Morte
A morte é a realidade que todos enfrentam, mas para o cristão ela não é o fim. A Bíblia ensina que Cristo venceu a morte e nos dá a esperança da ressurreição e da vida eterna.
Cristo venceu a morte
Onde está, ó morte, o teu aguilhão? Cristo destruiu o poder da morte e nos deu a vitória pela ressurreição.
"Kuko wapi, ee mauti, kushinda kwako?
Uko wapi, ee mauti, uchungu wako?"
Uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu ya dhambi ni sheria. Lakini Mungu apewe shukrani, yeye atupaye ushindi kupitia kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi.
Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni mauti.
Kwa maana kama vile mauti ilivyokuja kupitia kwa mtu mmoja, vivyo hivyo, ufufuo wa wafu umekuja kupitia kwa mtu mmoja.
Kwa maana kama vile katika Adamu watu wote wanakufa, vivyo hivyo katika Al-Masihi wote watafanywa hai.
Hili ni neno la kuaminiwa:
Kama tumekufa pamoja naye,
tutaishi pia pamoja naye.
Waliobarikiwa na walio watakatifu ni wale walio na sehemu katika ufufuo wa kwanza. Hao mauti ya pili haina nguvu juu yao, bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Al-Masihi, nao watatawala pamoja naye kwa muda wa miaka elfu.
A esperança da vida eterna
Jesus disse: 'Eu sou a ressurreição e a vida.' Quem crê nele não está morto, mas apenas adormecido — e um dia despertará para a glória.
Isa akamwambia, "Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi; na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?"
Isa akamwambia, "Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi; na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?"
Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata. Nami ninawapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe, wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka mikono yangu.
"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Kurudi kwake Bwana Isa
Lakini ndugu, hatutaki mkose kujua kuhusu wale waliolala katika mauti, ili msihuzunike kama watu wengine wasiokuwa na tumaini. Tunaamini kwamba Isa alikufa na kufufuka. Na kwa hivyo, tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja naye wale waliolala katika Isa.
Kwa maana Bwana Isa mwenyewe atashuka kutoka mbinguni, akitoa amri kwa sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, na sauti ya tarumbeta ya Mungu. Nao waliokufa wakiwa katika Al-Masihi watafufuka kwanza. Baada ya hilo sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu ili kumlaki Bwana Isa hewani, hivyo tutakuwa pamoja na Bwana Isa milele.
Não temas a morte
Não temas os que matam o corpo. Para o cristão, viver é Cristo e morrer é lucro. O vale da sombra da morte não assusta quem caminha com o Pastor.
Msiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho. Afadhali mwogopeni yeye awezaye kuiangamiza roho na mwili katika Jehanamu.
Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata.
Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Al-Masihi, na kufa ni faida.
Ninavutwa kati ya mambo mawili: Ninatamani kuondoka nikakae pamoja na Al-Masihi, jambo hilo ni bora zaidi. Lakini kwa sababu yenu ni muhimu zaidi mimi nikiendelea kuishi katika mwili.
Lakini uenyeji wetu uko mbinguni. Nasi tunamngoja kwa shauku Mwokozi kutoka huko, yaani Bwana Isa Al-Masihi, atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, ili upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote chini yake.
Hata nikipita katikati
ya bonde la uvuli wa mauti,
sitaogopa mabaya,
kwa maana wewe upo pamoja nami;
fimbo yako na mkongojo wako
vyanifariji.
Hata nikipita katikati
ya bonde la uvuli wa mauti,
sitaogopa mabaya,
kwa maana wewe upo pamoja nami;
fimbo yako na mkongojo wako
vyanifariji.
Kama tunaishi, tunaishi kwa Mwenyezi Mungu, nasi pia tukifa tunakufa kwa Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo basi, kama tukiishi au kama tukifa, sisi ni mali ya Mwenyezi Mungu.
A eternidade nos aguarda
Deus enxugará toda lágrima. A morte será o último inimigo destruído. Para os salvos, a morte é a porta de entrada na presença eterna de Deus.
Nami nikasikia sauti kubwa kutoka kile kiti cha enzi ikisema, "Sasa makao ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atakaa pamoja nao. Yeye atakuwa Mungu wao nao watakuwa watu wake, naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Atafuta kila chozi kutoka macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita."
Atafuta kila chozi kutoka macho yao. Mauti haitakuwepo tena, wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu, kwa maana mambo ya kwanza yamekwisha kupita."
Kama vile mwanadamu alivyowekewa kufa mara moja tu na baada ya kufa akabili hukumu,
Kwa maana nimekwisha kujua kwa hakika ya kuwa sio mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuja, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kingine chochote zitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Al-Masihi Isa, Bwana wetu.
Hakika, ni vigumu mtu yeyote kufa kwa ajili ya mwenye haki, ingawa inawezekana mtu akathubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema. Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Al-Masihi alikufa kwa ajili yetu.
Kwa maana ikiwa kutokana na kosa la mtu mmoja, mauti ilitawala kupitia huyo mtu mmoja, zaidi sana wale wanaopokea wingi wa neema ya Mungu na karama yake ya kuhesabiwa haki, watatawala katika uzima kupitia kwa huyo mtu mmoja, yaani Isa Al-Masihi.
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Al-Masihi Isa Bwana wetu.
A morte na perspectiva bíblica
Há tempo de nascer e tempo de morrer. A morte é realidade humana, mas Deus é Senhor tanto dos vivos quanto dos mortos.
Hekima
Afadhali sifa nzuri kuliko manukato safi,
nayo siku ya kufa kuliko ya kuzaliwa.
Wale wanaoenda kwa unyofu
huwa na amani;
hupata pumziko wanapolala mautini.
Watu wanaotembea katika giza
wameona nuru kuu,
wale wanaoishi katika nchi ya uvuli wa mauti,
nuru imewazukia.
lakini kamwe usile matunda ya mti wa kujua mema na mabaya, kwa maana siku utakapokula matunda yake, hakika utakufa."
Ni mtu gani awezaye kuishi na asione kifo,
au kujiokoa mwenyewe kutoka nguvu za kaburi?
Niende wapi nijiepushe na Roho yako?
Niende wapi niukimbie uso wako?
Nikienda juu mbinguni, wewe uko huko;
nikifanya vilindi kuwa kitanda changu,
wewe uko huko.
Nitie kama muhuri moyoni mwako,
kama muhuri kwenye mkono wako;
kwa maana upendo una nguvu kama mauti,
wivu wake ni mkatili kama Kuzimu.
Unachoma kama mwali wa moto,
kama mwali mkubwa wa moto wa Mwenyezi Mungu hasa.
"Sasa mimi ninakaribia kwenda katika njia ya watu wote wa dunia. Mnajua kwa mioyo yenu na roho zenu kwamba hakuna ahadi zozote njema Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, alizowaahidia, ambazo hazikutimia. Kila ahadi imetimizwa, hakuna hata moja ambayo haikutimia.
Kwa maana sifurahii kifo cha mtu yeyote, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Tubuni basi, mkaishi!
Isa akapaza sauti yake akasema, "Baba, mikononi mwako naikabidhi roho yangu." Baada ya kusema haya, akakata roho.
Kule Kuzimu alipokuwa akiteseka, alitazama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali, naye Lazaro alikuwa kifuani mwake. Hivyo yule tajiri akamwita, ‘Baba Ibrahimu, nihurumie na umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake ndani ya maji aupoze ulimi wangu, kwa sababu nina maumivu makuu kwenye moto huu.’
Basi ile tamaa mbaya ikishachukua mimba huzaa dhambi, nayo ile dhambi ikikomaa huzaa mauti.