii!"
Ilipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, "Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makundi ya watu ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula."
Isa akawaambia, "Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula."
Wakamjibu, "Tuna mikate mitano na samaki wawili tu."
Akawaambia, "Nileteeni hivyo vitu hapa." Isa akaagiza umati wa watu wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawagawia ule umati. Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili. Idadi ya watu waliokula walikuwa wanaume wapatao elfu tano, bila kuhesabu wanawake na watoto.
Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Isa akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji.
Isa alisha wanaume 4,000
Kisha Isa akawaita wanafunzi wake, akawaambia, "Ninahurumia umati huu wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa pamoja nami kwa muda wa siku tatu, na hawana chakula chochote. Nami sipendi kuwaaga watu wakiwa na njaa, wasije wakazimia njiani."
Wanafunzi wake wakasema, "Tutapata wapi mikate ya kutosha kulisha umati mkubwa namna hii, nasi tuko nyikani?"
Isa akawauliza, "Mnayo mikate mingapi?"
Wakamjibu, "Tunayo mikate saba na visamaki vichache."
Isa akaagiza watu wote waketi chini. Kisha akachukua ile mikate saba na wale samaki, naye akamshukuru Mungu, akavimega na kuwapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu. Wote wakala na kushiba. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba. Idadi ya watu walikuwa wanaume elfu nne, bila kuhesabu wanawake na watoto.
Isa na Petro watoa kodi ya Hekalu
Baada ya Isa na wanafunzi wake kufika Kapernaumu, wakusanya kodi ya Hekalu wakamjia Petro na kumuuliza, "Je, Mwalimu wenu halipi kodi ya Hekalu?"
Petro akajibu, "Ndiyo, yeye hulipa." Petro aliporudi nyumbani, Isa akawa wa kwanza kulizungumzia, akamuuliza, "Unaonaje Simoni? Wafalme wa dunia hupokea ushuru na kodi kutoka kwa nani? Je, ni kutoka kwa watoto wao au kutoka kwa watu wengine?"
Petro akamjibu, "Kutoka kwa watu wengine."
Isa akamwambia, "Kwa hiyo watoto wao wamesamehewa. Lakini ili tusije tukawaudhi, nenda baharini ukatupe ndoana. Mchukue samaki wa kwanza utakayemvua. Fungua kinywa chake nawe utakuta humo fedha, ichukue ukalipe kodi yako na yangu."
Mtini ulionyauka
Asubuhi na mapema, Isa alipokuwa akirudi mjini, alikuwa na njaa. Akauona mtini kando ya barabara, naye akaukaribia, lakini hakupata tunda lolote ila majani. Ndipo akauambia, "Wewe usizae matunda tena kamwe!" Papo hapo ule mtini ukanyauka.
Wanafunzi wake walipoona jambo hili, wakashangaa, wakamuuliza, "Imekuwaje mtini huu kunyauka ghafula?"
Isa akawajibu, "Amin, nawaambia, mkiwa na imani wala msiwe na shaka, si kwamba mtaweza kufanya tu yale yaliyofanyika kwa huu mtini, bali hata mkiuambia huu mlima, ‘Ng’oka, ukatupwe baharini,’ litafanyika. Yoyote mtakayoyaomba mkisali na mkiamini, mtayapokea."
Kukawa na dhoruba kali, nayo mawimbi yakaipiga ile mashua hata ikawa karibu kujaa maji. Isa alikuwa katika shetri, akiwa analala juu ya mto. Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, "Mwalimu, hujali kama tunazama?"
Akaamka, akaukemea ule upepo, akayaambia yale mawimbi, "Uwe kimya! Tulia!" Ule upepo ukatulia, kukawa shwari kabisa.
Isa akawaambia wanafunzi wake, "Kwa nini mnaogopa hivyo? Je, bado hamna imani?"
Nao wakawa wameogopa sana, wakaulizana, "Ni nani huyu? Hata upepo na mawimbi vinamtii!"
Mchana ulipokuwa umeendelea sana, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, "Mahali hapa ni nyikani, nazo saa zimeenda sana. Waage watu ili waende mashambani na vijijini jirani, wakajinunulie chakula."
Lakini Isa akawajibu, "Ninyi wapeni chakula."
Wakamwambia, "Je, twende tukanunue mikate ya dinari mia mbili ili tuwape watu hawa wale?"
Akawauliza, "Kuna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie."
Walipokwisha kujua, wakarudi, wakamwambia, "Kuna mikate mitano na samaki wawili."
Kisha Isa akawaamuru wawaketishe watu makundi makundi kwenye majani, nao wakaketi kwenye vikundi vya watu mia mia, na wengine hamsini hamsini. Isa akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi wake ili wawagawie wale watu wote. Pia akawagawia wote wale samaki wawili. Watu wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wake wakakusanya vipande vilivyosalia vya mikate na samaki, wakajaza vikapu kumi na viwili. Idadi ya wanaume waliokula walikuwa elfu tano.
Akawaona wanafunzi wake wanahangaika na kupiga makasia kwa nguvu, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho. Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Isa akawaendea wanafunzi wake, akiwa anatembea juu ya maji. Alikuwa karibu kuwapita, lakini walipomwona akitembea juu ya maji, wakadhani ni mzimu. Wakapiga yowe, kwa sababu wote walipomwona waliogopa.
Mara Isa akasema nao, akawaambia, "Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope!" Akapanda ndani ya mashua nao, na ule upepo ukakoma! Wakashangaa kabisa,
Isa alisha wanaume 4,000
Katika siku hizo, umati mkubwa wa watu walikusanyika tena. Kwa kuwa walikuwa hawana chakula, Isa akawaita wanafunzi wake akawaambia, "Ninahurumia umati huu wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa nami kwa muda wa siku tatu na hawana chakula. Nikiwaaga waende nyumbani bila kula, watazimia njiani kwa sababu baadhi yao wametoka mbali."
Wanafunzi wake wakamjibu, "Lakini hapa nyikani tutapata wapi mikate ya kutosha kuwalisha?"
Isa akawauliza, "Mna mikate mingapi?"
Wakajibu, "Tuna mikate saba."
Akawaambia watu waketi chini. Akaichukua ile mikate saba na kushukuru, baadaye akaimega na kuwapa wanafunzi wake ili wawagawie watu. Wanafunzi wake wakafanya hivyo. Walikuwa pia na visamaki vichache, Isa akavibariki, akawaamuru wanafunzi wake wawagawie watu. Wale watu walikula na kutosheka. Baadaye wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu saba. Watu waliokula walikuwa wapata elfu nne. Baada ya kuwaaga,
Isa aulaani mtini usiozaa
Kesho yake walipokuwa wakitoka Bethania, Isa alikuwa na njaa. Akauona mtini kwa mbali, naye akaenda ili aone kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, akakuta una majani tu, kwa kuwa hayakuwa majira ya tini. Akauambia ule mti, "Tangu leo mtu yeyote asile kamwe matunda kutoka kwako." Wanafunzi wake walimsikia akisema hayo.
Mtini ulionyauka
Kesho yake asubuhi walipokuwa wakipita, wakauona ule mtini umenyauka kutoka juu hadi kwenye mizizi yake. Petro akakumbuka na kumwambia Isa, "Mwalimu, tazama! Ule mtini ulioulaani umenyauka!"
Isa akawajibu, "Mwaminini Mungu. Amin, nawaambia, mtu yeyote atakayeuambia mlima huu, ‘Ng’oka ukatupwe baharini,’ wala asione shaka moyoni mwake, bali aamini kwamba hayo asemayo yametukia, atatimiziwa. Kwa sababu hiyo nawaambia, yoyote mtakayoyaomba mkisali, aminini kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu. Nanyi kila msimamapo kusali, sameheni mkiwa na neno na mtu, ili naye Baba yenu aliye mbinguni awasamehe ninyi makosa yenu. [
Wanafunzi wa kwanza wa Isa
Siku moja Isa alipokuwa amesimama karibu na Ziwa la Genesareti, watu wengi walimsonga ili wapate kusikia neno la Mungu. Akaona mashua mbili ukingoni mwa ziwa, zikiwa zimeachwa hapo na wavuvi waliokuwa wanaosha nyavu zao. Akaingia katika mojawapo ya hizo mashua ambayo ilikuwa ya Simoni, akamwomba aisogeze ndani ya maji kidogo kutoka ufuoni. Kisha akaketi na kufundisha watu akiwa mle ndani ya mashua.
Alipomaliza kunena, akamwambia Simoni, "Sasa peleka mashua hadi kilindini kisha mshushe nyavu zenu mkavue samaki."
Simoni akamjibu, "Bwana, tumefanya kazi ya kuchosha usiku kucha na hatukuvua chochote. Lakini, kwa neno lako nitazishusha nyavu."
Nao walipozishusha nyavu zao, wakavua samaki wengi sana, nyavu zao zikajaa zikaanza kukatika. Wakawaashiria wavuvi wenzao kwenye ile mashua nyingine ili waje kuwasaidia. Wakaja, wakajaza mashua zote mbili samaki hata zikaanza kuzama.
Simoni Petro alipoona haya yaliyotukia, alianguka miguuni pa Isa na kumwambia, "Bwana, ondoka kwangu. Mimi ni mtu mwenye dhambi!" Kwa kuwa yeye na wavuvi wenzake walikuwa wameshangazwa sana na wingi wa samaki waliokuwa wamepata. Vivyo hivyo wenzake Simoni, yaani Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, walishangazwa pia.
Ndipo Isa akamwambia Simoni, "Usiogope, tangu sasa utakuwa mvuvi wa watu." Hivyo wakasogeza mashua zao hadi ufuoni mwa bahari, wakaacha kila kitu na kumfuata.
Isa atuliza dhoruba
Siku moja Isa alipanda ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, "Tuvukeni hadi ng’ambo ya ziwa." Nao wakaondoka. Hivyo walipokuwa wakienda, akalala usingizi. Dhoruba kali ikatokea mle ziwani, hata mashua ikawa inajaa maji, nao walikuwa katika hatari kubwa.
Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, "Bwana, Bwana, tunaangamia!"
Yeye akaamka, akaukemea ule upepo na yale mawimbi; dhoruba ikakoma, nako kukawa shwari. Akawauliza wanafunzi wake, "Imani yenu iko wapi?"
Kwa woga na mshangao wakaulizana, "Huyu ni nani, ambaye anaamuru hata upepo na maji, navyo vikamtii?"
Isa atuliza dhoruba
Siku moja Isa alipanda ndani ya mashua pamoja na wanafunzi wake, akawaambia, "Tuvukeni hadi ng’ambo ya ziwa." Nao wakaondoka. Hivyo walipokuwa wakienda, akalala usingizi. Dhoruba kali ikatokea mle ziwani, hata mashua ikawa inajaa maji, nao walikuwa katika hatari kubwa.
Wanafunzi wake wakamwendea na kumwamsha, wakisema, "Bwana, Bwana, tunaangamia!"
Yeye akaamka, akaukemea ule upepo na yale mawimbi; dhoruba ikakoma, nako kukawa shwari. Akawauliza wanafunzi wake, "Imani yenu iko wapi?"
Kwa woga na mshangao wakaulizana, "Huyu ni nani, ambaye anaamuru hata upepo na maji, navyo vikamtii?"
Isa amponya mtu mwenye pepo mchafu
Basi wakafika katika nchi ya Wagerasi, iliyo upande wa pili wa ziwa kutoka Galilaya.
Ilipokaribia jioni, wale mitume kumi na wawili wakaenda kwa Isa na kumwambia, "Waage watu hawa ili waende vijijini jirani na mashambani, ili wapate chakula na mahali pa kulala, kwa maana hapa tuko nyikani."
Isa akawajibu, "Ninyi wapeni chakula."
Nao wakajibu, "Tuna mikate mitano na samaki wawili tu. Labda twende tukanunue chakula cha kuwatosha watu hawa wote." (Walikuwepo wanaume wapatao elfu tano.)
Isa akawaambia wanafunzi wake, "Waketisheni katika vikundi vya watu hamsini hamsini." Wanafunzi wakafanya hivyo, wakawaketisha wote. Isa akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama mbinguni, akavibariki na kuvimega. Kisha akawapa wanafunzi ili wawagawie watu. Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili.
Arusi huko Kana
Siku ya tatu kulikuwa na arusi katika mji wa Kana ya Galilaya, naye mama yake Isa alikuwepo. Isa pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini pia. Divai ilipokwisha, mama yake Isa akamwambia, "Wameishiwa na divai."
Isa akamwambia, "Mama, kwa nini unanihusisha? Saa yangu haijawadia."
Mama yake akawaambia wale watumishi, "Fanyeni lolote atakalowaambia."
Basi hapo palikuwa na mitungi sita iliyotengenezwa kwa mawe; iliwekwa hapo kwa ajili ya desturi ya Kiyahudi ya kujitakasa; kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu.
Isa akawaambia wale watumishi, "Ijazeni hiyo mitungi maji." Nao wakaijaza ile mitungi hadi juu.
Kisha akawaambia, "Sasa choteni hayo maji kidogo; mpelekeeni mkuu wa sherehe."
Hivyo wakachota, wakampelekea. Yule mkuu wa sherehe akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yamebadilishwa kuwa divai. Hakujua divai hiyo ilikotoka ingawa wale watumishi waliochota yale maji walifahamu. Basi akamwita bwana arusi kando, akamwambia, "Watu wote hutoa divai nzuri kwanza, kisha huleta ile divai hafifu wageni wakisha kunywa sana; lakini wewe umeiweka ile nzuri zaidi hadi sasa."
Huu ndio muujiza wa kwanza wa Isa; aliufanya huko Kana ya Galilaya. Hivyo Isa alidhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya.
Filipo akamjibu, "Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili hazitoshi kununua mikate ya kuwapa watu hawa ili kila mtu apate kidogo."
Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akamwambia, "Hapa kuna mvulana mmoja mwenye mikate mitano ya shayiri na samaki wawili wadogo. Lakini hivi vitatosha nini kwa watu hawa wote?"
Isa akasema, "Waketisheni watu chini." Palikuwa na majani mengi katika eneo lile, nao watu wakaketi (palikuwa na wanaume wapatao elfu tano). Ndipo Isa akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu na kuwagawia wale watu waliokuwa wameketi. Akafanya vivyo hivyo na wale samaki. Kila mtu akapata kadiri alivyotaka.
Watu wote walipokwisha kula na kushiba, akawaambia wanafunzi wake, "Kusanyeni vipande vilivyobaki vya ile mikate, kisipotee chochote." Hivyo wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili kwa vipande vya ile mikate mitano ya shayiri na samaki wale wawili wadogo vilivyobakishwa na waliokula.
Wanafunzi walipokuwa wameenda mwendo wa maili tatu au nne, walimwona Isa akitembea juu ya maji akikaribia mashua, nao wakaogopa sana. Lakini Isa akawaambia, "Ni mimi. Msiogope." Ndipo wakamkaribisha kwa furaha ndani ya mashua, na mara wakafika ufuoni walikokuwa wakienda.
Isa awatokea wanafunzi saba
Baada ya haya Isa akawatokea tena wanafunzi wake kando ya Bahari ya Tiberia. Yeye alijionesha kwao hivi: Simoni Petro, Tomaso (aitwaye Didimasi), Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo, na wanafunzi wengine wawili walikuwa pamoja. Simoni Petro akawaambia wenzake, "Mimi naenda kuvua samaki." Nao wakamwambia, "Tutaenda pamoja nawe." Wakatoka, wakaingia ndani ya mashua, lakini usiku ule hawakupata chochote.
Mara baada ya kupambazuka, Isa akasimama ufuoni, lakini wanafunzi hawakumtambua kwamba alikuwa Isa.
Isa akawaambia, "Wanangu, je, mna samaki wowote?"
Wakamjibu, "La."
Akawaambia, "Shusheni nyavu upande wa kuume wa mashua yenu nanyi mtapata samaki." Wakashusha nyavu, na tazama, wakapata samaki wengi mno hata wakashindwa kuvutia zile nyavu zilizojaa samaki ndani ya mashua.
Basi yule mwanafunzi aliyependwa na Isa akamwambia Petro, "Huyu ni Bwana Isa!" Simoni Petro aliposikia kwamba ni Bwana Isa, akajifunga nguo yake (kwa kuwa alikuwa ameitoa), naye akajitosa baharini. Wale wanafunzi wengine wakaja kwa ile mashua huku wakikokota ule wavu uliojaa samaki, maana hawakuwa mbali na nchi kavu, ilikuwa yapata dhiraa mia mbili. Walipofika ufuoni, wakaona moto wa makaa na samaki wakiokwa juu yake, na mikate.
Isa akawaambia, "Leteni baadhi ya hao samaki mliovua sasa hivi."
Simoni Petro akapanda kwenye mashua na kuukokota ule wavu ufuoni. Ulikuwa umejaa samaki wakubwa mia moja hamsini na watatu (153). Ingawa samaki walikuwa wengi kiasi hicho, ule wavu haukuchanika.
Libertações
Jesus expulsou demônios com autoridade. Os espíritos impuros não resistiam à sua palavra e saíam imediatamente.
Isa amponya mtumishi wa jemadari
Isa alipoingia Kapernaumu, jemadari mmoja alimjia, kumwomba msaada, akisema, "Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani na amepooza, tena ana maumivu makali ya kutisha."
Isa akamwambia, "Nitakuja na kumponya."
Lakini yule jemadari akamwambia, "Bwana, mimi sistahili wewe kuingia ndani ya nyumba yangu. Lakini sema neno tu, naye mtumishi wangu atapona. Kwa kuwa mimi mwenyewe ni mtu niliye chini ya mamlaka, nikiwa na askari chini yangu. Nikimwambia huyu, ‘Nenda,’ yeye huenda; na mwingine nikimwambia, ‘Njoo,’ yeye huja. Nikimwambia mtumishi wangu, ‘Fanya hivi,’ yeye hufanya."
Isa aliposikia maneno haya, alishangaa, akawaambia wale waliomfuata, "Amin, nawaambia, hata katika Israeli sijapata kuona yeyote mwenye imani kubwa namna hii. Ninawaambia kwamba wengi watatoka mashariki na magharibi, nao wataketi karamuni pamoja na Ibrahimu, Isaka na Yakobo katika ufalme wa mbinguni. Lakini warithi wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ambako kutakuwa kilio na kusaga meno."
Kisha Isa akamwambia yule jemadari, "Nenda na iwe kwako sawasawa na imani yako." Naye yule mtumishi akapona wakati ule ule.
Watu wawili wenye pepo wachafu waponywa
Walipofika ng’ambo katika nchi ya Wagerasi, watu wawili waliopagawa na pepo wachafu walitoka makaburini nao wakakutana naye. Watu hawa walikuwa wakali mno kiasi kwamba hakuna mtu aliyeweza kupita njia ile. Wakapaza sauti wakisema, "Una nini nasi, Mwana wa Mungu), wa kiroho, bali si wa kimwili.? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati ulioamriwa?"
Mbali kidogo kutoka pale walipokuwa, kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakila. Wale pepo wachafu wakamsihi Isa, "Ukitutoa humu, turuhusu twende kwenye lile kundi la nguruwe."
Akawaambia, "Nendeni!" Hivyo wakatoka na kuwaingia wale nguruwe, nalo kundi lote likateremka gengeni kwa kasi, likaingia katika ziwa na kufa ndani ya maji. Wale watu waliokuwa wakiwachunga hao nguruwe wakakimbia wakaingia mjini, wakaeleza yote yaliyowatokea wale waliokuwa wamepagawa na pepo wachafu. Kisha watu wote wa mji huo wakatoka kwenda kukutana na Isa. Nao walipomwona wakamsihi aondoke kwenye nchi yao.
Isa amponya bubu
Walipokuwa wanatoka, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu na ambaye hakuweza kuongea aliletwa kwa Isa. Yule pepo mchafu alipotolewa, yule mtu aliyekuwa bubu akaongea, na umati wa watu wakastaajabu na kusema, "Jambo kama hili kamwe halijapata kuonekana katika Israeli."
Isa na Beelzebuli
Kisha wakamletea mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, na alikuwa kipofu na bubu. Isa akamponya, hata akaweza kusema na kuona.
Imani ya mwanamke Mkanaani
Isa aliondoka mahali pale, akaenda sehemu za Tiro na Sidoni. Mwanamke mmoja Mkanaani aliyeishi sehemu jirani na hizo akaja kwake akilia, akasema, "Nihurumie, Ee Bwana, Mwana wa Daudi).! Binti yangu amepagawa na pepo mchafu, na anateseka sana."
Lakini Isa hakumjibu neno. Hivyo wanafunzi wake wakamwendea na kumsihi sana, wakisema, "Mwambie aende zake, kwa maana anaendelea kutupigia kelele."
Isa akajibu, "Nimetumwa tu kwa ajili ya kondoo wa Israeli waliopotea."
Lakini yule mwanamke akaja, akapiga magoti mbele ya Isa, akasema, "Bwana, nisaidie!"
Isa akajibu, "Si haki kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."
Yule mwanamke akajibu, "Ndiyo, Bwana, lakini hata mbwa hula makombo yanayoanguka kutoka kwa meza za bwana zao."
Ndipo Isa akamwambia, "Mwanamke, imani yako ni kubwa! Iwe kwako kama unavyotaka." Naye binti yake akapona tangu saa ile.
Isa amponya kijana mwenye pepo mchafu
Walipofika penye umati wa watu, mtu mmoja akamjia Isa na kupiga magoti mbele yake, akasema, "Bwana, mhurumie mwanangu. Yeye ana kifafa na anateseka sana. Mara kwa mara huanguka kwenye moto au kwenye maji. Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya."
Isa akajibu, "Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka! Nitakaa nanyi hadi lini? Nitawavumilia hadi lini? Mleteni mvulana hapa kwangu." Isa akamkemea yule pepo mchafu, akamtoka yule kijana, naye akapona tangu saa hiyo.
Wakati huo huo katika sinagogi lao palikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, naye akapaza sauti akisema, "Tuna nini nawe, Isa Al-Nasiri? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu!"
Lakini Isa akamkemea, akamwamuru, "Nyamaza! Mtoke mtu huyu!" Yule pepo mchafu akamgaragaza huyo mtu kwa nguvu, kisha akamtoka akipiga kelele kwa sauti kubwa.
Isa amponya mtu mwenye pepo mchafu
Isa na wanafunzi wake wakafika upande wa pili wa ziwa, wakaingia katika nchi ya Wagerasi. Isa alipotoka kwenye mashua, mara mtu mmoja mwenye pepo mchafu akatoka makaburini, akakutana naye. Mtu huyu aliishi makaburini, wala hakuna aliyeweza kumzuia hata kwa kumfunga minyororo. Kwa kuwa mara kwa mara alikuwa amefungwa minyororo mikononi na miguuni, lakini akaikata hiyo minyororo na kuzivunja zile pingu miguuni mwake. Hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa na nguvu za kumzuia. Usiku na mchana alikuwa makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe.
Alipomwona Isa kwa mbali, alimkimbilia, akapiga magoti mbele yake. Akapaza sauti kwa nguvu akisema, "Una nini nami, Isa, Mwana wa Mungu), wa kiroho, bali si wa kimwili. Aliye Juu Sana? Ninakusihi kwa jina la Mungu, usinitese!" Kwa kuwa Isa alikuwa amemwambia, "Mtoke mtu huyu, wewe pepo mchafu!"
Isa akamuuliza, "Jina lako ni nani?"
Akamjibu, "Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tuko wengi." Akamsihi Isa sana asiwapeleke nje ya nchi ile.
Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe lililokuwa likilisha karibu kando ya kilima. Wale pepo wachafu wakamsihi Isa wakisema, "Tuamuru twende kwenye wale nguruwe. Turuhusu tuwaingie." Basi Isa akawaruhusu, nao wale pepo wachafu wakatoka, wakawaingia hao nguruwe. Lile kundi lilikuwa na nguruwe wapatao elfu mbili, nao wote wakateremkia gengeni kwa kasi, nao wakatumbukia ziwani na kuzama.
Wale watu waliokuwa wakichunga hao nguruwe wakakimbilia mjini na vijijini kueleza yaliyotukia. Watu wakaenda kuona hayo yaliyokuwa yametukia.
Lakini ninyi mwafundisha kwamba mtu akimwambia baba yake au mama yake, ‘Kile ambacho ningeweza kukusaidia ni Korbani’ (yaani kimewekwa wakfu kwa Mungu), basi hawajibiki tena kumsaidia baba yake au mama yake. Kwa njia hiyo ninyi mnabatilisha neno la Mungu kwa mapokeo yenu mliyojiwekea. Nanyi mnafanya mambo mengi ya aina hiyo."
Vitu vinavyomnajisi mtu
Isa akaita tena umati ule wa watu, akawaambia, "Nisikilizeni nyote, na mwelewe jambo hili. Hakuna kitu kinachomwingia mtu kimtiacho unajisi, lakini kile kimtokacho ndicho kimtiacho unajisi. [
Imani ya mwanamke Myunani
Ndipo Isa akaondoka hapo akaenda sehemu za Tiro. Akaingia katika nyumba moja, naye hakutaka mtu yeyote ajue kwamba yuko humo. Lakini hakuweza kujificha. Mara mwanamke mmoja, ambaye binti yake mdogo alikuwa na pepo mchafu, akaja na kumpigia magoti miguuni pake. Basi huyo mwanamke alikuwa Myunani, aliyezaliwa Foinike ya Siria. Akamsihi Isa amtoe binti yake huyo pepo mchafu.
Isa akamwambia, "Waache watoto washibe kwanza, kwa maana si vyema kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa."
Lakini yule mwanamke akamjibu, "Bwana, hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya chakula cha watoto."
Ndipo Isa akamjibu, "Kwa sababu ya jibu lako, nenda zako nyumbani; yule pepo mchafu amemtoka binti yako."
Akaenda zake nyumbani akamkuta binti yake amelala kitandani, yule pepo mchafu akiwa amemtoka.
Mtu mmoja miongoni mwa umati ule wa watu akajibu, "Mwalimu, nilimleta kwako mwanangu ambaye ana pepo mchafu anayemfanya asiweze kuongea. Kila mara huyo pepo mchafu ampagaapo mwanangu, humwangusha chini na kumfanya atokwe povu mdomoni na kusaga meno, kisha mwili wake hukauka. Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo mchafu, lakini hawakuweza."
Isa akawaambia, "Enyi kizazi kisichoamini! Nitakuwa pamoja nanyi hadi lini? Nitawavumilia hadi lini? Mleteni mvulana kwangu."
Nao wakamleta yule mvulana. Yule pepo mchafu alipomwona Isa, mara akamtia yule mvulana kifafa, akaanguka, akagaagaa chini huku akitokwa na povu kinywani.
Isa akamuuliza baba yake, "Mwanao amekuwa katika hali hii tangu lini?"
Akamjibu, "Tangu utoto wake. Mara kwa mara huyo pepo mchafu amekuwa akimwangusha kwenye moto au kwenye maji ili kumwangamiza. Lakini kama unaweza kufanya jambo lolote, tafadhali tuhurumie utusaidie."
Isa akamwambia, "Ati, ‘Kama unaweza kufanya jambo lolote’? Yote yawezekana kwake yeye aaminiye."
Mara baba yake yule mvulana akapaza sauti akisema, "Ninaamini. Nisaidie kutokuamini kwangu!"
Isa alipoona kwamba umati wa watu wanakusanyika pamoja mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akimwambia, "Wewe pepo bubu na kiziwi, nakuamuru umtoke, wala usimwingie tena!"
Baada ya yule pepo mchafu kupiga kelele, akamtia kifafa kwa nguvu, akamtoka. Yule mvulana alikuwa kama maiti, hivyo watu wengi wakasema, "Amekufa." Lakini Isa akamshika mkono, akamwinua, naye akasimama.
Isa amponya mama mkwe wa Simoni na pia watu wengi
Isa akatoka katika sinagogi, akaenda nyumbani mwa Simoni. Basi huko alimkuta mama mkwe wa Simoni akiwa ameshikwa na homa kali, nao wakamwomba Isa amsaidie. Hivyo Isa akamwinamia na kukemea ile homa, nayo ikamwacha. Akaamka mara moja, naye akaanza kuwahudumia.
Isa aliposhuka kutoka mashua na kukanyaga ufuoni, alikutana na mtu mmoja wa mji ule aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, naye kwa muda mrefu alikuwa havai nguo wala kuishi nyumbani, bali aliishi makaburini. Alipomwona Isa, alipaza sauti, akajitupa chini mbele yake na kusema kwa sauti kuu, "Una nini nami, Isa, Mwana wa Mungu), wa kiroho, bali si wa kimwili. Aliye Juu Sana? Nakuomba, usinitese!" Wakati huo Isa alikuwa amemwamuru yule pepo mchafu amtoke huyo mtu. Mara nyingi huyo pepo mchafu alimpagaa, na hata alipofungwa kwa minyororo mikono na miguu na kuwekwa chini ya ulinzi, alikata hiyo minyororo na kupelekwa na huyo pepo mchafu kwenda nyikani.
Isa akamuuliza, "Jina lako ni nani?"
Akamjibu, "Legioni," kwa kuwa alikuwa ameingiwa na pepo wachafu wengi mno. Wale pepo wachafu wakamsihi sana asiwaamuru kwenda katika Shimo.
Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe hapo likilisha kando ya kilima. Wale pepo wachafu wakamsihi Isa awaruhusu wawaingie hao nguruwe, naye akawaruhusu. Wale pepo wachafu walipomtoka yule mtu, wakawaingia wale nguruwe, nalo kundi lote likateremkia gengeni kwa kasi, likatumbukia ziwani na kuzama.
Wale watu waliokuwa wakichunga lile kundi la nguruwe walipoona yaliyotukia, wakakimbia, wakaeneza habari hizi mjini na mashambani. Nao watu wakatoka kwenda kujionea wenyewe yaliyotukia. Walipofika hapo alipokuwa Isa, wakamkuta yule mtu aliyetokwa na pepo wachafu amekaa karibu na Isa, akiwa amevaa nguo na mwenye akili timamu! Wakaogopa.
"Amin, nawaambia, wako baadhi ya watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona ufalme wa Mungu."
Isa abadilika sura
Yapata siku nane baada ya Isa kusema hayo, aliwachukua Petro, Yohana na Yakobo, akaenda nao mlimani kuomba. Alipokuwa akiomba, sura ya uso wake ikabadilika, nayo mavazi yake yakametameta kama miali ya radi. Ghafula wakawaona watu wawili, ndio Musa na Ilya, wakizungumza naye. Walionekana katika utukufu wakizungumza na Isa kuhusu kifo chake ambacho kingetokea huko Yerusalemu.
Petro na wenzake walikuwa wamelala usingizi mzito. Walipoamka, wakaona utukufu wa Isa na wale watu wawili waliokuwa wamesimama pamoja naye. Musa na Ilya walipokuwa wanaondoka, Petro akamwambia Isa, "Bwana, ni vizuri tukae hapa! Tutajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kingine cha Musa na kingine cha Ilya." Lakini Petro hakujua alichosema.
Mtu mmoja katika umati ule akapaza sauti, akasema, "Mwalimu, naomba umwangalie mwanangu, kwani ndiye mtoto wangu wa pekee. Mara kwa mara pepo mchafu humpagaa na kumfanya apige mayowe, kisha humwangusha na kumtia kifafa hata akatokwa na povu kinywani. Huyo pepo mchafu anamtesa sana, na hamwachi ila mara chache. Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo mchafu, lakini hawakuweza."
Isa akawajibu, "Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka! Nitakaa nanyi na kuwavumilia hadi lini? Mlete mwanao hapa."
Hata yule mtoto alipokuwa akija, yule pepo mchafu akamwangusha, akamtia kifafa. Lakini Isa akamkemea yule pepo mchafu amtoke, akamponya yule mtoto, na akamrudisha kwa baba yake. Watu wote wakastaajabia uweza mkuu wa Mungu.
Wakati bado watu walikuwa wanastaajabia hayo yote aliyokuwa akiyafanya Isa, yeye akawaambia wanafunzi wake:
Isa na Beelzebuli
Basi Isa alikuwa anamtoa pepo mchafu kutoka kwa mtu aliyekuwa bubu. Yule pepo mchafu alipomtoka yule mtu aliyekuwa bubu, akaanza kuongea, nao umati wa watu wakashangaa.
Mmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu kwa upanga, akamkata sikio la kuume.
Lakini Isa akasema, "Acheni!" Akaligusa lile sikio la yule mtu na kumponya.
Wajumbe wa Yahya walipoondoka, Isa akaanza kusema na umati wa watu kuhusu Yahya. Akawauliza, "Mlipoenda kule nyikani, mlienda kuona nini? Je, ni unyasi ukipeperushwa na upepo? Kama sivyo, mlienda kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi ya kifahari? La hasha! Watu wanaovaa mavazi ya kifahari na kuishi maisha ya anasa wako katika majumba ya kifalme. Lakini mlienda kuona nini? Mlienda kumwona nabii? Naam, nawaambia, yeye ni zaidi ya nabii. Huyu ndiye ambaye habari zake zimeandikwa:
" ‘Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako,
atakayetengeneza njia mbele yako.’
Nawaambia, miongoni mwa wale waliozaliwa na wanawake, hakuna aliye mkuu kuliko Yahya. Lakini yeye aliye mdogo kabisa katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko Yahya."
(Watu wote, hata watoza ushuru, waliposikia maneno ya Isa, walikubali kwamba mpango wa Mungu ni haki, maana walikuwa wamebatizwa na Yahya. Lakini Mafarisayo na wataalamu wa Torati walikataa mpango wa Mungu kwao kwa kutokubali kubatizwa na Yahya.)